Koffi Olomide, Mzee Wa "Mizigo"

Antoine Koffi Olomidé (amezaliwa tarehe 13 Agosti 1956), ni mwimbaji, mtayarishaji, na mtunzi wa ngoma aina ya soukous kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Alizaliwa Kisangani, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mama mzaliwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na baba mzaliwa wa Kongo, na alilelewa katika mji wa Kinshasa.
Alienda Ufaransa kusoma. Akiwa Paris, alianza kucheza gitaa na kuandika nyimbo. Aliporudi Kongo, alikuwa mwanachama wa Viva la Musica, bendi ya Papa Wemba. Koffi aliimarisha mtindo wa polepole wa soukous, uliokuwa umeisha umaarufu. Aliuita mtindo huu Tcha Tcho, na ulipata umaarufu nje ya Kongo. Muziki wa Koffi unaweza kusababisha utata, maana hutumia matukio na mada inayofikiriwa vibaya na kihafidhina katika jamii. Yeye pia ameshiriki katika mradi wa muziki wa salsa wa Africando.

Koffi ameshinda tuzo nne za Kora katika Afrika ya Kusini na pia alishinda msanii bora katika Afrika ya Kati. Ameowa na ana watoto watano.

Albamu ya Olomide Haut de Gamme: Koweït, Rive Gauche imeorodheshwa katika Albamu 1001
 
Dah! Salute mkuu! Sina la kuongezea zaidi ya kusema ulete na ya pepe kalle!

Akhsante Mkuu ila kwa Pepe Kalle sijajikita sana Kwake na nimejikita 100% kwa hawa ' Manguli ' wa Kizazi cha kati cha akina Koffi Olomide, JB Mpiana, Werrason na Extra Musica ile ya Roga Roga iitwayo Extra Musica Zangul Zangul. Hata hivyo naamini wapo Watu humu ambao wana ' nondo ' za kutosha za kumuhusu Hayati Kabasele Yampanya Pepe Kalle na watasikia ' kilio ' chako na watakupa majibu yako ' mujarab ' kabisa.
 
Kaka uko na knowledge ya kutosha pande hizo,Mimi mwenyewe shabiki mkubwa wa mziki wa Congo.

Akhsante Mkuu na tupo pamoja. Hakuna kitu ninachokipenda duniani kama kucheza na kusikiliza muziki wa Congo na yote hayo ni 9 ila 10 hakuna Bendi ninayoipenda na Mwanamuziki ninayempenda duniani kama ya Wenge Musica Bon Chic Bon Genre yake Jean Bedele Tshituka Mpiana. Napenda mno mziki Mkuu ila hii ya Congo na hapa Bongo huvutiwa sana na Bendi mbili tu ambazo naona wanajaribu kupiga kama Wenge akina Twanga Pepeta na FM Academia na huwa nikipata ' vijihela ' vyangu kidogo vya ' ngama ' basi kila Weekend ukija Mango Garden au New Msasani Club hutoweza kukosa kumwona ' Le Mathematicien ' GENTAMYCINE.
 
wakuu naomba mniwekee link ya huyo ndugu aliewadadavua wasanii hawa na mambo yao ya kishirikina,pliz,pliz,pliz naomba mniwekee.nna hamu sn ya kusoma huo Uzi.natanguliza shukrani.
 

Mkuu labda tu niseme unapofushwa na mapenzi yako binafsi kwa wenga na kutokumpenda Koffi

Kwa taarifa yako tu hakuna mwanamuziki mwenye nidhamu ya muziki Congo kama Koffi na kundi lake, ukiachilia mbali udhaifu wake wa kupenda totoz na wivu
Lakini bendi yake ndio bendi iliyodumu muda mrefu kuliko zoote na bado ipo katika kiwango kilekile

Kuhusu wanamuziki kuhama ni jambo la kawaida sana kwa waCongo, kimsingi hakuna mwanmuziki amaezalisha wanamuziki wengi nguli kama koffi na wakaondoka(sina haja ya kutaja majina)
Lakini bahati mbaya Koffi akichukua yeye unaitwa wizi
Unakumbuka kuna wakati Koffi alifanyiwa mtimanyongo na matajiri wa Congo akachukuliwa wasanii wake asilimia 80 wakaanzishiwa bendi ya Academia? Mwisho wa siku karibu woote walirudi na bendi ikawa imara

