Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nataka kushare nanyi experience moja katika utafutaji.
Kuna kipindi nilipoteza muda sana kwa kuhama hama. Nilikuwa na marafiki zangu kadhaa watafutaji, na Mungu kawabariki yani mtu kupata milion 7 kwa miki au 50 kwa mwezi kwao ni kawaida.
Sasa nikawa ninaona kile ninachofanya mimi kama ninapoteza muda yani nachelewa kufika. Nikikaa nao yani wanaongelea mamilioni ya ela ama vile wanaongelea sijui nini. Hili jambo likawa linanipa moto sana. Usingizi sipati usiku ninawaza na mimi nifanyeje niende nao sawa. Kama wao wameweza wana nini na mimi nishindwe nina nini?
Nikajikuta nakuwa kama upepo, nikisikia wanawekeza huku na mimi speed naenda kuwekeza huko. Wao wanaweka mitaji mikubwa mimi kwa kusua sua naweza vipesa vyangu. Mara nyingine miradi inakufa mimi ninaumia maana nilichowekeza kilikuw kikubwa kwangu. Wenzangu hata hawaumii sana maana pesa kwao ina flow tu.
Yani, nilijikuta nahama hama kuanzia kilimo, ufugaji, samaki, miti, madini na kadhalika.
Mwisho nikawa jack of many trades master of none.
Nikakaa na kutafakari upya, nikaona nitakufa kwa presha binadamu tumezidiana, na muda mwingine inabidi kwenda slow. Wale jamaa walikuwa wana niisnpire ila nilikuwa inspired mpaka nilikuwa naelekea kuchanganyikiwa.
Ikabidi nianze kukaa mbali nao na kustick na plans zangu mwenyewe badala ya kustick na za kwao.
Nikawa sitaki tena kusikia story zao za mwanangu nimepiga milioni mia kwenye mradi flani maana zilikuwa zinanichanganya kabisa na kunivuruga kichwa.
Najua kuna watu wengi wana tatizo kama langu. Mafanikio ya watu ni inspiration kwetu, lakini kuna mtu ukitaka yafuatilia yanakufanya ujione huna maana, na umechelewa sana unaishia kupata stress. Ni vizuri kujifunza kupitia watu wanaofanya vizuri, ila jifunze na uache kufuatilia ufanye yako pia.
Na mafanikio hayaji ghafla, yanahitaji mtu awe coinsistent na kile anachokifanya. Stick na kkile unachokifanya hata kama ni kidogo lakini kifanye ukiwa na ndoto kubwa.
Muwe na siku njema
One day yes mkuu[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] mtamuonaje wakati anakimbiza plan zake?
Mateso ya huyu jamaa yangu ni copy and paste na ya kwangu. Ukisikia mafanikio ya wengine unakuwa emotional sana, bila kujua kwamba kila mmoja kapangiwa kufanikiwa kwenye sekta yake tofauti. Ukimsikia mfuga kuku wa nyama na mayai utadhani kila mfuga kuku ni milionea. Ukimsikia muuza hardware utadhani wee unacheza ktk maisha.
Hali kadhalika ukimsikia mwenye duka kariakoo anashinnda China, unaweza kudhani wewe kwenye maisha umefeli sana. Lakini kumbe ni wewe tu hujajulia kipi kitakutoa, sio lazima iwe biashara ya kwenda China ana Dubai, kumbe hata hicho ukifanyacho, ukiacha kufanya kwa mazoea unatoka tu fresh. Tujipe moyo wakuu, tuko vizuri sana.
Nakuombea iwe hivyo mkuu. One day ukipata nafasi tubadilishane mawazo kwa hili na lileOne day yes mkuu