Komaa na wazo lako usibabaike na mawazo ya wengine, utafika tu

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
Nataka kushare nanyi experience moja katika utafutaji.

Kuna kipindi nilipoteza muda sana kwa kuhama hama. Nilikuwa na marafiki zangu kadhaa watafutaji, na Mungu kawabariki yani mtu kupata milion 7 kwa miki au 50 kwa mwezi kwao ni kawaida.

Sasa nikawa ninaona kile ninachofanya mimi kama ninapoteza muda yani nachelewa kufika. Nikikaa nao yani wanaongelea mamilioni ya ela ama vile wanaongelea sijui nini. Hili jambo likawa linanipa moto sana. Usingizi sipati usiku ninawaza na mimi nifanyeje niende nao sawa. Kama wao wameweza wana nini na mimi nishindwe nina nini?

Nikajikuta nakuwa kama upepo, nikisikia wanawekeza huku na mimi speed naenda kuwekeza huko. Wao wanaweka mitaji mikubwa mimi kwa kusua sua naweza vipesa vyangu. Mara nyingine miradi inakufa mimi ninaumia maana nilichowekeza kilikuw kikubwa kwangu. Wenzangu hata hawaumii sana maana pesa kwao ina flow tu.

Yani, nilijikuta nahama hama kuanzia kilimo, ufugaji, samaki, miti, madini na kadhalika.
Mwisho nikawa jack of many trades master of none.

Nikakaa na kutafakari upya, nikaona nitakufa kwa presha binadamu tumezidiana, na muda mwingine inabidi kwenda slow. Wale jamaa walikuwa wana niisnpire ila nilikuwa inspired mpaka nilikuwa naelekea kuchanganyikiwa.

Ikabidi nianze kukaa mbali nao na kustick na plans zangu mwenyewe badala ya kustick na za kwao.
Nikawa sitaki tena kusikia story zao za mwanangu nimepiga milioni mia kwenye mradi flani maana zilikuwa zinanichanganya kabisa na kunivuruga kichwa.

Najua kuna watu wengi wana tatizo kama langu. Mafanikio ya watu ni inspiration kwetu, lakini kuna mtu ukitaka yafuatilia yanakufanya ujione huna maana, na umechelewa sana unaishia kupata stress. Ni vizuri kujifunza kupitia watu wanaofanya vizuri, ila jifunze na uache kufuatilia ufanye yako pia.

Na mafanikio hayaji ghafla, yanahitaji mtu awe coinsistent na kile anachokifanya. Stick na kkile unachokifanya hata kama ni kidogo lakini kifanye ukiwa na ndoto kubwa.

Muwe na siku njema
 
Za kuambiwa changanya na zako

Story za kupiga pesa kariakoo
Story za kupiga pesa mafinga mbao
Story za kupiga pesa mererani
Story za kupiga pesa migodini dhahabu
Story za kupiga pesa forex
 
Ndio maana ata kijiwen saiv atukuoni
Kila lakheli Mkuu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app

🤣 🤣 🤣 mtamuonaje wakati anakimbiza plan zake?
Mateso ya huyu jamaa yangu ni copy and paste na ya kwangu. Ukisikia mafanikio ya wengine unakuwa emotional sana, bila kujua kwamba kila mmoja kapangiwa kufanikiwa kwenye sekta yake tofauti. Ukimsikia mfuga kuku wa nyama na mayai utadhani kila mfuga kuku ni milionea. Ukimsikia muuza hardware utadhani wee unacheza ktk maisha.

Hali kadhalika ukimsikia mwenye duka kariakoo anashinnda China, unaweza kudhani wewe kwenye maisha umefeli sana. Lakini kumbe ni wewe tu hujajulia kipi kitakutoa, sio lazima iwe biashara ya kwenda China ana Dubai, kumbe hata hicho ukifanyacho, ukiacha kufanya kwa mazoea unatoka tu fresh. Tujipe moyo wakuu, tuko vizuri sana.
 
Mimi pia nilikua mtu wa namna hiyo kuacha jambo katikati na kufanya jambo lengine ila kwasasa nimeona ni vyema kutulia na jambo moja mpaka mwisho asante sana.
 
Za kuambiwa changanya na zako

Story za kupiga pesa kariakoo
Story za kupiga pesa mafinga mbao
Story za kupiga pesa mererani
Story za kupiga pesa migodini dhahabu
Story za kupiga pesa forex
Mkuu kwani unahis ni za uongo...watu wnaapiga pesa huko kwel...cha maana ni ku stay in your own lane...boresha unachofanya...pambania hapo
 
Watu wanapiga pesa sana, hata hao ninaowasema wana ela kinoma, ukiwapa sijui biashara ya kuzalisha milion kwa mwezi wanaona unawazingua tu.
 
