Kombe la Shirikisho Africa: Gor Mahia yaifunga Yanga kwa magoli 4-0

kovai tamil taiga

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2013
Posts
1,451
Reaction score
2,059
Timu ya soka ya Yanga ya Tanzania imeendelea kufanya vibaya katika mechi za makundi kugombea kombe la Shirikisho la Afrika baada ya kutandikwa kwa magoli manne kwa bila dhidi ya wenyeji wao Gor Mahia ya Kenya

Magoli ya washindi katika mechi hiyo yalifungwa na Tusiyenge 22" , Guikan 45" , Haji Mwinyi 65" (Own Goal) na Guikan tena 86"
 
Ni Aibu kubwa
Mtu unajitoa Kagame ili kujiandaa na mechi za kimataifa
unaenda kutuaibisha kama Taifa!!
Tuombe radhi Taifa! Hao walikua wanawakilisha badge ya Yanga sio Tanzania, ko wamehiabisha badge ya Yanga.
Povu ruhusa
 
Kama kawa wakishinda wanawakilisha taifa wakifungwa ya kwao na mashabiki wao!
 
4G ni mali halisi ya Yanga. Hairuhusiwi kuuzwa
 
Matokeo kat ya Gor mahia vs Yanga ni 4 - Bashite
 
Ni Aibu kubwa
Mtu unajitoa Kagame ili kujiandaa na mechi za kimataifa
unaenda kutuaibisha kama Taifa!!
Walijitoa Kagame kwa kisingizio cha kujiandaa ili wachezaji wasichoke halafu wanakuja kufungwa 4G na mtu aliyecheza kagame hadi nusu fainali
 
Nampongeza Aliyewapa [HASHTAG]#NdalaFC[/HASHTAG] wazo la Kujitoa [HASHTAG]#KagameCup[/HASHTAG] kwani imewasaidia Kupunguza idadi ya Magoli, Venginevyo Wangelikula goli 10 Kwa 0.
 
Ni vema yanga wakashauriwa kupumzika Michezo ya Kimataifa hadi watakapo maliza matatizo yao kwanza lasivyo naona Dozen ya Magoli inanukia..,
Naona wanamalizia mechi 3 za mwisho za CAF kwa kuwa hairuhusiwi kujitoa.Watapumzika mpaka 2022 hivi maana kwa timu hii ubingwa wa ligi na ASFC watasahau .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…