Kwahiyo sio tena kikosi kipana?
Kikosi kipana kipo, kwani kila timu ina kikosi kipana kwakuwa licha ya kuwa na kikosi cha kwanza kila timu ina kikosi cha pili.
Ila kikosi cha pili cha Simba Sports ni cha hovyo sana.
Wachezaji wanapiga mipira hovyo tu na hawana umakini uwanjani.
Sio kwamba kwakuwa tumefungwa na Mashujaa Sports Club hapana.
Kikosi hicho kimecheza mpira wa hovyo sana, na hata siku ile na KMC kilikata pumzi mapema kikawa kinalinda goli tu kipindi cha pili.
Mashujaa wamestahili ushindi maana walicheza vizuri kupita akina Ali Selemani.
Hiki kikosi kunakula mshahara wa bure kabisa kwa mgongo wa wenzao.
Unashangaa hata huko mazoezini wanafanya kitu gani, wanabutua tu mipira.
Wakifika golini kazi yao ni kupiga mpita nje ya goli tu.
Ona kaingia Chama kapiga faulo iliyolenga goli na ikazaa goli.
Hao vijana wameenda hadi Uturuki lifanya mazoezi lakini hawana shukrani hata ya kucheza kwa umakini uwanjani, walizidiwa hata na wenzao wanaocheza mpira kwa kujitolea tu, na wanaishi kwa posho ndogo tu.
Wanarukaruka tu uwanjani muda wote na kocha anawaangalia tu. Kwa wakweli Wanaighalimu timu sana na kuifedhehesha nembo ya Simba Sports.
Hii Ni Aibu Kwetu sisi Wadau wa Simba Sports Wamesababisha tukejeriwe mwaka mzima, huku mishahara wanakula wao.
Shame On Them.