Koffi Olomide deported following JKIA assault

Koffi Olomide deported following JKIA assault

I don't see this happening in Tanzania. Well done Kenyans. Huku kwetu mchina kampiga hadi kumuua mfanyakazi aliyedai nyongeza ya mshahara na vyombo vya ulinzi vimehamia Dodoma kwenye mkutano wa chama.
 
Huyo bimdada pamoja na kuambulia mateke, kibarua ndio kimeshaota nyasi. Ila hilo la kumrudisha nyumbani lilikuwa halitoshi alitakiwa ashtakiwe ili ajifunze kuheshimu binaadamu wenzake

Adhabu yake ilitakiwa iwe kifungo cha mwezi mmoja jela,viboko kumi wakati anaanza adhabu yake na vingine kumi wakati anamaliza adhabu yake.
 
Adhabu yake ilitakiwa iwe kifungo cha mwezi mmoja jela,viboko kumi wakati anaanza adhabu yake na vingine kumi wakati anamaliza adhabu yake.
Hivi ingekuwa ni mtu wa kawaida ungeona adhabu hiyo ingekuwa ndio stahili yake, lakini kwa kuwa ni yeye ameondoka salama. Najiuliza hivi yule jamaa aliyemuita kuja kupiga show ndo isha kula kwake? Au Kofi atalipa gharama?
 
Hapa kwetu msanii maarufu aliyehukumiwa kwa ulawiti wa watoto aliahidiwa kutolewa ikiwa bwana mkubwa mmoja angeshinda sababu ya kumtoa ni kwamba yeye (msanii) ni maarufu mno kukaa jela.

Kwetu kila kitu ni siasa tu.

BTW:Siyo tukio la kwanza kwa Koffi kumpiga mtu hadharani tena ugenini hata Malawi or Mozambique alifanya hiki hiki kwa promoter na akatokomea.

Safi sana Kenya.
 
Safi sana,anadharau sana huyu,sijui kwa vile ana hela,ndo maana hawezi kanyaga ulaya,maana anahitajika Paris ili kujibu mashitaka ya kumbaka dancer wake,aendelee kumuonea huyo huyo mjinga mjinga Cindy le coeur
 
Ushawishi na mashabiki wengi alonao vinampa kiburi.
Manyan'gau wametenda ipasavyo.
Zaidi ya hapo anatuhuma huko ufaransa za kubaka
 
Huyu mkongo Kofi kamshambulia mnenguaji kwa makusudi ii afukuzwe nchini Kenya,ni kama tukio la kupanga ili asifanye show.
 
Safi sana wakenya, kwa hili mmenifurahisha sana. Huu unafaa uwe mfano wa kuigwa. Mimi nikikuona unampiga mwanamke mbele yangu basi ujue nahusika moja kwa moja, lazima nikupe vitasa vya maana uweke kumbukumbu maishani mwako.
 
Hatua muafaka dhidi ya huyu mdhalilishaji wa wanawake. Halafu badala ya kuomba samahani kwamba alichofanya si sawa bado anadai hakukusudia kumpiga. Hongera kwa Serikali ya Kenya kwa kutoyumba kwenye uamuzi wenu na Wakenya wote kule twitter na Facebook waliopinga kwa nguvu zote kitendo kile cha udhalilishaji.
 
Hongera kwako pia Mkuu kwa kuwa wa kwanza kupinga kitendo kile pamoja na kushambuliwa na baadhi humu. I salute you Sir.

Safi sana wakenya, kwa hili mmenifurahisha sana. Huu unafaa uwe mfano wa kuigwa. Mimi nikikuona unampiga mwanamke mbele yangu basi ujue nahusika moja kwa moja, lazima nikupe vitasa vya maana uweke kumbukumbu maishani mwako.
 
Kenyan minister kasemaje, eti ame "face the full force of the law." Sheria yao ilipofikia ndio hapo, deportation? Full force of the law?

Anyhow, namshangaa sana Koffi. Im sure Koffi ameanza kupata exposure ya kuondoka misituni Afrika humu wakati wengine tuko chekechea lakini bado mpaka leo lina u primitive wetu wa kijima.

Formative years spent in the equatorial forests, you ain't changing him.
 
Back
Top Bottom