Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC): Simba SC 2-3 Mashujaa FC | Uwanja wa Taifa, Dar es salaam | 26/12/2018

Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC): Simba SC 2-3 Mashujaa FC | Uwanja wa Taifa, Dar es salaam | 26/12/2018

Dah dida kapodoaaa

Heri ya Christmas ,hii zawadi ya Boxing Day ,ni wewe ndio unaitoa kupitia Mashujaa ?[/QUOTE]
 
Sisi Wadau wa Simba Sports, tuko radhi na maamuzi yoyote watakao fanya viongizi kwa hawa vijana wa Simba waliocheza Leo.
Kama Bechi waache wakae benchi hadi mikataba yao iishe, kama mkopo basi wapelekwe mkopo.
Ni kwamba hawana kiwango cha kuichezea Simba Sports.
Ukiiangalia timu kama Barcalona pamoja na uwezo wao wote ule, kila mechi wanaingiza full mziki wote.
Kama wanataka kujaribu wachezaji wapya wanawaweka wawili au watatu.
Yaani Simba wanamchezesha mchezaji anaitwa Selemani, na anarukaruka tu uwanjani dakika zote na anaachwa tu.
Viongozi na Bechi la ufundi hebu watendeeni haki wadau wa Simba.
Mnapewa kila kitu, lakini mnaonekana hamtimizi wajibu wenu.
 
Kwahiyo sio tena kikosi kipana?
 
Kwahiyo sio tena kikosi kipana?
Kikosi kipana kipo, kwani kila timu ina kikosi kipana kwakuwa licha ya kuwa na kikosi cha kwanza kila timu ina kikosi cha pili.
Ila kikosi cha pili cha Simba Sports ni cha hovyo sana.
Wachezaji wanapiga mipira hovyo tu na hawana umakini uwanjani.
Sio kwamba kwakuwa tumefungwa na Mashujaa Sports Club hapana.
Kikosi hicho kimecheza mpira wa hovyo sana, na hata siku ile na KMC kilikata pumzi mapema kikawa kinalinda goli tu kipindi cha pili.
Mashujaa wamestahili ushindi maana walicheza vizuri kupita akina Ali Selemani.
Hiki kikosi kunakula mshahara wa bure kabisa kwa mgongo wa wenzao.
Unashangaa hata huko mazoezini wanafanya kitu gani, wanabutua tu mipira.
Wakifika golini kazi yao ni kupiga mpita nje ya goli tu.
Ona kaingia Chama kapiga faulo iliyolenga goli na ikazaa goli.
Hao vijana wameenda hadi Uturuki lifanya mazoezi lakini hawana shukrani hata ya kucheza kwa umakini uwanjani, walizidiwa hata na wenzao wanaocheza mpira kwa kujitolea tu, na wanaishi kwa posho ndogo tu.
Wanarukaruka tu uwanjani muda wote na kocha anawaangalia tu. Kwa wakweli Wanaighalimu timu sana na kuifedhehesha nembo ya Simba Sports.
Hii Ni Aibu Kwetu sisi Wadau wa Simba Sports Wamesababisha tukejeriwe mwaka mzima, huku mishahara wanakula wao.
Shame On Them.
 
Vijana waTimu ya Pili ya Simba wamebahatika kuwa katika timu Bora kabisa na yenye mipango thabiti ya maendeleo.
Hii fulsa inaliliwa na wachezaji wengi wa hapa Afrika Mashariki na Kati.
Wakipata fulsa ya kuipigania timu wanarukaruka tu. Wakikaa Benchi wanajifanya kunung'unika kwa huzuni.
Hii nafasi watakuja kuikumbuka maisha yao yote ya soka, kama watakuja kuipoteza kwa ujinga wao tu.
Mtu umesajiriwa Simba sc, kwa heshima zote, kwanini usifanye bidii ili kulipa fadhira kwa wadau wa Simba na kwa manufaa yako na nchi kwa ujumla.
Kwanini usiwe unafanya mazoezi binafsi ili kuboresha kiwango chako.
Huwa nashangaa sana, Ndemla anapiga mashuti makali sana kwanini hajifunzi kupiga faulo za karibu na goli ?
Kwanini Ndemla hajifunzi kulenga goli.
Ndemla anapata nafasi nyingi tu za kufunga lakini sijui haraka au nini, mengi anapiga nje sawa na Kichuya naye.
Oneni mfano kwa timu ya Mashujaa, mashuti matatu golini yamezaa magoli matatu.
Naona wote mliocheza leo kama mtabahatika tena na kuharibu basi mjue safari yenu imefika mwisho.
Badala ya kujituma ili mnunuliwe nje ya nchi nyie mnafanya juu chini ili mkacheza ligi daraja la kwanza.
Simba leo inajitangaza kimataifa, kipindi kifupi kijacho dunia nzima itaishuhudia Simba ikicheza kimataifa na kuwatangaza wachezaji wake ktk masoko ya kimataifa, ni fulsa nzuri hiyo kujitangaza uwezo wenu.
Nyie mmebaki kuridhika tu na kiwango chenu kibovu, hamtaki kujifunza hata kwa Samata.
Nawaona jinsi mnavyotembea uwanjani kwa kuridhika kuwa mmeshaujua mpira.
Poleni sana vijanawazee
 
I understand. Simba timu kubwa sana. Level yao sio kucheza na Mashujaa. Level yao ni timu kama Al Aly, Esperance, TP Mazembe, Libolo, Asec Mimosa nk.
It was just a minor slip.
😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom