Naendelea kusoma kitabu cha mwandishi Erik Kabendera, In the name of the President.
Kabendera anafichua juu ya tukio la mauaji ya Komando mstaafu wa JWTZ na ambaye alishiriki katika Jaribio la Mapinduzi la Mwaka 1982 dhidi ya Serikali ya Nyerere.
Kabendera anasema hayo wakati alipokuwa Gereza la Segerea wakati alipopewa kesi ya uhujumu uchumi, utakatishaji wa fedha pamoja ukwepaji kodi. “ Nilikuwa selo wakati nilipopewa kikaratasi kutoka kwa mtu asiyejulikana akiniambia kuwa Chistopher Kadego alikamatwa siku 3 nyuma kabla ya kukamatwa kwangu kisha kupigwa risasi na watu wasiojulikana.”
Kabendera anaendelea kufafanua; Kadego nilimfahamu kama miaka 15 iliyopita na alikuwa mtu mwema, sema kitendo chake kushiriki katika makundi mbalimbali ya waasi kama lile kundi la Kabila katika Vita dhidi ya Mobutu mwaka 1997 na baadae kupinga baadhi ya maamuzi ya Magufuli nafikiri matatizo yalianzia hapo.
Magufuli akapenyezewa taarifa kuwa Kadego alikuwa ni Komando mstaafu hatari na aliyeshiriki jaribio la kumpindua Nyerere.
Ikumbukwe Kadego alikuwa na miaka 67 hivyo hakuwa Kadego yule kijanaa machachari. Hayati Magufuli aliagiza Kadego “ashughulikiwe” maana alikuwa anahatarisha usalama wake.
Akatekwa na kupigwa risasi na watu waliokuja kujulikana baadae kuwa ni watu wa ikulu.
My note;
Hayati alikuwa muoga sana, unamuuaje mzee wa miaka 67? Hayati hakuwa na ubinadamu kabisa.