Kombe la Dunia 2022: Tunavikosa sana vionjo tulivyovizoea kwenye mitanange ya Kombe la Dunia

Na hatuwezi kuja kuviona Kwa sababu siku hizi wachezaji hawachezi kuonesha vipaji vyao bali wanaucheza mfumo wa kocha

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
Ni kweli hatuwezi kuja kuviona tena kwa sababu Lengo kuu la mpira limebadilika sana!! Mpira umekuwa biashara zaidi kuliko burudani!! Hata nchi za Amerika ya kusini ambapo mcheza soka alikuwa anajihesabu kama anacheza ngoma na lengo kuu likiwa kuonesha kipaji na kuburudisha watazamaji, siku hizi wameiga soka la ulaya la kasi na pasi ili mradi goli lipatikane!
 
Ukishamtaja babe wangu Ronaldinho gaucho ushanivuruga akili. Nilianza kuangalia mpira 2002 nikiwa mdogo madaftari yangu ya secondari yamechorwa picha za Ronaldinho bae
.
 
Ronaldinho aliendaga wapi? Nina miaka sijamsikia
 
Mpira huo wa individual skills umeshapitwa na wakati hakuna kocha anayetaka wachezaji kama hao mpira wa sasa ni wa kwenye kitabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…