Uchambuzi mzuri wa kumuhusu ' Large Degaire ' Koffi Olomide na hongera sana kwa hilo Mkuu ila tambua ya kuwa hata kama ana uwezo gani ila katika fani yoyote ile kama huna ' nidhamu ' ni kazi bure. Koffi Olomide anasumbuliwa mno na ' ulimbukeni ' hasa baada ya kuwa ni Mtoto aliyekulia katika familia ya kimasikini na kuishi kimasikini vile vile mpaka alivyopata Pesa ndipo akaanza ' kubadilika ' na ndiyo maana hata afanyeje huwa ' hafurukuti ' kwa lolote au chochote kutoka kwa Vijana waliokulia katika ' utajiri ' akina Jean Bedele Tshituka Mpiana na Ngiama Makanda Werrason ambao wao ' mziki ' hawafanyii ' dhiki ' au ' shida ' hasa ukizingatia wote Baba zao walikuwa ni ' Mabalozi ' wa nchi kubwa za Ulaya enzi za Rais Mobutu Seseseko Kuku Wa Zabanga ' Le Grand Leadear '. Na anachokifanya sasa Koffi Olomide ni kuiba tu Wanamuziki wa akina Wenge Musica BCBG na Wenge Musica Maison Mere lakini kinachomuumiza na kumshangaza ni kwamba kila ' akinyakuwa ' Wanamuziki ' mahiri ' huko akina JB Mpiana na Werrason wanaingia ' chimbo ' na kuibua vijana wapya kabisa ambao huja kuwa ' moto wa kuotea mbali ' na ' tishio ' pia.
Mfano Koffi Olomide alimnyakuwa ' Drummer ' maarufu sana wa Wenge Musica BCBG ya JB Mpiana aitwae Titina Alcapone ' Le Grand Prete ' ila muda mfupi tu JB Mpiana akaibua ' fundi ' wa kuzikaanga ' chips ' ama ' drums ' aitwae Seguen Mignon a.k.a Maniata ambaye kwa kweli amemfunika vibaya mno Titina na sasa ' kapotea '.
Hakuishia tu hapo bali Koffi Olomide akaendelea na ' upuuzi ' wake ambapo safari hii akaenda katika bendi ya Werrason ya Wenge Musica Maison Mere na ' kumnyakua ' kwa ' jeuri ' Rapa au Fundi wa ' kughani ' wenyewe Wakongo huwaita ' atalakus ' na Wafaransa huwaita ' animateurs ' aitwae Rwinga Keps au kwa jina ' maarufu ' la muziki alijulikana sana kama ' Brigade Sabateur ' ambapo baada tu ya kumchukua Werrason hakuchelewa na mara moja akaenda kukiibua ' kifaa ' kimoja ' matata ' katika ' kurapu ' aliyekuwa akiitwa Celeo Mozami Muviu au kwa jina maarufu anaitwa ' Stramme ' ambaye alikuja kumfunika vibaya sana Brigade na hadi sasa kapotea.
Hata hivyo kwa faida yako Mkuu Koffi Olomide ni mzuri tu wa kuimba miziki hii ya ' Video ' ila wenye ' shughuli ' yao hasa katika ' live ' perfomances Congo nzima hakuna anayewafunika Wenge Musica BCBG ya JB Mpiana na Wenge Musica Maison Mere ya Werrason na ndiyo maaana hata Kampuni kubwa kabisa ya ' Kilevi ' kinachopendwa Congo nzima kiitwacho ' PRIMUS ' imeingia ' mkataba ' nao mnono lakini kwa Koffi Olomide ' wamesitisha ' baada ya kuona kuwa hana ' mashabiki ' wengi anapokuwa anapiga katika concerts zake sehemu mbalimbali duniani.
Mkuu labda tu niseme unapofushwa na mapenzi yako binafsi kwa wenga na kutokumpenda Koffi
Kwa taarifa yako tu hakuna mwanamuziki mwenye nidhamu ya muziki Congo kama Koffi na kundi lake, ukiachilia mbali udhaifu wake wa kupenda totoz na wivu
Lakini bendi yake ndio bendi iliyodumu muda mrefu kuliko zoote na bado ipo katika kiwango kilekile
Kuhusu wanamuziki kuhama ni jambo la kawaida sana kwa waCongo, kimsingi hakuna mwanmuziki amaezalisha wanamuziki wengi nguli kama koffi na wakaondoka(sina haja ya kutaja majina)
Lakini bahati mbaya Koffi akichukua yeye unaitwa wizi
Unakumbuka kuna wakati Koffi alifanyiwa mtimanyongo na matajiri wa Congo akachukuliwa wasanii wake asilimia 80 wakaanzishiwa bendi ya Academia? Mwisho wa siku karibu woote walirudi na bendi ikawa imara
Kuhusu utajiri hapo ndio usiseme kabisaa, Koffi hakuwa masikini wa kutupwa kama unavyojaribu kuaminisha, Alizaliwa Kinshasa na masomo yake ya juu alipatia Paris, ana exposure ya kutosha na pesa ka fight zake sio za baba
Werrason na Mpiana ni wanamuziki wazuri sana lakini hawana nidhamu ya muziki wala pesa zao, hawana la maana lolote wanaweza kijivunia zaidi ya kula sana bata Paris na wakiishiwa kidogo wanageuka ombaomba kwa kujikomba kwa matajiri wa kicongo tofauti na koffi
Wapo wanao amini koffie ndie mwanamuziki tajiri zaidi Afrika, amewekeza kuanzia Congo hadi paris
Kuhusu live, usichokijua ni jambo moja koffi na akina wenga wanapiga muziki tofauti kidogo ingawa wote mtaita bolingo, ila la koffi ni taratibu na la akina wenga ni mpele mpela
Huwezi kusema R Kelly ahajui muziki kwakua Usher Raymond anashambulia sana jukwaa kwa kucheza zaidi ya R Kelly
Kuhusu mikataba minono hapo ndio usiseme kabisa, fanya utafiti hiyo kampuni imekaa na koffi muda gani na kwanini imemuacha na je anamikataba gani mingine
Unaweza usiamini lakini hizi ndio taarifa sahihi kwa sasa, kwamba Koffi na kijana wake ipupa ndio wanamuziki wanaosumbua zaidi congo kwa kupiga sana matamasha ya bei ndefu duniani kote
Lakini hii haimaanishi akina wenga( namaanisha Werrason na Mpiana) pamoja Gora kwamba hawako vizuri kmuziki