Doctor Ngariba
JF-Expert Member
- Jan 28, 2020
- 588
- 951
Habari JF members,
Naomba turejee kauli ya Rais wetu Samia alipokuwa anazungumza na wahariri wa vyombo vya habari alipoulizwa kuhusu katiba mpya na siasa za majukwaa. Simple tu alijibu dhamira yake kubwa ni kuifungua nchi kiuchumi japo katiba ni muhimu pia.
Lakini kwa hali ilivyo inaonekana kwa namna fulani dhamira hii yaweza kuyeyuka kutokana na kuwepo kwa baadhi ya kodi na tozo zilizoletwa na serikali yake kupitia bajeti ya serikali iliyosomwa hivi karibuni bungeni.
Kwa kuwa mheshimiwa Rais alikubali kukosolewa na kushauriwa serikali yake, naomba pia kupitia jukwaa hili (ambalo naamini na yeye yumo) tumshauri katika kodi/tozo hizi labda atapokea ushauri wetu na kuufanyia kazi.
1. Kodi kwenye miamala ya simu
2. Kodi kwenye mafuta
Kwa kuanza mimi nashauri hii kodi ya kwenye miamala ya simu ifutwe ama ikishindikana kabisa basi ipunguzwe maana itaongeza umaskini na kupunguza ajira za watu waliojiajiri katika utoaji wa huduma ya mobile money.