Kodtec Speaker systems

Kodtec Speaker systems

kma nisingekuwa na kodtec 2912 ningeiishi hapa kwa muda


kwa mdundo ninaosikia nisingejiuliza mara 2 kwenye price tag
Screenshot_20230423-110641_UC%20Browser.jpg
 
Yaan Kuna jamaa ni dereva wa bas za iringa hua anapaki kalibu na kwangu huku dodoma, asa alikua akija anapiga ziki lake kuubwa la Sony xplod zile 1350w ila na Mimi siku nimenunua nmefunga usiku kucha .
asubui yake hakwenda kazin asa nikaliwasha mwanangu, yaan nilimshutua akiwa kwenye bas lake anafanya service na nilikua natest wimbo wa fire boy-jealous yaan Ile wimbo unaanza tu kwanza niliiskia watu wanaguna huko nje baadae nikaona anajileta kuangalia Nini Tena kitu Gani nmeweka alishangaa saana mpaka alijikuta ananiuliza maswali mengi mpaka anayarudiarudia.

Narudia Tena these pioneers subwoofers are fkng thumping crazy yaan uwez amini na mwonekano wake wa saani saani aseh kodtec wakasome

Both two are Total 800 RMS watts
Mpwa nitakuja kuweka kijiwe kwako..😀😀😀
 
Au kama ukishindwa waweza jichanga taratibu ukaanza kununua spika Moja ya pioneer mf .ts w309d4 au 310d4 200k/= alafu amplifaya za deochestra au boschmann 300k/=, tweeter zako midi za kawaida za Sony mega bass
Na power supply Yako geton mambo yanakua mazuri,
Coz mi mwenyewe nilenda kununua kodtec kt 2912 nikakuta mdada anachat aan tu kumuuliza subwoofer niliyokupa ninaiitaji pale pale akaniropokea eti "hazipo zimeisha" wakati mi naiona kwenye Kona imefunikwa na box , nikamwangalia yule dada Tena nikaona Bado anachat nikaamua kutoka nikaona Ile model ya kt 2809 kalibu na mlango wao nikaiulizia akanambia ety "subwoofer zote hazipo zimeisha" yaan niliumia kichiz nikaenda kupumzika kwanza uwanjan kesho yake nikawaza upya kufikilia kununua vinu vya pioneer nilienda Kwa mafundi wa magari kuwauliza wakaniuliza nataka kufunga spika ngapi ? Nikawaambia nne , akasema ""nne?"" Nkasema ndio akaniuliza kwani una nyumba Yako au umepanga ? Nikawaambia nmpanga wakanambia nazingua, nitasababisha craki kwenye Kuta , ndo wakanishauri niweke mbili na hizo mbili nijiandae Kwa notes ya mwenye nyumba.
In shot mambo Yako ivi.
1. Power supply
2. Tweeter nne
3. Amplifier
4. (2)pioneer subwoofers ts w309d4
12inches (ikiwa chini ya bed)
5. Midi (hazijafuguliwa au kufungwa nasubilia box zake kutoka Kwa fundi)
jumla imekucost bei gani mkuu kuunda hyo system??
 
wakuu nisaidieni ntapata wapi kodtec subwoofer 2913 au 2812 maana nimewachek insta wameambia kwa sasa hawana brand hizo.. je kuna maduka tofauti na haya wanauza hizi model.. nipo dodoma
Kiufupi sahv Kodtec wamebase kwenyw mablender sijui Microphone mara Juice Dispenser na vitu kama Rice cooker!! Sijui mambo ya mziki wana lile lihometheatre lao basi sijui kwanini
 
Aya .
1.socket extension
2.Power supply.
3.Wiring kit.
4.Subwoofer speaker unayoitaka mf HCCA ORION🤓 au pioneer.
5. Box kubwa la spika.
6. Mids (midi) speakers au spika mayai 6"x9" za pioneer au kampuni yoyote, ZENYE watts za kutosha.
7. Tweeter nzuri kama alpine na pioneer (achana na tweeter za aftano)
8. Amplifier kulingana na watti za spika Yako.
9. Equalizer.
10. Crossover (optional) Kwa sabab most of amplifaya zinakua na internal crossovers ila ni muimu kuwa nayo kama independent hardware.
10. dynamic sound processor (DSPs)optional, hapa haka kakifaa kanatoa mziki tunaopenda kuusikiliza ndo sehem yake yaan Kila production iliyotumika Kwenye mziki unaiskia directly , ila jipange Kwenye gharama yake ndo maana nasema ni optional.
11. Receiver au Bluetooth mp3/mp4 player.

NB soma maelekezo ya Kila kifaa utakachonunua
hatuna hela za kununua SvS subs au Sunfire,kilichobaki ni kusuka tu
 
Tupe specification zake kidogo
Unataka specification za Chinese subwoofer?
Mwenzio yalinikuta kwenye sea piano sp 912 nilipoona wameandika et subwoofer frequency response 20hz--200hz
Na satellite frequency response 150hz--20khz
Nikaona maisha ni Marais ,
Kudadek nilidownload equalizer ya sim inayoanzia 20hz mpaka 16khz
Nikaset vizuri daah mwanzon ilikua inajitaid inapiga deep bass kias flan ila sasaivi spika lake ukizidisha saut ikawa kubwa linaanza kutapika bass kama linabanja vile.. yaan ndo nilikoma kumwamin mchina daah
 
Back
Top Bottom