Tetesi: Kodi ya kibali cha harusi, birthday, send off, ubatizo, kumtoa mwali kufutwa mapema na Rais Magufuli

Tetesi: Kodi ya kibali cha harusi, birthday, send off, ubatizo, kumtoa mwali kufutwa mapema na Rais Magufuli

Wanawatuma watangaze kodi ambazo ni kero harafu wao wenyewe wanakuja kuzifuta...
 
Wanawatuma watangaze kodi ambazo ni kero harafu wao wenyewe wanakuja kuzifuta...
 
Kwenu jukwaani.

Hivi karibuni kila halmashauri humu nchini imekuwa ikibuni vyanzo vya mapato. Baadhi zimeenda mbali kwa kupendekeza tozo ya Tsh 50,000 kwa kibali cha sherehe kama harusi, birthday/bethidei, send off nk.

Habari kutoka chanzo changu cha uhakika jikoni kabisa serikalini, kimedai Rais Magufuli ataibuka mapema mwezi ujao wa February na kukataza kodi hizi.

Chanzo hiki kimedai kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu kote nchini umekuwa chanzo cha kufutwa kwa kodi hii iliyobuniwa na watendaji ili kukuza mapato ktk halmashauri.

Chanzo hicho jikoni serikalini kimedai CCM na serikali hawataki na hawapo tayari kwa mzozo wowote na wananchi mwaka huu na hata vitendo vya bomoabomoa huenda nazo zikakomeshwa kwa muda.

Kwahiyo tukihisi labda huyo ambaye umemtaja ataibuka Siku si nyingi kutengua hayo maamuzi ndiyo Yeye aliyelitengeneza na hapa anatafuta tu turufu ya Kisiasa kwa Wananchi tutakuwa tunakosea au tunamsingizia?
 
Hizo kodi za harusi na misiba zimeanza lini na wapi jamani? Halafu wamesahau graduation kuanzia chekechea, la Saba, fomfoo, fomsksi, stakishahada, shahada, pihechidi, zamivu, zawizi, zawivu, na kwa wingi wa shule, seminari, na vyuo mpaka vya kodi! Na vya polisi, geshi, magareza, mahakimu, manesi, wakunga, waganga wa kienyeji, wainjilisiti, mapadiri, arobaini, manyamapori, na kazalika! Mweh!
 
Tatizo ni ule uvivu wa kufikiri wa hawa watu wa Halmashauri na viongozi wengine, mbona sehemu za kukusanya kodi ni nyingi tu, tukianza na:-
  • Faini kwa kutupa taka hovyo
  • Vile vibanda vya kupiga simu kama zamani vya TTCL
  • Kutoa mifuko ya kijani kwa kila nyumba ili chupa za plastic au bidhaa za plastic viwe vinakusanywa, wao inakuwa collection tu..
  • Kutoa huduma za "Removal Services", yaani ukitaka kuhama au kubebewa vitu nyumbani waitwe wao na malori au ma-Cante yao..
  • Wajenge nyumba za kukodisha...
  • Wawe na mabasi ya usafirishaji raia..
  • Watoe huduma za kulipia kwenye ushauri wa kibiashara, ujengaji, afya na ustawi wa jamii..
  • ...
Je wako humu wasikie yetu?!
 
wasiwasi wangu ni kuwa hata hivi vitambulisho hivi vya wajasiriamali baadae vikionekana vinawazuia machinga kufanya biashara navyo vitafutwa
 
hivi maumivu ya hizo kodi na makato ya cat katika vocha na luku yepi yanaawagusa walio wengi tena wanyonge
 
Tatizo ni ule uvivu wa kufikiri wa hawa watu wa Halmashauri na viongozi wengine, mbona sehemu za kukusanya kodi ni nyingi tu, tukianza na:-
  • Faini kwa kutupa taka hovyo
  • Vile vibanda vya kupiga simu kama zamani vya TTCL
  • Kutoa mifuko ya kijani kwa kila nyumba ili chupa za plastic au bidhaa za plastic viwe vinakusanywa, wao inakuwa collection tu..
  • Kutoa huduma za "Removal Services", yaani ukitaka kuhama au kubebewa vitu nyumbani waitwe wao na malori au ma-Cante yao..
  • Wajenge nyumba za kukodisha...
  • Wawe na mabasi ya usafirishaji raia..
  • Watoe huduma za kulipia kwenye ushauri wa kibiashara, ujengaji, afya na ustawi wa jamii..
  • ...
Je wako humu wasikie yetu?!
hayo hufanywa na sekta binfsi sio kwa gvt hii hata hivyo mazingira magumu yaliyopo nchi itakuwa ngumu
 
Kwahiyo tukihisi labda huyo ambaye umemtaja ataibuka Siku si nyingi kutengua hayo maamuzi ndiyo Yeye aliyelitengeneza na hapa anatafuta tu turufu ya Kisiasa kwa Wananchi tutakuwa tunakosea au tunamsingizia?
Cha maana wewe ujue tu kodi ataifuta.
 
Kwa ninavyomjua Jiwe atapita humo humo ulipoandika, wewe ngoja tuendelee kupiga kelele halafu yule jamaa kwa kupenda sifa atakuja na kuifuta hiyo kodi ili aonekane ni shujaa na mtetezi.
Sasa kuna ubaya akifuta kitu hakifai! Au shida yako unawaza atapata sifa na nyie njaa yenu kubwa ni kusifiwa hivyo mwingine akisifiwa inakua wivu na ugomvi.
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Yaani
Mkuu Wa Mkoa Yupo
Mkuu Wa Wilaya Yupo
Waziri Yupo
Saa Nyingine Ninaowateua Wananiangusha Sana
 
Back
Top Bottom