Kombe la Cecafa Senior Challenge 2009

KOCHA Marcio Maximo anajua atakuwa kwenye wakati ngumu zaidi kuliko kipindi chochote alichokaa Tanzania endapo kikosi chake cha Kilimanjaro Stars kitapoteza mchezo wa leo dhidi ya ndugu zao wa Zanzibar Heroes katika mechi ya kufa au kupona ya michuano ya Chalenji.
Mbrazil alishudia Kilimanjaro Stars wakipokea kipigo cha mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya mabingwa watetezi, Uganda, The Cranes.
Katika mchezo huo, Zanzibar ikishinda itakuwa imejihakikishia nafasi ya kuvuka hatua ya makundi huku Kili Stars ikibakiza saa chache za kuendelea kuishi mjini hapa ikishindwa kuvuka hatua hiyo ya awali ya michuano ya mwaka huu.
Hii ni mara ya pili kwa timu hizo kukutana katika mchezo wa kuamua hatma yao, katika michuano hiyo iliyofanyika mwezi Januari mwaka huu nchini Uganda, Tanzania ilikwenda kwenye mchezo dhidi ya Zanzibar wakihitaji kushinda ili kufufua matumaini yao ya kusoga mbele kama ilivyo sasa.
Katika mchezo huo uliochezwa mjini Kampala kwenye Uwanja wa Nakivubo, Kilimanjaro Stars ili shinda kwa mabao 2-1 shukrani kwa Danny Mrwanda na Athumani Idd, huku lile la kufutia machozi la Zanzibar likifungwa na Nadir Haroub ‘Canavaro’.
Hali hiyo imemfanya kocha Maximo kusema kuwa hakuna shaka kwamba itakuwa ni kazi ngumu kwao hasa ikizingatiwa ukweli kuwa wachezaji wa timu hizo mbili wanajuana udhaifu, ubora.
“Wao wana pointi mkononi na mabao mengi tofauti na sisi. Mchezo huu utakuwa mgumu kwa vile wachezaji wetu wanajuana, lakini naamini kwa morali ya wachezaji wangu niliyoiona katika kipindi cha pili cha mechi dhidi ya Uganda inatia matumaini.
“Tutatumia mfumo wa soka ya kushambulia na kukaba nafasi kwa vile uwezo huo tunao na tuna wachezaji ambao wanaweza kufanya hiyo kazi. Kwenye mchezo na Uganda tuliathirika baada ya Juma Nyosso kuonyeshwa kadi nyekundu.
“Kwa hiyo kila mmoja ilibidi afanye kazi ya ziada ya kukaba, ndiyo maana ikabidi na mfumo ubadilike. Lakini, katika mchezo dhidi ya Zanzibar, kikosi chote kitakuwepo. “Kufungwa kwenye mechi ya kwanza hakuwezi kutufanya tupoteze matumaini na muda, bado tuna mechi mbili , dhidi ya Burundi na Zanzibar leo, tushirikiane tufanye kazi hawa vijana wana uelekeo.”
Zanzibar ambayo inalingia kumbukumbu yake ya ushindi wa kishindo wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Bara katika fainali zilizochezwa nchini Kenya, Oktoba 10, 1967 wakati huo lijulikana kama Kombe Palmares Chalenji.
Katika michuano iliyofanyika mwaka 2004 nchini Ethiopia ilishudia timu hizo mbili zikiaga mashindano hatua ya awali kwa Zanzibar kupata pointi tatu pekee baada ya kuinyuka Tanzania Bat kwa mabao 4-2.
Mabao ya Zanzibar yaliyofungwa na Said Abdella dakika ya 6 kwa mkwaju wa penalti, Abdella Juma 29, 73, Twaha Mohamed 85; huku yale ya Kilimanjaro Stars yakifungwa na Mecky Mexime 23, Athumani Machupa 32.
Kocha wa Zanzibar, Hemed Morocco alisisitiza kuwa mchezo wa leo utakuwa mgumu, lakini hawaihofii Kili Stars hata kidogo ingawa wanajua ni timu ngumu. “Hapa tumekuja na jeshi kamili, ndio maana unaona watu wanacheza soka ya ukweli na ushindi unapatikana na utakuwa mkubwa, sisi hatuna maneno mengi njooni muone soka yetu dhidi ya Kili Stars.
“Tunataka kuendeleza rekodi yetu ya ushindi na kwa vyovyoe vile hatutakubali kushindwa,”alisisitiza kocha huyo akiungwa mkono na kiungo Abdi Kassim anayeichezea Yanga ambaye pia ni nahodha.
Mchezo huo unatazamiwa kuwa na ushindani wa aina yake hasa kutokana Zanzibar Heroes kuwa nao Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwenye safu ya ulinzi pamoja na Abdi Kassim na Abdulrahim Amour kwenye kiungo, wote ambao wanaichezea Taifa Stars chini ya Maximo.
Kili Stars imenufaishwa na kuwapo kwa Henry Joseph kwenye kiungo kwani ameonyesha mabadiliko makubwa kiuchezaji pale kocha Maximo alipomwingiza katika kipindi cha pili kwenye mechi dhidi ya Uganda.
Tanzania Bara pamoja na kuwa miongoni mwa waanzilishi wa michuano hiyo mikongwe 1926 ilifanikiwa kutwaa taji hilo kwa mara kwanza mwaka 1974 na kusubili kwa miaka 20 kuchukua kwa mara pili mwaka1994, huku ndugu zake Zanzibar wakitwaa ubingwa mara moja mwaka 1995.
source:zanzibar yetu web blog
 
