Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) Stand United Vs Simba SC, Dimba la Kambarage

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC), hatua ya 16 bora, kupigwa leo February 25, 2020 ambapo Stand United Chama la Wana, wanawakabili Simba SC, Wekundu wa Msimbazi, kwenye dimba la Kambarage mjini Shinyanga.

Stand United ambao wanaoshiriki michuano ya ligi daraja la kwanza FDL, walitinga hatua ya 16 bora baada ya kuwaondosha Majimaji kwa mikwaju ya penati kwa 5-4 baada ya kumalizika kwa dakika 90 kwa sare ya 1-1 kwenye dimba la Majimaji, Songea.

Simba SC ambayo inashuka dimbani katika mchezo huu wakiwa na morali ya juu kabisa huku wakiwa wametoka kuwasha moto kwenye VPL, imetinga 16 bora baada ya kufanikiwa kuwafurusha Mwadui FC kwa jumla ya mabao 2-1

Kocha wa Stand United, Atuga Manyundo amesema, anawafahamu vilivyo Simba ni timu bora, lakini wamejipanga kupambana kuwaondosha Simba, kwani wachezaji wake amewapa mbinu zote.

Kocha wa Simba, Sven Vanderbroeck amesema, kila mmoja yupo tayari kwa mchezo, lakini kwenya mchezo mmoja hatuwezi kuwatumia wachezaji wote 29 hivyo lazima kuchagua wachezaji wa kuwatumia, na kwa huu mchezo labda kutakuwa na mabadiliko machache.

"Mashabiki wetu wajitokeze kutushangilia, tupo kwenye hali nzuri na tutacheza mchezo mzuri" amesema Vanderbroeck.

Huu ni mtanange wa kukata na soka, nani kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya ASFC? wachezaji kuamua ndani ya dakika 90.

Kumbuka mchezo huu wa Azam Sports Federation kupigwa kuanzia saa 10: 00 jioni..Usikose Ukaambiwa

.......Ghazwat....


Wanaoanza SSC:

Beno Kakolanya, Haruna Shamte, Gadiel Michael, Tairone Santos, Kennedy Juma, Gerson Fraga, Hassan Dilunga, Sharaf Shiboub, Meddie Kagere, Ibrahim Ajibu, Shiza Kichuya.

Akiba:

Salmu, Wawa, Mkude, Chama, Kahata, Kanda, Juma.


 
00' Naaaam kipute kimeanza uwanja wa Kambarage safari ya dakika 90

Patashika ya ASFC kuwania kufuzu robo fainali kati ya Stand United na Simba SC
 
05' mashambulizi ni kwa pande zote huku Simba wakipata kona ambayo haikuzaa bao

Stand United 0-0 Simba SC
 
15' Bado milango ni migumu huku kila timu ikijaribu kutafuta bao bila mafanikio, Simba wakilisakama zaidi lango la Stand
 
25' Mchezaji wa Stand yupo chini baada ya kupata rabsha, free kick kuelekea Simba

Inapigwaaaaaa na mpira unaambaa na kutoka njeee
 
Nahodha wa Simba leo ni Gadiel Michael

38' Kichuya anapiga krosi ambayo inashindwa kumaliziwa vizuri, daah ilikuwa nafasi tamu kuandika bao
 
Anapigaaa njeee, mchezaji mmoja wa Stand United alimjaribu Beno kwa mbali, lakini shuti lake limepaa juu ya lango.

Stand Utd 0-0 Simba SC
 
45+3'

Kuelekea kuwa mapumziko kwenye michuano hii ya ASFC

Shamte anapiga krosi, anatokea golikipa na kuunyaka mpira ule

Naaaaaaam mpira ni mapumziko ambapo timu zote zinatoka bila kufungana katika dakika 45 za mwanzo

ASFC, HT: Stand United 0-0 Simba SC
 
Yah, game ni ngumu, timu zinacheza kwa tahadhari

Upande wa Simba wanacheza vizuri ingawa hakuna bao lakini wachezaji wanapambana, wanapanga mashambulizi kama ile nafasi ya Shiboub almanusura Simba iandike bao kwa mpira wake kugonga mwamba
Vip Simba inacheza vizuri au?
 
Penatiiiiiiii kuelekea Stand United baada mchezaji kuunawa mpira eneo la 18.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…