Kodi ya miamala ya simu ifutwe ama ipunguzwe; itaongeza umaskini na kupunguza ajira

Kodi ya miamala ya simu ifutwe ama ipunguzwe; itaongeza umaskini na kupunguza ajira

Wacha waendelee kushupaza shingo, ikiwa watumishi wa kawaida na digirii zao wanaweza kuishi kwa sh. 700,000/= -1,500,000/= kuna sababu gani ya kumlipa zaidi milion 10 mwanasiasa ambaye sifa yake ni kujua kusoma na na kuandika? Kwa umuhimu upi kwenye Taifa hili? Kusinzia bungeni na kukurupuka unapiga makofi ndiyo umuhimu wake?
Kwa mishahara yao hiyo hiyo ya watumishi KODI imezingatiwa. Lips KODI tujenge taifa letuuu. Misaada haina tija kwa maendeleo yetu.
 
Wao miamala yao wanafanyia bank, na ndio maana hawajaweka tozo huko.

Jiulize kwan bank ile sio miamala? Kwann kusiwekwe tozo na huko ili tulipe sote?

Wakati mwingine napenda tukamuliwe zaid ya hapa ili akili zitusogee tusiende kuchagua viongozi kwa kufuata nyimbo na fulana
Hata usipowachagua watakutawala tuu hawa ni wakoloni weusi.
 
Nimeshaongea sana kuwa wanaoturudisha nyuma nchi hii ni wabunge. Hiki cheo hakina maana zaidi ya kutuletea matabaka.

Bunge lisiwepo. Hata hao wanaopigania Katiba mpya, hawajabeba ajenda ya kitaifa zaidi ya kutafuta upenyo wa kwenda bungeni kuendelea kuwanyonya watanzania.

Tunaweza kuendelea kuwa na mabaraza ya madiwani yanatosha kabisa. Pia kukawa na Baraza kuu la madiwani lenye uwakilishi wa madiwani wawili au watatu kila mkoa kwa ajili ya kuishauri serikali na kutunga sheria.

Wabunge ndio maadui wa maendeleo ya Tanzania. Tuanze kupunguza hizi takataka ndio tuhimize Katiba mpya
 
Habari JF members,

Naomba turejee kauli ya Rais wetu Samia alipokuwa anazungumza na wahariri wa vyombo vya habari alipoulizwa kuhusu katiba mpya na siasa za majukwaa. Simple tu alijibu dhamira yake kubwa ni kuifungua nchi kiuchumi japo katiba ni muhimu pia.

Lakini kwa hali ilivyo inaonekana kwa namna fulani dhamira hii yaweza kuyeyuka kutokana na kuwepo kwa baadhi ya kodi na tozo zilizoletwa na serikali yake kupitia bajeti ya serikali iliyosomwa hivi karibuni bungeni.

Kwa kuwa mheshimiwa Rais alikubali kukosolewa na kushauriwa serikali yake, naomba pia kupitia jukwaa hili (ambalo naamini na yeye yumo) tumshauri katika kodi/tozo hizi labda atapokea ushauri wetu na kuufanyia kazi.

1. Kodi kwenye miamala ya simu
2. Kodi kwenye mafuta

Kwa kuanza mimi nashauri hii kodi ya kwenye miamala ya simu ifutwe ama ikishindikana kabisa basi ipunguzwe maana itaongeza umaskini na kupunguza ajira za watu waliojiajiri katika utoaji wa huduma ya mobile money.
Ni kufunga biashara zote za maduka ya mitandao ya simu tuone kama watapata hizo pesa
 
Serikali imefilisika imeamua kuwapora watu wake.Dunia mzima Hakuna tozo kama hizi
Serikali ni mm na we we . tulipe KODI kwa maendeleo yetu. Hata kwa mabeberu wenu nako maendeleo yao wamejiletea wao wenyewe kwa KODI zao. Lipa KODI
 
Back
Top Bottom