Kwani ili uwashirikishe ufanyeje maana wote mnasema haiwezekani bila kutuambia kwanini haiwezekani na ili iwezekane unafanyaje ??????????? ( tuongee kwa hoja sio kama walevi wa mataputapu ndio mantiki ya uwepo wa JF)
Mkuu swala LA kumshirikisha chrisbrown kwenye wimbo wako sio swala dogo, unatakiwa uwe na qualifications za maana, at least angekuwa Kati ya A-LIST STARS IN AFRICA, na bado angehitaji nguvu kubwa ya mshawishi anayefahamiana na uongozi wa Chris kwasababu Chris alisema huwa hatozi gharama kwenye collable hilo linakuwa linaleta uzito... Upande wa Lil wyne, duuh nako shida maana yule sidhani kama anafanya bure collable, na wenzetu wameendelea sana kwahiyo gharama yake inakuwa sio kitoto.. Kama unakumbuka kcee alitaka kumshirikisha nick minaj akaambiwa gharama kama mil 630+ kwa wakati huo 2014 ambapo sasa hivi dola imepanda itakuwa imesogea zaidi, sasa hapo fanya makadirio yako upande wa lil wyne..
Sio kitoto kufanya collable na hao watu, na hata kama itawezekana haitakuwa na impact inayotakiwa.. Hakuna mafanikio bila juhudi, na Mb dog yupo vizuri kwahiyo anachotakiwa ni kukomaa zaidi kwa kuangalia game ipo vipi na sio kuruka step