BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Nimekutana na andiko hili la ndugu yetu, nikaona si vibaya tukashea pamoja, maana naona kaandika vitu vingi vya msingi kwa mtazamo wangu, japo sikulazimishi kuamini kama ni kweli au la, msome ndugu Mushi....
88888888888888
Na Thadei Ole Mushi
Kama kuna jambo ambalo nitasimama kidete kulitetea hapa nchini bila kuogopa ni maslahi ya masikini wa nchi hii. Unawaona hao watoto hapo pichani?
Hii ni Shule ya Msingi Olgira, Kata ya Sunya, Kiteto mkoani Manyara. Shule hii ina madarasa matano na wanafunzi 600 na walimu watano. Kwenye Shule hii kuna watoto wanatokea Kitongoji cha Natushi Km 12 kufika Shuleni anafika anaanza kupambana na mazingira kama haya, wakati huo kuna kiongozi anatumia V8 la Serikali kupeleka mwanawe pale Feza.
Kuna wakati Masikini wanatakiwa kuhoji ipo hivi....
Serikali imetoa Scholarship za wanafunzi waliofanya vizuri masomo ya Sayansi kwenda kusoma nje ya nchi. Nimepitia majina ya wanafunzi wanaolengwa na mpango huo nikakuta asilimia 95 wanatokea Shule za Private ambazo ada yake si chini ya milioni tatu. Kwa kuwa watoto hawa wa matajiri walipata mazingira mazuri na shule bora basi wamefanikiwa kufikia ufaulu wa juu.
Mtoto wa masikini kama hawa unaowaona hapa Pichani ni ngumu kuja kukutana na kodi ya wazazi wake akaitumia kusoma. Hata hivyo mimi naamini mtoto aliyetoka shule ya serikali ya kawaida akapata hata two ana uwezo mkubwa kuliko hawa wanaolishwa kila kitu pale St. Mary's. Mtoto anayetembea kwa miguu KM 12 shule haina walimu, chakula ni shida, Mzazi wake kauza kila kitu mtoto asome halafu anapata two huyu ndiye anayetakiwa kusaidiwa.
Nilikuwa nina fikiri
1. Fedha zilizolenga kupeleka wanafunzi kusoma nje ya nchi kwa mwaka huu ziende zikajenge hii shule ya Olgira na nyingine zenye hali kama hii.
2. Jambo la Pili vitengenezwe vigezo ambavyo vitasaidia kodi ya nchi hii kukutana na mtoto wa maskini, mathalan hii scholarship iliyopewa jina la Rais Samia inaendeleza ubaguzi na tabaka la elimu lililopo nchini. Nadhani wanafunzi waliopata one za sayansi toka shule za Serikali za kawaida ndio wapewe hii fursa.
3. Wanafunzi waliosoma Private kwa kuwa wazazi wao wana unafuu wa maisha basi Serikali inaweza kuwasaidia kutafuta vyuo huko nje na kuwasaidia nauli lakini issue ya ada wazazi wawalipie wenyewe.
Inauma sana haya yanayoendelea...... Watoto wa maskini watabaki kuwa wapiga kura wa watoto wa viongozi na wenye fedha. Niwaombe vijana kuacha kushinda kuangalia vichekesho Tiktok na kutafuta Connections badala yake washiriki kwenye siasa za nchi hii. Niwaombe vijana kujadili mustakabali wa taifa lao. Niwaombe vijana kuachakujadili vitu vya kijinga jinga na kufuatilia mambo ya msingi ya taifa lao.
Nisaidie kushare kama umekubaliana na mtizamo huu.
Ole Mushi.
0712702602.