Tetesi: Kodi ya kibali cha harusi, birthday, send off, ubatizo, kumtoa mwali kufutwa mapema na Rais Magufuli

Tetesi: Kodi ya kibali cha harusi, birthday, send off, ubatizo, kumtoa mwali kufutwa mapema na Rais Magufuli

Hizo kodi za harusi na misiba zimeanza lini na wapi jamani? Halafu wamesahau graduation kuanzia chekechea, la Saba, fomfoo, fomsksi, stakishahada, shahada, pihechidi, zamivu, zawizi, zawivu, na kwa wingi wa shule, seminari, na vyuo mpaka vya kodi! Na vya polisi, geshi, magareza, mahakimu, manesi, wakunga, waganga wa kienyeji, wainjilisiti, mapadiri, arobaini, manyamapori, na kazalika! Mweh!
Tarehe moja February zimeanza kwa halmashauri moja ya jiji la Dar
 
Ni sawa tu. Inatakiwa ukienda pale daraja la kigamboni kupita picha wakati wa sherehe yako ya harusi au wakati wowote ulipe pia. Mbona kwingine tunalipa.
Kwenu jukwaani.

Hivi karibuni kila halmashauri humu nchini imekuwa ikibuni vyanzo vya mapato. Baadhi zimeenda mbali kwa kupendekeza tozo ya Tsh 50,000 kwa kibali cha sherehe kama harusi, birthday/bethidei, send off nk.

Habari kutoka chanzo changu cha uhakika jikoni kabisa serikalini, kimedai Rais Magufuli ataibuka mapema mwezi ujao wa February na kukataza kodi hizi.

Chanzo hiki kimedai kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu kote nchini umekuwa chanzo cha kufutwa kwa kodi hii iliyobuniwa na watendaji ili kukuza mapato ktk halmashauri.

Chanzo hicho jikoni serikalini kimedai CCM na serikali hawataki na hawapo tayari kwa mzozo wowote na wananchi mwaka huu na hata vitendo vya bomoabomoa huenda nazo zikakomeshwa kwa muda.
 
Ni sawa tu. Inatakiwa ukienda pale daraja la kigamboni kupita picha wakati wa sherehe yako ya harusi au wakati wowote ulipe pia. Mbona kwingine tunalipa.
Ndiyo hivyo Jemedari anaifuta
 
Back
Top Bottom