Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,547
- 7,167
Kwenu jukwaani.
Hivi karibuni kila halmashauri humu nchini imekuwa ikibuni vyanzo vya mapato. Baadhi zimeenda mbali kwa kupendekeza tozo ya Tsh 50,000 kwa kibali cha sherehe kama harusi, birthday/bethidei, send off nk.
Habari kutoka chanzo changu cha uhakika jikoni kabisa serikalini, kimedai Rais Magufuli ataibuka mapema mwezi ujao wa February na kukataza kodi hizi.
Chanzo hiki kimedai kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu kote nchini umekuwa chanzo cha kufutwa kwa kodi hii iliyobuniwa na watendaji ili kukuza mapato ktk halmashauri.
Chanzo hicho jikoni serikalini kimedai CCM na serikali hawataki na hawapo tayari kwa mzozo wowote na wananchi mwaka huu na hata vitendo vya bomoabomoa huenda nazo zikakomeshwa kwa muda.