Kodi ya Majengo bado ni tatizo

Kodi ya Majengo bado ni tatizo

Tuendeleze mawazo ya Magufuri, nyumba isiyo ya ghorofa 10,000, ghorofa moja 50,000 n.k wazee wenye nyumba zisizo na wapangaji bure, nyumba za nyasi bure
Duh!
mzee naona unajitetea,
Hata hivyo kodi ya majengo lazima itozwe kulingana na thamani ya nyumba na eneo ilipo.
nasisitiza kuwa makadirio yaliyo fanywa na maafisa ardhi kati ya mwaka 2017 sio sahihi hivyo tuna shauri makadirio yafanyike kwa kuzingatia uhalisia wa nyumba na maeneo zilipo.
 
Kama ni hivyo nimestuka sivuti umeme ni mwendo wa solar tuu

Sent from my VFD 200 using JamiiForums mobile app
vuta umeme mzee, kuna faida nyingi kama unalipia kodi jengo lako,
faida moja wapo ni kutambulika endapo unataka kutumia kukopa fedha Benki n.k.
hivyo ukiendelee kutumia solar unajichelewesha mwenyewe na mwisho umasikini hakuachii.
 
mfumo ulio pendekezwa kwa kutumia Luku sio mbaya ni mzuri tu, ila unahitaji kufanyiwa maboresho mfano;
1.Jina la mmiliki wa nyumba/wamilkki

2. Namba ya nyumba.

3. Makadirio ya kodi kwa nyumba n.k

waziri wa fedha atoe ufafanuzi zaidi ili wananchi waelewe mfumo huu vizuri.
 
Kuna nyumba chungu mzima hata zilizo kwenye maeneo yaliyopimwa hazitozwi kodi ya jengo (labda waingize kwenye viwanja), nina mifano halisi karibu kabisa na ninapoishi, kuna jamaa alikuwa mkurugenzi mahali fulani ana nyumba 6 hazina wapangaji ameweka vijana wanakaa kwa makubaliano wasilipe kodi ila wazilinde tu na wala halipi kodi ya majengo
 
Kuna nyumba chungu mzima hata zilizo kwenye maeneo yaliyopimwa hazitozwi kodi ya jengo (labda waingize kwenye viwanja), nina mifano halisi karibu kabisa na ninapoishi, kuna jamaa alikuwa mkurugenzi mahali fulani ana nyumba 6 hazina wapangaji ameweka vijana wanakaa kwa makubaliano wasilipe kodi ila wazilinde tu na wala halipi kodi ya majengo
ni kweli unacho kisema, sasa inatakiwa zoezi lifanyike kuzitambua nyumba zote kila eneo, zisajiliwe kwa majina ya wahusika/wamiliki halafu tuanze zoezi la kulipa kwa mfumo wa LUKU.
kwanza lifanyike zoezi la kuhakika na kusajili nyumba zote upya, zoezi hili linaweza kufanywa na wizara ya ardhi wakishirikiana na serikali za mitaa.hakika kodi italipwa na taifa litapata chake.
 
tatizo sio gharama za kuweka umeme tatizo ni uhaba wa vifaa kama vile nguzo, unaweza kukaa mwaka mzima unasubiria nguzo ya umeme!! lazima tuangalia mambo kwa uhalisia wake, usijitazame wewe au watu wanao ishi masaki, tuangalie wakazi wanao ishi pembezoni mwa miji na hata vijijini.
Mkuu waziri amesema tuna nguzo za kutosha kusambaza umeme nchi nzima, halafu mjini wengi umeme wanao hapa tunawazungumzia hasa walio nje ya mji.

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu waziri amesema tuna nguzo za kutosha kusambaza umeme nchi nzima, halafu mjini wengi umeme wanao hapa tunawazungumzia hasa walio nje ya mji.

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
ufafanuzi mzuri umeshatolewa na waziri wa fedha,
sasa wananchi wameelewa na tuko tayari kulipa kodi kwa mfumo huo wa Luku.
 
Kodi ya majengo haswa kwa nyumba ambazo hazijapimwa, hazina hati miliki wala namba za mitaa/namba za nyumba ni vigumu kukusanya kodi mpaka pale utaratibu mzuri utakapo wekwa.

Watu wengi wanao miliki nyumba wapo katika maeneo yasiyo rasmi, nyumba hazina hati, hazina namba lakini baya zaidi makadirio yaliyofanywa na maafisa wa TRA hayajazingatia vigezo hivyo kodi kuwa kubwa au hata kuwa ndogo.

Kodi ya majengo iangaliwe upya ndipo tuanze kutoza.

Kwa sasa hivi bili za madai ya kodi za majengo zimelundikana ktk ofisi za serikali za mitaaa wahusika hawajui lolote.
Usijali wanakusanya kutumia luku hazitolundikana tena
 
Back
Top Bottom