Kuhusu utajiri hapo ndio usiseme kabisaa, Koffi hakuwa masikini wa kutupwa kama unavyojaribu kuaminisha, Alizaliwa Kinshasa na masomo yake ya juu alipatia Paris, ana exposure ya kutosha na pesa ka fight zake sio za baba
Werrason na Mpiana ni wanamuziki wazuri sana lakini hawana nidhamu ya muziki wala pesa zao, hawana la maana lolote wanaweza kijivunia zaidi ya kula sana bata Paris na wakiishiwa kidogo wanageuka ombaomba kwa kujikomba kwa matajiri wa kicongo tofauti na koffi
Wapo wanao amini koffie ndie mwanamuziki tajiri zaidi Afrika, amewekeza kuanzia Congo hadi paris

Kuhusu live, usichokijua ni jambo moja koffi na akina wenga wanapiga muziki tofauti kidogo ingawa wote mtaita bolingo, ila la koffi ni taratibu na la akina wenga ni mpele mpela

Huwezi kusema R Kelly ahajui muziki kwakua Usher Raymond anashambulia sana jukwaa kwa kucheza zaidi ya R Kelly

Kuhusu mikataba minono hapo ndio usiseme kabisa, fanya utafiti hiyo kampuni imekaa na koffi muda gani na kwanini imemuacha na je anamikataba gani mingine

Unaweza usiamini lakini hizi ndio taarifa sahihi kwa sasa, kwamba Koffi na kijana wake ipupa ndio wanamuziki wanaosumbua zaidi congo kwa kupiga sana matamasha ya bei ndefu duniani kote
Lakini hii haimaanishi akina wenga( namaanisha Werrason na Mpiana) pamoja Gora kwamba hawako vizuri kmuziki
 
Akhsante Mkuu.

Somo moja nimeondoka nalo kwenye post yako ni kuweka NIDHAMU kwenye Kila kitu. Nikakumbuka mfano wa Baba wa Taifa na yule waziri wa uingereza aliyepatikana na kashfa ya kutembea na kimada akaandika barua ya kujiuzulu, waziri mkuu aliishia kuteua waziri mwingine tu. Reputation muhimu sana
 
 
Mkuu hii imetulia,inaonyesha wazi Gentamycine ni mshabiki wa Werrason na JB, pamoja na mapungufu aliyonayo amekuwa akifanya vzr kwenye game kwa muda mrefu.
 
Binafsi Namkubali Koffi hasa alipoibiwa wanamuziki wake ambao walianzisha quarter later academia na walitoa album nzuri sana Nikajua Koffi kaisha lakini alikuja na album mpya na Style kali zaidi na kuonyesha nini maana ya Ukongwe&kipaji,pamoja na hayo amerudisha muziki wa Congo kwa hii nyimbo mpya ekotite yaani jamaa noma ni Kama Dully Sykes toka enzi hizo Anaturusha na hajawahi kuchuja.
 
Mkuu umeniwahi tu kusema haya uliyoyasema,tatizo la GENTAMYCNE anawapenda sana bcbg wengemusica na wenge maison merre kiasi kwamba wamemtia upofu hata haoni ubora wa koffie Olomide but all in all koffie ni baba ya muziki kwa kizazi cha NNE Kongo.
 
Koffi atabaki juu. Kwenye record ya wanamuziki kumi wenye mafanikio Africa hao akina Bin Adam na Solola Bien mbona hawapo? Le Grande Mopao Mokonzi ni namba nyingine.
 
Popoma uko vizuri. Uchambuzi makini
 
Ukiniuliza Mimi in yupi msanii bora Wa Africa wa Muda wote nitakuambia si mwingine Bali ni Mopao , Koffi olomide nyimbo zake kwangu huwa hazichuji napenda anavyopangilia sauti ya waimbaji wake na pia jinsi anavyoongeaongea kwenye nyimbo zake, kiasi kwamba nimekalili anavyoongeaongea hata nikiwa peke yangu najikuta nami naongea kama Yake ukiwa karibu yangu waweza fikiri nakusemesha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…