Kodi za Tanzania Bara zifanane na za Zanzibar

Kodi za Tanzania Bara zifanane na za Zanzibar

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,650
Reaction score
21,014
Kwa jina la JMT.

Sijashuhidia hili ila miaka mingi nimekuwa nasikia kuwa kodi huko visiwa vya Zanzibar iko chini sana. Zamani ndugu yangu mmoja alikuwa anafuata vitu huko. Juzi kati kuna jamaa yangu kanunua TV huko. Hata magari nasikia kodi ipo chini sana.

Napendekeza kodi za Bara ziwe sawa na za Zanzibar. Mbona Serikali ya Zanzibar inaenda kwa kodi hiyohiyo!

Naamini Tanzania bara kukiwa na kodi ndogo basi itakuwa ndiyo kitovu cha biashara kwa Africa ya mashariki na kati, na pengine hata kusini.

Mtu hataona haja ya kufuata bidhaa Dubai au Gwanzuu wakati anaipata kariakoo, au Tunduma au huko mpakani Kigoma, Kagera, Kasumulu nk, kwa bei ileile.

Tuifanye Tanzania kuwa kitovu cha biashara.

#Kazi iendelee#
 
Kodi hazipo chini kilichopo ni watu kuingiza bidhaa kimagendo na hivyo Bei kuwa chini
 
Sasa hivi wabongo wanaenda kununua bidhaa Uganda zilizopitia bandari ya dar.
Huko serikali imelala, bidhaa zinapita mipakani bila udhibiti hivyo Bei yao inakuwa chini sana
 
Hii variation ya tax rates Kati ya Tanganyika na Zanzibar inatokana na mitazamo ya wakuu wa nchi. Rais Mwinyi wa Zanzibar si muumini wa kodi kandamizi au kodi yenye elementi zozote za dhuluma ila kwa upande wa Tanganyika hizi kodi kandamizi asili yake hasa ni mtazamo mbovu aliokuwa nao Mwendazake.

Ila kwa awamu Hii ya sita tutegemee neema kwasababu Mama ameshafanya declaration kabisa kuwa bora kukosa mapato kuliko kuwa na mapato yatokanayo na dhuluma. So tumpe Mama muda ni imani yangu good time is just around the corner
 
Ni kweli lakini hii ni shithole country labda bi Mkubwa aamue kweli kweli.
 
Hii variation ya tax rates Kati ya Tanganyika na Zanzibar inatokana na mitazamo ya wakuu wa nchi. Rais Mwinyi wa Zanzibar si muumini wa kodi kandamizi au kodi yenye elementi zozote za dhuluma ila kwa upande wa Tanganyika hizi kodi kandamizi asili yake hasa ni mtazamo mbovu aliokuwa nao Mwendazake. Ila kwa awamu Hii ya sita tutegemee neema kwasababu Mama ameshafanya declaration kabisa kuwa bora kukosa mapato kuliko kuwa na mapato yatokanayo na dhuluma. So tumpe Mama muda ni imani yangu good time is just around the corner
Kwamba jambo hilo la kodi nafuu lilianza alipoingia Mwinyi? Miaka ya 2000 mpaka 2008 nimenunua vitu zenji kwa bei nafuu tofauti na bara, mwendazake alikuwa nani? Na Mwinyi?
 
Sasa hivi wabongo wanaenda kununua bidhaa Uganda zilizopitia bandari ya dar.
Kwa sasa nipo hapa Tunduma Kuna vitenge na kanga zinatoka Zambia bei poa usipime, nilipohoji wakasema ni wale wafanyabiashara waliokua na maduka pale kariakoo baada ya serikali ya kijambazi na kishetani kuwafanyia kitu mbaya wakaona isiwe shida.

Na vile vile nina mzee wangu alikua na duka upande wa Tanzania alikua anatozwa kodi laki 7 alipoona inamkata alihamia upande wa Zambia sasa kule analipia elfu 80 ya kitanzania kwa duka lile lile hebu ona maajabu hayo na kule ikitokea huo mwaka hujalipa wakija mwakani au ukienda mwenyewe kulipia hawakuulizi mambo ya mwaka jana.
 
from laki 7 to 80,000 kwann asihame? lazima tufanyie marekebisho kodi zetu
 
Hii variation ya tax rates Kati ya Tanganyika na Zanzibar inatokana na mitazamo ya wakuu wa nchi. Rais Mwinyi wa Zanzibar si muumini wa kodi kandamizi au kodi yenye elementi zozote za dhuluma ila kwa upande wa Tanganyika hizi kodi kandamizi asili yake hasa ni mtazamo mbovu aliokuwa nao Mwendazake.

Ila kwa awamu Hii ya sita tutegemee neema kwasababu Mama ameshafanya declaration kabisa kuwa bora kukosa mapato kuliko kuwa na mapato yatokanayo na dhuluma. So tumpe Mama muda ni imani yangu good time is just around the corner
Huu muziki huwa haulembi atakapo anza kukosa mishahara ndo ataelewa kodi kandamizi, polisi fine, permit fee na vyanzo vingine vinakujaje!!.. kunatatizo la kimfumo ambapo mfumo ili ujengeke ni lazima uwe na watu waliokubaliana kuujenga na kuuheshimu ...ila mkisigana kwa ubinafsi, majigambo, kutafuta sifa nk. Usitegemee kuona nuru.
 
Huu mziki huwa haulembi atakapo anza kukosa mishahara ndo ataelewa kodi kandami, polisi fine, permit fee na vyanzo vingine vinakujaje!!.. kunatatizo la kimfumo ambapo mfumo ili ujengeke ni lazima uwe na watu waliokubaliana kuujenga na kuheshimu ...ila mkisigana kwa ubinafsi, majigambo, kutafuta sifa nk. Usitegemee kuona nuru.
hapo mwanzo umeandika nothing but dua la kuku. serikal haijawahi kosa mshahara hata siku moja.
Kodi itaendelea kukusanywa kama kawaida.
kodi kandamizi na mambo mengine ndio vinafanya watu waone wanaonewa.. scorching earth method inajenga uadui kati ya mlipa kodi na serikali
 
Kodi ndio uchumi wa nchi, hakuna nchi yoyote inayojitambua ambayo haikusanyi kodi, kwa Tz kinachotakiwa si kupunguza kodi Ila kuongeza base ya walipaji, kodi iwe nyingi zaidi ili iakisi maisha ya watu wote hata wafanyabiashara. Kata
 
hapo mwanzo umeandika nothing but dua la kuku. serikal haijawahi kosa mshahara hata siku moja.
Kodi itaendelea kukusanywa kama kawaida.
kodi kandamizi na mambo mengine ndio vinafanya watu waone wanaonewa.. scorching earth method inajenga uadui kati ya mlipa kodi na serikali
Dua la kuku hahaha! Hujui hata unachojaribu kukifiria... Anyway nachokiona uwezo wako ni mdogo sana kwenye expenditure za nchi hii. Nakuacha kama ulivyo.
 
Dua la kuku hahaha! Hujui hata unachojaribu kukifiria... Anyway nachokiona uwezo wako ni mdogo sana kwenye expenditure za nchi hii. Nakuacha kama ulivyo.
hahaha naona umejib nothing but ngonjera. try to hit the point man.
 
Bara kukiwa na kodi sawa na zanzibar, kutakuwa na wateja wachache sana watakaopitishia mizigo huko kwasababu ya population yake, bora huku iwe kubwa ili walau kule watu wakanunue vitu na wenzetu wapate wateja.
 
Back
Top Bottom