Koffi Olomide ndio msanii bora wa muda wote kutoka Congo

Ushasema koffi ni msAnii bora ukitoa generation ya kina luambo
Hujui madilu naye ni generation ya luambo ?
Anyway kwa kizazi kipya koffi olomide na fally ipupa de carpe ya mervele ndio wasanii bora wa muda wote
 
Isikilize Album nzima utapenda zaidi kuna ngoma inaitwa micko
 
Heshima kwako.mkuu
 
Massiya natamani nikualike home halafu tusikilize miziki ya Franco aka L'a okanga la ndju pene. Tena kwenye saturi zile mziki wake unatoka bomba vibaya mnoo. Fikiria unasikiliza bisalela au freins a man au Mario. Baba hawamjui Franco hawa.
 
Mkuu ahsante. Kutaja Bisalela umenikumbusha wimbo maridhawa waimbaji wakiwa na Micheal Boyibanda, Kiambukuta Josky na Wuta Mayi wakiongozwa na Youlou Mabiala (Mwana wa OK Jazz au Mwana Luambo). Solo ya Luambo na Mtunzi /rythm gitaa akiwa Papa Lutumba. Kutokana na wimbo wa Simaro mwingine uitawao Mabele ulioimbwa na Sam Mangwana ambao ulikaa juu ya charts kwa muda mrefu Mzee Luambo aliwaita wapigaji wake viongozi machweo na kuwaambia kwa muda wa miezi sita ijayo ni tungo zangu tu ndio zitapigwa live. Huu ndiyo mwimbo uliyofanya Simaro kupachikwa title ya Le Poete (mwanamashairi). Balaa nyingine ilitokea kati ya Maya mtunzi Simaro mwimbaji Carlyto Lassa na Mario mtunzi Luambo waimbaji Luambo na Madillu-Carlyto akachaguliwa kuwa mwimbaji bora Zaire wa Mwaka na Lutumba Simaro mtunzi bora, Mario ikapigwa chini (Luambo aliwashangaa waandishi wale waliopiga kura). Wakati huu TP OK Jazz ilikuwa na makundi mawili la ndani DRC chini ya Simaro na la nje Europe chini ya Franco. Stori hizi zinaonyesha ndani ya TP OK Jazz kulikuwa na miamba ilito tukuka na sifa moja wapo ya Luambo ni kukubali kufanya kazi na mafundi hawa na kuwa ongoza kupata kikosi ambacho huenda aina yake isitokee tena.

Ila Likoffi Jamani Linajua toka mdogo mpaka leo nasikiliza na kuzicheza nyimbo zake,huyu mtu anajua bwana
 
Li Mopao dudu lenye a.k.a nyingi dunia nzima!!
 
Massiya natamani nikualike home halafu tusikilize miziki ya Franco aka L'a okanga la ndju pene. Tena kwenye saturi zile mziki wake unatoka bomba vibaya mnoo. Fikiria unasikiliza bisalela au freins a man au Mario. Baba hawamjui Franco hawa.
sebene lipo?gitaa maana raha ya congo man hata nyimbo ikiwa ya taratibu unacheza kiboss boss hapo ndo koffi alipotuwin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…