Kodi, ushuru na tozo za Tanzanua ni kero kubwa

Kodi, ushuru na tozo za Tanzanua ni kero kubwa

Cha kuchekesha humu Jf tutachekana ila behind keyboards kila mtu anajua kinachomuweka mjini. Mi nimewasilisha hoja wahusika wanapita watasoma. Wakistaafu watoto wao watakuja kuwaambia haya na watatamani wangeyafanya haya kipindi wakiwa madarakani ila mda huo ni too late so vizazi vinaendelea kusota.
Taja hzo tozo ambazo unaona unaonewa, pia umemskia mzee magufuli?? We lala [emoji28]
 
Habari Wanajamvi. Kuna tatizo kubwa Tanzania ambalo tusipoliongelea litatufikisha pabaya kama wananchi na kunufaisha serikali. Hivi kijana unahitimu chuo, siku ya mahafali, wageni rasmi ambao ni wenye wadhifa mkubwa kama spika wa bunge n.k. Anashika mic na kusema wahitimu mjiajiri huku mkijiangalia mko zaidi ya maelfu. Sawa unasema nisikae bure nyumbani ngoja nitafute namna nijiajiri. ume save ka ela kako kadogo ili ufungue hata biashara ya kukuingizia walau elfu mbili faida kwa siku unajikuta hela yote imeishia kwenye kodi kabla hata hujafungua hiyo Biashara yenyewe. Faida unaanza kuiona baada ya miezi kadhaa. Naongea kama mhanga wa hili jambo TRA mnatukaba sana sijui wengine wanaosota zaidi yangu wana survive vipi ila tusipo lisemea hili tutaisha. Na sijui kama liliwahi kuongelewa kwenye kampeni kwa raia mliopo karibu naMhe Rais jamani hali ni mbaya mtaani. Yaani TRA wanatamani wapite na majumbani mwa watu watoze kodi za vichwa. Hapo sijagusia ushuru wala tozo zingine maana thread haitaisha ila ni TOO MUCH[emoji1430].
Tuliwaambia njoo tuandamane mkatuona sisi wachochezi
 
Kabla sijaanzisha biashara yoyote nitamtafuta mtaalamu wa Kodi anipe shule nielewe kila kitu kabla sijaanza hatua ya kwanza.

Naona kuna shida watu wanaanza tu hatua then wakifikisha hatua ya 8/10 wanakuja kujua kuna mambo mazito ambayo angejua mwanzo asingeendelea na mchakato
 
Ushuru wa taka ushuru wa ulinzi shirikishi kodi TRA kodi ya pango.dawasa miter zao zinaenda mwendo kasi.umeme unanunua unakatwa rea.kazi ajira hakuna, vitu bei juu cement mafuta sukari nk. Biashara hakuna.nitakosaje kupata pressure na heart attack. Kila siku watu wanaondoka wanafariki kwa prressure ee mungu tuokoe
 
Ndugu yangu, bishara nliyokua naifanya ni ya vitu vidogo vidogo tu vya kawaida nikasema haya maisha ya kushinda unategemea hela za kupewa siyataki acha nijipambanie mwenyewe. Trailer likaanza nazunguka manispaa sijui TRA sijui mjumbe kutafuta vibali etc, kodi nishalipa kila kitu nilisota na wanakwambia ulipe ile Tax clearance hata duka halijaanza yani mtu angenisimulia ningebisha ila nilijionea mwenyewe. Majukumu yalinizidi kodi ikawa inaenda kila siku wanaleta kodi mpya mara premise registration kama unauza chakula yani mlolongo nikaamua kufunga duka kwanza niheme nijipange upya ndo nirudi. Jamani TRA msipokuja na majibu ya haya maswala nitaleta barua mwenyewe ofisini kwenu. Kuna watu wanasota sana huko mtaani. Sijui mnataka tuishije tunafanya kazi bila kuangalia jinsia ili mradi usiwe tegemeo kwa mzazi ila mnatuvunja sana moyo. Sana
Kama umefunga biashara fanya uwataarifu ili waweke rekodi zao sawa ili baadaye usije lia peke yako!
 
