Duh!Tuendeleze mawazo ya Magufuri, nyumba isiyo ya ghorofa 10,000, ghorofa moja 50,000 n.k wazee wenye nyumba zisizo na wapangaji bure, nyumba za nyasi bure
vuta umeme mzee, kuna faida nyingi kama unalipia kodi jengo lako,Kama ni hivyo nimestuka sivuti umeme ni mwendo wa solar tuu
Sent from my VFD 200 using JamiiForums mobile app
ni kweli unacho kisema, sasa inatakiwa zoezi lifanyike kuzitambua nyumba zote kila eneo, zisajiliwe kwa majina ya wahusika/wamiliki halafu tuanze zoezi la kulipa kwa mfumo wa LUKU.Kuna nyumba chungu mzima hata zilizo kwenye maeneo yaliyopimwa hazitozwi kodi ya jengo (labda waingize kwenye viwanja), nina mifano halisi karibu kabisa na ninapoishi, kuna jamaa alikuwa mkurugenzi mahali fulani ana nyumba 6 hazina wapangaji ameweka vijana wanakaa kwa makubaliano wasilipe kodi ila wazilinde tu na wala halipi kodi ya majengo
Mkuu waziri amesema tuna nguzo za kutosha kusambaza umeme nchi nzima, halafu mjini wengi umeme wanao hapa tunawazungumzia hasa walio nje ya mji.tatizo sio gharama za kuweka umeme tatizo ni uhaba wa vifaa kama vile nguzo, unaweza kukaa mwaka mzima unasubiria nguzo ya umeme!! lazima tuangalia mambo kwa uhalisia wake, usijitazame wewe au watu wanao ishi masaki, tuangalie wakazi wanao ishi pembezoni mwa miji na hata vijijini.
ufafanuzi mzuri umeshatolewa na waziri wa fedha,Mkuu waziri amesema tuna nguzo za kutosha kusambaza umeme nchi nzima, halafu mjini wengi umeme wanao hapa tunawazungumzia hasa walio nje ya mji.
Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Usijali wanakusanya kutumia luku hazitolundikana tenaKodi ya majengo haswa kwa nyumba ambazo hazijapimwa, hazina hati miliki wala namba za mitaa/namba za nyumba ni vigumu kukusanya kodi mpaka pale utaratibu mzuri utakapo wekwa.
Watu wengi wanao miliki nyumba wapo katika maeneo yasiyo rasmi, nyumba hazina hati, hazina namba lakini baya zaidi makadirio yaliyofanywa na maafisa wa TRA hayajazingatia vigezo hivyo kodi kuwa kubwa au hata kuwa ndogo.
Kodi ya majengo iangaliwe upya ndipo tuanze kutoza.
Kwa sasa hivi bili za madai ya kodi za majengo zimelundikana ktk ofisi za serikali za mitaaa wahusika hawajui lolote.