Komando mstaafu na aliyeshriki Jaribio la Mapinduzi dhidi ya Nyerere mwaka 1982, Christopher Kadego alitekwa na kuuwawa kwa amri ya Rais Magufuli

Komando mstaafu na aliyeshriki Jaribio la Mapinduzi dhidi ya Nyerere mwaka 1982, Christopher Kadego alitekwa na kuuwawa kwa amri ya Rais Magufuli

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
18,960
Reaction score
67,654
Naendelea kusoma kitabu cha mwandishi Erik Kabendera, In the name of the President.

Kabendera anafichua juu ya tukio la mauaji ya Komando mstaafu wa JWTZ na ambaye alishiriki katika Jaribio la Mapinduzi la Mwaka 1982 dhidi ya Serikali ya Nyerere.

Kabendera anasema hayo wakati alipokuwa Gereza la Segerea wakati alipopewa kesi ya uhujumu uchumi, utakatishaji wa fedha pamoja ukwepaji kodi. “ Nilikuwa selo wakati nilipopewa kikaratasi kutoka kwa mtu asiyejulikana akiniambia kuwa Chistopher Kadego alikamatwa siku 3 nyuma kabla ya kukamatwa kwangu kisha kupigwa risasi na watu wasiojulikana.”

Kabendera anaendelea kufafanua; Kadego nilimfahamu kama miaka 15 iliyopita na alikuwa mtu mwema, sema kitendo chake kushiriki katika makundi mbalimbali ya waasi kama lile kundi la Kabila katika Vita dhidi ya Mobutu mwaka 1997 na baadae kupinga baadhi ya maamuzi ya Magufuli nafikiri matatizo yalianzia hapo.

Magufuli akapenyezewa taarifa kuwa Kadego alikuwa ni Komando mstaafu hatari na aliyeshiriki jaribio la kumpindua Nyerere.

Ikumbukwe Kadego alikuwa na miaka 67 hivyo hakuwa Kadego yule kijanaa machachari. Hayati Magufuli aliagiza Kadego “ashughulikiwe” maana alikuwa anahatarisha usalama wake.

Akatekwa na kupigwa risasi na watu waliokuja kujulikana baadae kuwa ni watu wa ikulu.

My note;
Hayati alikuwa muoga sana, unamuuaje mzee wa miaka 67? Hayati hakuwa na ubinadamu kabisa.
 
If all those rumours are real...
He was a SADIST president ever..
20241121_163920.jpg
 
Eti mtu GEREZANI halafu mtu huyo huyo apate habari mbaya tu zaidi ya 100 kumhusu mtu mmoja tu....... tena taarifa hizo akizipata akiwa gerezani tena kutoka vyanzo tofauti....!
UFADHILI na NGUVU nyingi inayotumika kumchafua MAGUFULI unatia mashaka sana juu ya wenzetu hawa wenye ufadhili wa moja kwa moja wa nchi za ULAYA......
(Nimefurahi kwa sehemu kwa TRUMP kuifutilia mbali USAID kwani inafadhili baadhi ya machafuko kwenye nchi kama upuuzi huu)

NB: baada ya USAID kufaliki, tutegemee wanasiasa wengi "waliojikimbiza" kurejea na kuacha upuuzi wao wa kuichafua nchi yetu pendwa kwa manufaa yao na ya WEUPE
 
Stori naona haijajitosheleza kwanza kabendera anasema alipata kikaratasi akiwa gerezani hana uhakika wowote na hiyo taarifa.
Kadego alifanya kosa gani/ alikosana nini na Magufuli mpaka kumtumia watu?
Hahahaha, alikua anajazia kurasa za kitabu Kwa story km hizo, eti alipitishiwa kikaratasi as if ni Bonge la Siri alipewa
 
Back
Top Bottom