Mkuu ninavyojua makazi ya vijijini hayako kwenye utaratibu rasmi wa kulipa kodi ya jengo kwa sababu ni makazi duni ambayo yapo kwenye maeneo ambayo hayajarasimishwa, hii ndo failure kubwa kwa hii serikali ya chifu hangaya ku maximize makusanyo bila kujali taratibu na sheria wala kujali hali za maisha na vipato vya watu. Hayati mwalimu Nyerere aliwahi kusema na hapa namnukuu 'Serikali corrupt haikusanyi kodi, inawaogopa matajiri ambao kimsingi ndo wanatakiwa kulipa kodi na inabaki kufukuzana na maskini' haya maneno ya Nyerere yanaishi leo hii kwa sababu matajiri na wakoloni wanaoitwa wawekezaji wanapata faida kubwa na kujitwalia rasilimali bwerere huku wanyonge wakitaabishwa kwa kodi na tozo zinazobuniwa kwao kila kukicha...........rasilimali zetu, gesi, madini, mbuga, bandari zinamnufaisha nani hadi tuwe watumwa kwenye nchi yetu wenyewe!