Kodi ya miamala ya simu ifutwe ama ipunguzwe; itaongeza umaskini na kupunguza ajira

Kodi ya miamala ya simu ifutwe ama ipunguzwe; itaongeza umaskini na kupunguza ajira

Habarini za wakati huu wapendwa wakuu natumai mko vyema

Sikuwahi kuandika thread ila naomba niandike.

Masikitiko yangu makubwa hasa kwa kundi la vijana na wadau wote wanaofanya kazi ya ujasiriamali kupitia kufanya miamala mbali mbali hii ni kutokana na kupanda kwa gharama za tozo kupitia makampuni ya mawasiliano ninayo yaona mbeleni ni yafuatayo.

1. Vijana wanaenda kupoteza ajira hasa waliojiajiri kupitia miamala

2. Fedha iliyokuwa inaonekana inaenda kupotea rasmi, means watu wataacha kuweka fedha kupitia makampuni ya simu au mabenki wakihofia makato

3. Tunakwenda kunyanyasa kundi kubwa la tuliokuwa tunawaita wanyonge.

Rai yangu kwa Mh. Raisi kama anaona njia ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ni kupitia miamala ya simu si sahihi, kuna wazazi ndugu jamaa na marafiki waliokuwa wakitumiwa fedha kupitia mitandao hiyo hali itaenda kukwama hivyo kuongeza wimbi la umasikini uliokithiri.

Njia pekee ya kuongeza mapato ni wapunguze mishahara na posho za wabunge na kupunguza idadi ya misafara isiyo na lazima

AM TIRED
 
Nami naunga mkono hili la kulipa kodi lkn ili liwe na uzito na lipokelewe vizuri na Wananchi, nashauri viongozi wetu watumie busara ndogo tu, waonyeshe uzalendo kwa vitendo...
Hata wao mawaziri mishahara yao inakatwa kulingana ilivyo, hata we we umekatwa sehemu ndogoogoo kabisaaa. Tujibane ndugu zanguni maendeleo yanagarama zakee. Tutoe kodii tujenge nchi yetuuuuu.
 
Hakuna mtanzania ambaye halipi kodi, unaweza kumtaja hapa km yupo.
Tangu Benjamin afute Kodi ya kichwa (direct tax) Kodi ile ilihamishiwa kwenye bidhaa na huduma.
Kodi IPI iliyohamishiwa kwenye bidhaaa?? Mbona ulaya KODI ya kichwa bado inaendelea kwani wao hawanunui bidhaaa? Au wakati uli tulipokua tunatoa KODI ya kichwa, kwani bidhaaa tulikua hatununui?
 
Kodi IPI iliyohamishiwa kwenye bidhaaa?? Mbona ulaya KODI ya kichwa bado inaendelea kwani wao hawanunui bidhaaa???. Au wakati uli tulipokua tunatoa KODI ya kichwa, kwani bidhaaa tulikua hatununui??
Bidhaa na huduma zinanunuliwa tangu enzi na popote pale duniani. Kwa Tanzania, wakati wa kodi ya kichwa, bidhaa/huduma hazikuwa zikilipiwa kodi na mlaji,, mlipaji alikuwa mfanyabiashara au mtoa huduma

Baada ya kufuta ile kodi, ikahamishiwa kwenye huduma/bidhaa kwa mlaji wa mwisho. Kama unaweza kurejea habari za kodi za 2000's, utajua hili.

Mwananchi alianza kulipa indirect tax kupitia kila bidhaa/huduma anayoilipia. Ile Kodi ilienda inapanda hadi hiv sasa imefika 18% na ndio hii VAT

Sasa, mwananchi analipa VAT kwa kila muamala, na hana sehemu ya kuikwepa, then anaambiwa aongeze certain amount kwa muamala huohuo... Inafikirisha, inaghadhabisha sana.

Nasimama kukosolewa!!!
 
Nasimama kukosolewa!
Tulipe kodiiii
 
Habari JF members,

Naomba turejee kauli ya Rais wetu Samia alipokuwa anazungumza na wahariri wa vyombo vya habari alipoulizwa kuhusu katiba mpya na siasa za majukwaa. Simple tu alijibu dhamira yake kubwa ni kuifungua nchi kiuchumi japo katiba ni muhimu pia.

Lakini kwa hali ilivyo inaonekana kwa namna fulani dhamira hii yaweza kuyeyuka kutokana na kuwepo kwa baadhi ya kodi na tozo zilizoletwa na serikali yake kupitia bajeti ya serikali iliyosomwa hivi karibuni bungeni.

Kwa kuwa mheshimiwa Rais alikubali kukosolewa na kushauriwa serikali yake, naomba pia kupitia jukwaa hili (ambalo naamini na yeye yumo) tumshauri katika kodi/tozo hizi labda atapokea ushauri wetu na kuufanyia kazi.

1. Kodi kwenye miamala ya simu
2. Kodi kwenye mafuta

Kwa kuanza mimi nashauri hii kodi ya kwenye miamala ya simu ifutwe ama ikishindikana kabisa basi ipunguzwe maana itaongeza umaskini na kupunguza ajira za watu waliojiajiri katika utoaji wa huduma ya mobile money.
1626343736921.png
 
Watu wakidai katiba mpya kuna wengine wana pinga
Kwa huu ushoga katiba mpya ni lazima nilikuwa sioni maana sababu maslahi yangu hayakuguswa ila kwa sasa tuko pamoja katiba mpya lazma iandikwe na wale kenge mjengoni pale wasilipwe zaidi ya million 3. Maana vingine vyote wanabebwa!
 
Gharama za maisha hapa nchini bado zipo chini mnoooooooo.
Ipo haja ya serikali kuongeza tozo nyingi zaidi kwenye huduma mbalimbali za kijamii
 
Tulioko kwenye vibanda vya mawakala kutoa pesa zetu zote kabla zahama la makato alijatukuta tukutane hapa.
 
Hata wao mawaziri mishahara yao inakatwa kulingana ilivyo, hata we we umekatwa sehemu ndogoogoo kabisaaa. Tujibane ndugu zanguni maendeleo yanagarama zakee. Tutoe kodii tujenge nchi yetuuuuu.
Wacha waendelee kushupaza shingo, ikiwa watumishi wa kawaida na digirii zao wanaweza kuishi kwa sh. 700,000/= -1,500,000/= kuna sababu gani ya kumlipa zaidi milion 10 mwanasiasa ambaye sifa yake ni kujua kusoma na na kuandika? Kwa umuhimu upi kwenye Taifa hili? Kusinzia bungeni na kukurupuka unapiga makofi ndiyo umuhimu wake?
 
Back
Top Bottom