Kombe la Shirikisho Afrika: Yanga vs BDF XI [14 Feb 2014]

Kombe la Shirikisho Afrika: Yanga vs BDF XI [14 Feb 2014]

Watu8

Platinum Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
73,773
Reaction score
102,126
Mechi za kombe la shirikisho barani Afrika kwa ngazi ya vilabu zinaanza mwishoni mwa wiki hii.

Wawakilishi wa Tanzania Bara Young Africans SC watakuwa nyumbani wakimenyana na BDF XI kutoka Botswana katika mechi ya kwanza ya mzunguko wa kwanza.

Hali ya hewa ya jiji la Dar es Salaam kwa siku ya leo ni jua, vipindi vifupi vya mawingu huku upepo ukivuma kutoka kaskazini mashariki kuelekea kusini magharibi.

Yanga SC 2 (FT) 0 BDF XI
Dk.1, 56 Amisi Tambwe

1600 PM

Waamuzi:
Thierry Nkurunzinza (Bur)
Ramadhani Nijimbere (Bur)
George Gatogato (Bur)

Get
=====================

UPDATES:

MMGL0060.jpg

Mchezaji wa timu ya Yanga,Mrisho Khalfan Ngassa akiwania mpira na Mchezaji wa timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es salaam leo

MMGL0118.jpg

Mashabiki ya Yanga wakifuatilia mchezo kwa makini

Mpira umekwisha na matokeo ni Yanga SC 2 - 0 BDF XI

Magoli yote mawili yamefungwa na Hamis Tambwe dakika ya kwanza ya mchezo na dakika ya 55 ya mchezo.

Watu8 hebu tujuze sisi ambao tupo mikoani tutauonaje mtanange huu wa Kuala Lumpur...? Au ndo tutegemee radio pekee?
 
Last edited by a moderator:
Watu8 hebu tujuze sisi ambao tupo mikoani tutauonaje mtanange huu wa Kuala Lumpur...? Au ndo tutegemee radio pekee?

Mkuu sijajua bado TV gani itakuwa hewani...

Azam One wao watakuwa Uganda wakionesha mechi ya URA...

Sijui kwa stesheni zao nyingine zioneshazo michezo...
 
Last edited by a moderator:
Nadhani updates zitapatikana hapahapa maana jf ni kila kitu
 
Hata sijui Leo nguvu zangu za ushangiliaji nizielekeze wapi
 
Hata sijui Leo nguvu zangu za ushangiliaji nizielekeze wapi

Timu ya wananchi...

Usiwe kama mwenyekiti wenu anayesubiri atakachokiona uwanjani...
 
Watu8 hebu tujuze sisi ambao tupo mikoani tutauonaje mtanange huu wa Kuala Lumpur...? Au ndo tutegemee radio pekee?

Azam tv kwenye azam two leo katika ratiba ya vipindi vyao wameweka GAME ya YANGA vs BDF XI kuanzia saa 15:00-18:30, Ila sina uhakika sana kama Azam tv wamefikia makubaliano na uongoz wa Yanga ili hii Game LIVE.....
 
Last edited by a moderator:
Azam tv kwenye azam two leo katika ratiba ya vipindi vyao wameweka GAME ya YANGA vs BDF XI kuanzia saa 15:00-18:30, Ila sina uhakika sana kama Azam tv wamefikia makubaliano na uongoz wa Yanga ili hii Game LIVE.....
Watakuwa wamekubaliana.
 
Sisi kutoka mji wa Gaborone sijui hawa BDF kumi na moja watatutoa kimasomaso au ndo watambwelambwela.

Umeshaanza kutengeneza mazingira ya kulikimbia jukwaa kuanzia saa 16:00-18:30. Uncle NGASSA ameahidi kuafundisha mpira hawa MAKHIRIKHIRI. Pole yenu watani na kesho polisi moro wameahidi kuwafundisha namna ya kumkamata mwiz kimya kimya.
 
Nadhani updates zitapatikana hapahapa maana jf ni kila kitu

Siyo Zitapatikana Bali Tayari Zimeshapatikana Na Ni Kwamba Timu Yangu Pendwa Ya Yanga FC Leo Itaibuka Na Ushindi Wa Goli 7 Kwa 0 Na Magoli Yote Yatafungwa Na Yussuph Maji Atapiga Hatrick, Jerry Muro Nae Atapiga Hatrick Huku Commandoo Wao Carlos Nae Akitupia Kamoko. Happy Valentine Yanga Wote Na Tupeni Leo Raha Ya Mtakatifu Valentino Kwa Ushindi Mnono Na Msituaibishe Simba Wote Leo Tupo Nyuma Yenu TUNAWAPUMULIA Kwa Kuwashangilia.
 
Back
Top Bottom