Leo ni kumharibu mtu tu.
Kila la kheri Zanzibar Heroes na nawatakia mchezo mzuri ndgu zetu wa bara wajitahidi tusiwafunge nyingi kama Burundi.
 
DUUUUUUU labda wanatubebaaa.............
 
Hatimaye the kilimanjaro stars leo imewapa faraja watanganyika baada ya kuwachapa wazanzibari bao 1-0 kwenye kombe la chalenji huko mumiasi kenya
bao la tanganyika lilifungwa na mrisho ngasa
 
Mkuu, acha kuamsha mengine

Si kuamsha Mengine..

Hujawahi kusikia hawa jamaa wazenji wanadai nchi yao.

Sasa wakiipata, wewe nchi yako itakuwa nini?

Msiogope na visivyoogopeka men.
TANGANYIKA IPO...NA I HAI!...huh!
 
nafahamu forum hii ni ya michezo na sanaa ila panapohitaji kueleweshana tutaeleweshana
tanzania ni muungano wa tanganyika na zanzibar sasa leo zanzibar imecheza na sehemu ya pili ya tanzania, ni ipi hiyo kama sio tanganyika?
tanganyika ni nchi yetu kama hauijui au hatuidai ni ujinga wetu wenyewe wanaojua haki yao wanadai kutambuliwa kwa nchi yao kwenye masuala ya nje ya muungano vipi na sisi tusidai yetu?



by the way bora kilimanjaro stars wameanza kuvaa jezi nyeupe labda zitakuwa na bahati kwetu maana hata ghana baada ya makumi ya miaka ya juvaa jezi za njano zilizoshindwa kuwasaidia sasa wanavaa jezi nyeupe nazo zimekuwa na bahati kwao haha haa haa
 
ingekuwa kwenye inchi ambazo wameinvest kwenye football MAKSIMO ANGEKUWA HANA KAZI SIKU NYINGI SANA ZILIZOPITA
 
Too late too little!
una maana gani? mbona point ni sawa na zenji tofauti ni magoli, hapo labda huyo mganda kama atamchapa mtu kwenye game lake la pili ila mpaka sasa vijana wanayo nafasi, game la tatu ndio litatoa picha nzuri zaidi.
 
tanganyika ni nchi yetu kama hauijui au hatuidai ni ujinga wetu wenyewe wanaojua haki yao wanadai kutambuliwa kwa nchi yao kwenye masuala ya nje ya muungano vipi na sisi tusidai yetu?

Hivi Rais wa Tanganyika ni nani vile? Na kama Tanganyika ipo kwa nini unasema tuidai?
 
Mpira wa miguu kweli sometime unaweza ukakufanya uchanganyikiwe, cheki jinsi zenji walivyomtandika burundi (4-0), then uganda walivyompiga kili stars (2-0) then malizia kutathmini mgeuzo wa bara kwa zenji (1-0), kwa kile kipigo cha zenji kwa waburundi ilikuwa dhahili kuwa kili atabeba mengi ila ndio hivyo tena wabara wamepata pa kunyoa leo....... wenye shemeji zao wazenji poleni.. tehtehteh
 
Zanzibar si timu ya kiuchapa tanzania. Naamini tutavuka hatua na kukutana na Uganda kwa mara nyingine. hawa jamaa huwa wanajipigia tu hata hatuwasumbui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…