Hailipiwi hio mzee ni free angalia chini kabisa imeandikwa “issued free of charge”
Tax Clearance ni bure lakin huwezi kuipata mpaka at least uwe umelipia quarter 1 au zaidi kadiri ya kodi uliyokadiriwa.
 
Ni kweli hali mbaya sana TRA na manispaa wanaua biashara za wajasilia Mali

Kuna mdada alimaliza chuo akafungua kabiashara kake akaenda akapata tin na lesene mwaka ukaisha akashindwa kurinuu leseni yake manispaa wakapita wakamkamata

Kule manispaa akakuta anadaiwa leseni elfu 80 na service Levy elfu 50 inabidi aanzie TRA nako wanataka 130000/=

Jumla 260000/= kwa kweli ukiangalia hicho kiduka ndani yake kuna vijuice maji na vocha kama akilipa hiyo kodi basi na biashara inakua imeishia hapo

Sasa kitu ambacho kimenishangaza ni hiki Mimi ambae sina taaruma yoyote ya ukusanyaji wa kodi nikiifanyia tathimini ile biashara naona kabisa haina uwezo wa kulipa hizo kodi

Je! Wao wanapoenda dukani kwa mjasilia Mali kwa nini hawafanyi hiyo tathimini ili kuona kama hiyo biashara ina uwezo huo au haina na kama haina wamuache ili ajijenge wamfuate tena baada ya mwaka mmoja

Ila wao kigezo chao kama unabishara ndani ya flemu basi haijalishi ni lazima tu ulipe kodi

Nilicho gundua kusoma na kuelimika ni vitu viwili tofauti na watanzania huwa wanasoma lakini hawaelimiki
 
Hailipiwi hio mzee ni free angalia chini kabisa imeandikwa “issued free of charge”
Mungu wangu ni shahidi. Niliilipa na hadi leo stakabadhi ninayo. Nilipofika pale nilijaribu sana kueleweshwa hilo swala wakasema hapana lazima ulipe ndo upewe. Tena ilikua kama 83,333 kwa miezi mitatu. Ni wajeuri wale wadada tena ukikuta foleni ndo hata hakuangalii usoni. Anakwambia kalipe urudi kwenye foleni dada sogea nihudumie wengine. Wengi hawajui kama Biashara mpya haulipi. Mimi nimekuja kujua baada ya kufungua biashara. Tatizo lipo kubwa na TRA WANAJUA
Hamjaelewana. Champagnee Alielipa kalipa makadirio ya kodi sio kwamba kalipia tax clearance.
 
Habari Wanajamvi. Kuna tatizo kubwa Tanzania ambalo tusipoliongelea litatufikisha pabaya kama wananchi na kunufaisha serikali. Hivi kijana unahitimu chuo, siku ya mahafali, wageni rasmi ambao ni wenye wadhifa mkubwa kama spika wa bunge n.k. Anashika mic na kusema wahitimu mjiajiri huku mkijiangalia mko zaidi ya maelfu. Sawa unasema nisikae bure nyumbani ngoja nitafute namna nijiajiri. ume save ka ela kako kadogo ili ufungue hata biashara ya kukuingizia walau elfu mbili faida kwa siku unajikuta hela yote imeishia kwenye kodi kabla hata hujafungua hiyo Biashara yenyewe. Faida unaanza kuiona baada ya miezi kadhaa. Naongea kama mhanga wa hili jambo TRA mnatukaba sana sijui wengine wanaosota zaidi yangu wana survive vipi ila tusipo lisemea hili tutaisha. Na sijui kama liliwahi kuongelewa kwenye kampeni kwa raia mliopo karibu naMhe Rais jamani hali ni mbaya mtaani. Yaani TRA wanatamani wapite na majumbani mwa watu watoze kodi za vichwa. Hapo sijagusia ushuru wala tozo zingine maana thread haitaisha ila ni TOO MUCH🙌🏽.
Toa mapendekezo yako mkuu
 
Subiri january ifike muone mziki wake .
Si mmeshaona hadi wafuga kuku wanatakiwa kibali?sasa kodi ya kichwa na ushuru wa baiskel unakuja na ole wako uko na kibaskel chako hakina stika uone
 
Back
Top Bottom