Kombe la Shirikisho Afrika: Yanga vs BDF XI [14 Feb 2014]

Kila siku kukataa mechi zisionyeshwe tu sijui inawasaidia nini??

Tena hawa viongoz wa Yanga wapumbavu sana, Mimi naipenda yanga lakini kwa hili la Yusuph Manji na akina Jerry Muro la kukataa game ya yanga vs bdf kuoneshwa live ni upumbavu. Wanategemea wapenz wa yanga wanaoishi mikoani wataionea wapi yanga!!! Miaka nenda rudi wanakusanya hayo mapato ya mlangoni lakin hata uwanja wa mazoez hakuna, iweje wamekomalia azam tv!! Manji acha ujinga bhana, Wanajangwani wengi hatujafurahishwa na hili.
 
Azam wamegoma kutuonesha gemu badala take wameweka ya Kenya ...uzalendo is a big question in Tz

Yanga ndo waliogomea match kuonyeshwa live na azam tv, Ujinga wa MANJI na maslahi yake ndio yanayotutesa wanajangwani wengi.
 
Kipindi cha pili kimeanza...

Yanga 1 - 0 BDF XI
 

Hili jambo limeudhi wengi sana huku kitaa. Timu yenye base ya mashabiki nchi nzima na nje kuzuia game isionyeshwe ni ushamba na mambo ya kizamani mno. Ushindi wa leo hautaleta hamasa iliyotarajiwa kufuatia kasoro hii. Wengi wamechukia sana
 
Safi sana manji,hatutaki unyonyaji cc

Acha kushadadia huu ujinga bhana, mara ngapi yanga wamekuwa wakikusanya hayo mamilioni lakin hayajulikani yanakoishia!!?
 
Yanga wanapata bao la pili...

Amisi Tambwe anaunganisha kwa majalo iliyomiminwa na Ngassa...

Dk 56

Yanga 2 - 0 BDF XI
 
Hili jambo limeudhi wengi sana huku kitaa. Timu yenye base ya mashabiki nchi nzima na nje kuzuia game isionyeshwe ni ushamba na mambo ya kizamani mno. Ushindi wa leo hautaleta hamasa iliyotarajiwa kufuatia kasoro hii. Wengi wamechukia sana

Mimi sijachukia,unataka yanga ipate pesa kupitia kwa nani..kabla ya azam tv ulikuwa unaangalia wapi mechi..kila kitu tu kinakwanda kimaslahi na sio kufurahishana kinafki
 
wabongo hawana uzalendo,mi simba lakini hii tabia ya simba kushangilia club hii ya Botswana imeniudhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…