Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 144
KOCHA Marcio Maximo anajua atakuwa kwenye wakati ngumu zaidi kuliko kipindi chochote alichokaa Tanzania endapo kikosi chake cha Kilimanjaro Stars kitapoteza mchezo wa leo dhidi ya ndugu zao wa Zanzibar Heroes katika mechi ya kufa au kupona ya michuano ya Chalenji.
Mbrazil alishudia Kilimanjaro Stars wakipokea kipigo cha mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya mabingwa watetezi, Uganda, The Cranes.
Katika mchezo huo, Zanzibar ikishinda itakuwa imejihakikishia nafasi ya kuvuka hatua ya makundi huku Kili Stars ikibakiza saa chache za kuendelea kuishi mjini hapa ikishindwa kuvuka hatua hiyo ya awali ya michuano ya mwaka huu.
Hii ni mara ya pili kwa timu hizo kukutana katika mchezo wa kuamua hatma yao, katika michuano hiyo iliyofanyika mwezi Januari mwaka huu nchini Uganda, Tanzania ilikwenda kwenye mchezo dhidi ya Zanzibar wakihitaji kushinda ili kufufua matumaini yao ya kusoga mbele kama ilivyo sasa.
Katika mchezo huo uliochezwa mjini Kampala kwenye Uwanja wa Nakivubo, Kilimanjaro Stars ili shinda kwa mabao 2-1 shukrani kwa Danny Mrwanda na Athumani Idd, huku lile la kufutia machozi la Zanzibar likifungwa na Nadir Haroub Canavaro.
Hali hiyo imemfanya kocha Maximo kusema kuwa hakuna shaka kwamba itakuwa ni kazi ngumu kwao hasa ikizingatiwa ukweli kuwa wachezaji wa timu hizo mbili wanajuana udhaifu, ubora.
Wao wana pointi mkononi na mabao mengi tofauti na sisi. Mchezo huu utakuwa mgumu kwa vile wachezaji wetu wanajuana, lakini naamini kwa morali ya wachezaji wangu niliyoiona katika kipindi cha pili cha mechi dhidi ya Uganda inatia matumaini.
Tutatumia mfumo wa soka ya kushambulia na kukaba nafasi kwa vile uwezo huo tunao na tuna wachezaji ambao wanaweza kufanya hiyo kazi. Kwenye mchezo na Uganda tuliathirika baada ya Juma Nyosso kuonyeshwa kadi nyekundu.
Kwa hiyo kila mmoja ilibidi afanye kazi ya ziada ya kukaba, ndiyo maana ikabidi na mfumo ubadilike. Lakini, katika mchezo dhidi ya Zanzibar, kikosi chote kitakuwepo. Kufungwa kwenye mechi ya kwanza hakuwezi kutufanya tupoteze matumaini na muda, bado tuna mechi mbili , dhidi ya Burundi na Zanzibar leo, tushirikiane tufanye kazi hawa vijana wana uelekeo.
Zanzibar ambayo inalingia kumbukumbu yake ya ushindi wa kishindo wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Bara katika fainali zilizochezwa nchini Kenya, Oktoba 10, 1967 wakati huo lijulikana kama Kombe Palmares Chalenji.
Katika michuano iliyofanyika mwaka 2004 nchini Ethiopia ilishudia timu hizo mbili zikiaga mashindano hatua ya awali kwa Zanzibar kupata pointi tatu pekee baada ya kuinyuka Tanzania Bat kwa mabao 4-2.
Mabao ya Zanzibar yaliyofungwa na Said Abdella dakika ya 6 kwa mkwaju wa penalti, Abdella Juma 29, 73, Twaha Mohamed 85; huku yale ya Kilimanjaro Stars yakifungwa na Mecky Mexime 23, Athumani Machupa 32.
Kocha wa Zanzibar, Hemed Morocco alisisitiza kuwa mchezo wa leo utakuwa mgumu, lakini hawaihofii Kili Stars hata kidogo ingawa wanajua ni timu ngumu. Hapa tumekuja na jeshi kamili, ndio maana unaona watu wanacheza soka ya ukweli na ushindi unapatikana na utakuwa mkubwa, sisi hatuna maneno mengi njooni muone soka yetu dhidi ya Kili Stars.
Tunataka kuendeleza rekodi yetu ya ushindi na kwa vyovyoe vile hatutakubali kushindwa,alisisitiza kocha huyo akiungwa mkono na kiungo Abdi Kassim anayeichezea Yanga ambaye pia ni nahodha.
Mchezo huo unatazamiwa kuwa na ushindani wa aina yake hasa kutokana Zanzibar Heroes kuwa nao Nadir Haroub Cannavaro kwenye safu ya ulinzi pamoja na Abdi Kassim na Abdulrahim Amour kwenye kiungo, wote ambao wanaichezea Taifa Stars chini ya Maximo.
Kili Stars imenufaishwa na kuwapo kwa Henry Joseph kwenye kiungo kwani ameonyesha mabadiliko makubwa kiuchezaji pale kocha Maximo alipomwingiza katika kipindi cha pili kwenye mechi dhidi ya Uganda.
Tanzania Bara pamoja na kuwa miongoni mwa waanzilishi wa michuano hiyo mikongwe 1926 ilifanikiwa kutwaa taji hilo kwa mara kwanza mwaka 1974 na kusubili kwa miaka 20 kuchukua kwa mara pili mwaka1994, huku ndugu zake Zanzibar wakitwaa ubingwa mara moja mwaka 1995.
source:zanzibar yetu web blog