Kodi ya Majengo kupitia luku rasmi Vijijini

Mimi nawapongeza kwa kuwakata,kila MTU achangie Uchumi wa nchi hii.Mbona wa mjini wamewezesha REA kwa muda wote.
 
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Mkuu
Kweli kabisa alafu kwa mwaka unalipia 12000

Bado watu wanalalamika!

Ova
huko vijijini zipo nyumba zingine thamani yake haifiki laki moja waliwekewa huu umeme wa REA.
Kwa watu kama hao kulipa hiyo 12000/=
ni sawa?
 
Chifu ashikilie hapohapo tena ikiwezekana aingize na land tax huko huko maana wakati ule watu wengine wakimbakiwa kodi na kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi kuna watu walikuwa wakishangilia na kumsifu jiwe.
 
Kweli kabisa alafu kwa mwaka unalipia 12000

Bado watu wanalalamika!

Ova
Unakosea sana, Kodi ya jengo ni kwa makazi yaliyopimwa ama kurasimishwa.
Vijijini wana aina yao ya ardhi inaitwa "village land" na wanasheria yao village land act.
Makazi ya vijijini hayajapimwa, hivyo nyumba hazitambuliki kwenye upangaji. Watu Kama hao kuwatoza Kodi ya jengo ni kuwaonea.
Walichapaswa kufanya ni kupima makazi yao na kuyaingiza kwenye mchoro
 
Fact mkuu Kwa mfano bibi yangu alienda lipia benk mwanzoni mwa Mwaka huu Kodi ya jengo ya Mwaka mzima ila maajabu juzi walipoanza huu mfumo anaanza katwa Tena!
Aisee hii si double taxation kabisa?
 
TANESCO ni kweli hii system imeanza kama ni kweli je, mlitoa taarifa kama hapana je, lini mumeanza utaratibu mpya pasipo taarifa?

Nipo nasubiri majibu nawasikilizia counter
Mie napendekeza kila mmiliki wa nyumba ajulikane ili anaponunua luku asiendelee kukatwa na hii ionyeshe kuwa kwa mwaka amemaliza deni.kuepuka ukatwaji wa luku kila unaponunua umeme,maana wapigaji wa hela nao walishajiandaa kuiba hiyo hela tafadhali mtuondolee usumbufu wa kukatwa kila unapofanya miamala ya luku.
 
Yote haya yamesababishwa na viongozi wasiokuwa nahuruma kwa watu waishio vijijini ambapo mtu anapata pesa kwa maramoja kwa msimu,na matharani wangekuwa wameandaa utaratibu wa ulipaji Kodi za majengo kusingekuwa na sintofahamu kwa mteja.nasema kwa sababu mie tayali wameshakata alfu mbili.
 
Yeah,

Niliona isiwe tabu nikakimbilia Burundi Mkuu, maisha iko huku[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hatuoni shida Kama wananchi wangekuwa wameshawaingiza kwenye utaratibu wa ujazaji wa fomu za nyumba na kuwa vigezo ama Haina vigezo.sasa hapa tunaibiwa kwakutokuwa na mpangilo wa makazi husika.
 
Ndio maana ninasema wameharakisha ukatwaji wa Kodi,kwani bado vijiji vingi havijapimwa na umeme ameshavuta,hivo Cha msingi tu nikuvipima vijiji vyote ili viingizwe kwenye ramani na hatimae watu walipe Kodi ya jengo kwa utaratibu usioleta Shaka kwa mpokeaji wa mwisho vinginevyo tutakuwa tunawachangia kumalizia nyumba zao na kununua magari ya kifahari na hii Ni hatari Kama wananchi tutanyamaza.
 
Mimi na wenzangu tuna kikundi cha Tofali tumejenga Banda tu la miti tukaweka Mashine zetu za kufyatua tofali Tunashangaa tunakatwa haya makato tena pesa nyingi.
Tanesco wamekurupuka ktk hili
 
Hatari sanaaaa, wanasema wanataka kuwasaidia masikini lakini cha ajabu masikini anachokipata wanakunyakua juu juu duu🤔
 
Ndo hivyo inatakiwa walipe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…