Ok
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] mtamuonaje wakati anakimbiza plan zake?
Mateso ya huyu jamaa yangu ni copy and paste na ya kwangu. Ukisikia mafanikio ya wengine unakuwa emotional sana, bila kujua kwamba kila mmoja kapangiwa kufanikiwa kwenye sekta yake tofauti. Ukimsikia mfuga kuku wa nyama na mayai utadhani kila mfuga kuku ni milionea. Ukimsikia muuza hardware utadhani wee unacheza ktk maisha.

Hali kadhalika ukimsikia mwenye duka kariakoo anashinnda China, unaweza kudhani wewe kwenye maisha umefeli sana. Lakini kumbe ni wewe tu hujajulia kipi kitakutoa, sio lazima iwe biashara ya kwenda China ana Dubai, kumbe hata hicho ukifanyacho, ukiacha kufanya kwa mazoea unatoka tu fresh. Tujipe moyo wakuu, tuko vizuri sana.
 
Pole sana...
Ni kweli kabisa uliyosema... Fanya kile unachoweza mengine yatajipa yenyewe...

Cc: mahondaw
 
...it is hard to accomplish something positively,if you don't know of what you want...
 
Nataka kushare nanyi experience moja katika utafutaji.

Kuna kipindi nilipoteza muda sana kwa kuhama hama. Nilikuwa na marafiki zangu kadhaa watafutaji, na Mungu kawabariki yani mtu kupata milion 7 kwa miki au 50 kwa mwezi kwao ni kawaida.

Sasa nikawa ninaona kile ninachofanya mimi kama ninapoteza muda yani nachelewa kufika. Nikikaa nao yani wanaongelea mamilioni ya ela ama vile wanaongelea sijui nini. Hili jambo likawa linanipa moto sana. Usingizi sipati usiku ninawaza na mimi nifanyeje niende nao sawa. Kama wao wameweza wana nini na mimi nishindwe nina nini?

Nikajikuta nakuwa kama upepo, nikisikia wanawekeza huku na mimi speed naenda kuwekeza huko. Wao wanaweka mitaji mikubwa mimi kwa kusua sua naweza vipesa vyangu. Mara nyingine miradi inakufa mimi ninaumia maana nilichowekeza kilikuw kikubwa kwangu. Wenzangu hata hawaumii sana maana pesa kwao ina flow tu.

Yani, nilijikuta nahama hama kuanzia kilimo, ufugaji, samaki, miti, madini na kadhalika.
Mwisho nikawa jack of many trades master of none.

Nikakaa na kutafakari upya, nikaona nitakufa kwa presha binadamu tumezidiana, na muda mwingine inabidi kwenda slow. Wale jamaa walikuwa wana niisnpire ila nilikuwa inspired mpaka nilikuwa naelekea kuchanganyikiwa.

Ikabidi nianze kukaa mbali nao na kustick na plans zangu mwenyewe badala ya kustick na za kwao.
Nikawa sitaki tena kusikia story zao za mwanangu nimepiga milioni mia kwenye mradi flani maana zilikuwa zinanichanganya kabisa na kunivuruga kichwa.

Najua kuna watu wengi wana tatizo kama langu. Mafanikio ya watu ni inspiration kwetu, lakini kuna mtu ukitaka yafuatilia yanakufanya ujione huna maana, na umechelewa sana unaishia kupata stress. Ni vizuri kujifunza kupitia watu wanaofanya vizuri, ila jifunze na uache kufuatilia ufanye yako pia.

Na mafanikio hayaji ghafla, yanahitaji mtu awe coinsistent na kile anachokifanya. Stick na kkile unachokifanya hata kama ni kidogo lakini kifanye ukiwa na ndoto kubwa.

Muwe na siku njema
Mleta mada uko sahihi 100%. Safi kabisa. Sema sometimes watu wengine hawakuambii yaliyojificha ndani mwao. Wengine wanapiga sawa business unazoona wewe machoni mwako kumbe nyuma ya pazia kuna issues flani za uharamu zinaendelea. Hii unaweza usiniamini lkn nakuambia nikiwa na bonge la confidence.

Arusha kuna eti muuza karanga hizi za kutembeza barabarani hizi enzi hizo eti alinunua gari ndogo kali kwa hiyo biashara ya karanga ya kutembeza!! Alivuma sana enzi hizo.

Kwa akili yako kweli uuze zile karanga kijiko kimoja shs 20 uje umiliki gari ya milioni kumi mpaka kumi na tano inawezekana kweli? Sawa inaweza iwezekane lakn aisee it will take years and years za kufa mtu tusidanganyane lazima na mimi niongeze za kwangu akili.
 
Hata mm nikifikiriaga unavoingiza dollar zako huwa nadata knoma. najiulza kwan mm nakosa nn? pc ninayo,bando ninalo, english naijua khaaaa nafeli wapi? WTF is this lyf doing to me?
 
hata mm nikifikiriaga unavoingiza dollar zako huwa nadata knoma. najiulza kwan mm nakosa nn? pc ninayo,bando ninalo, english naijua khaaaa nafeli wapi? WTF is this lyf doing to me?
Inabidi ucheze kama pele na uwe consistent na ujifunze kila siku kitu kipya
 
Back
Top Bottom