Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) Stand United Vs Simba SC, Dimba la Kambarage

Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) Stand United Vs Simba SC, Dimba la Kambarage

Nahisi mnaombea Simba atoke ili mjihakikishie nafasi ya kombe la shirikisho.

Leo Gwambina lazima awachezeshe mbina (ngoma)
Yanga kwa Gwambina ni Sawa na Fisi kukabidhiwa Bucha, kesho Kwasukwasu watachezeshwa Nyimbo zote za GAMBOSH
 
80' Free Kick kuelekea Stand Utd, anakwenda kupiga Chamaaaaa, Kona

Kona mbili zimepigwa bila kuzaa bao

Stand United 1-1 Simba SC
 
87' Maulid kwake Abdy Mwete Stand wanapanga mipango kuona namna gani Watapenya ngome ya Simba
 
Cha ajabu leo nyie ndio mumekimbia uzi. 😅😅😅😅😅😅

Ushindi upo jamaani.
Sio kweli tupo mkuu ...mbona tunashinda hii game!
Ila natanguliza hongera kwa Stand ,wamejitahidi mziki wa Simba SI wa kitoto!
 
Anakwenda Kwake Kagere eneo la hatari, nafasi kwa Simba anapigaaa lakini golikipa anadaka

Stand United 1-1 Simba SC
 
Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC), hatua ya 16 bora, kupigwa leo February 25, 2020 ambapo Stand United Chama la Wana, wanawakabili Simba SC, Wekundu wa Msimbazi, kwenye dimba la Kambarage mjini Shinyanga.

Stand United ambao wanaoshiriki michuano ya ligi daraja la kwanza FDL, walitinga hatua ya 16 bora baada ya kuwaondosha Majimaji kwa mikwaju ya penati kwa 5-4 baada ya kumalizika kwa dakika 90 kwa sare ya 1-1 kwenye dimba la Majimaji, Songea.

Simba SC ambayo inashuka dimbani katika mchezo huu wakiwa na morali ya juu kabisa huku wakiwa wametoka kuwasha moto kwenye VPL, imetinga 16 bora baada ya kufanikiwa kuwafurusha Mwadui FC kwa jumla ya mabao 2-1

Kocha wa Stand United, Atuga Manyundo amesema, anawafahamu vilivyo Simba ni timu bora, lakini wamejipanga kupambana kuwaondosha Simba, kwani wachezaji wake amewapa mbinu zote.

Kocha wa Simba, Sven Vanderbroeck amesema, kila mmoja yupo tayari kwa mchezo, lakini kwenya mchezo mmoja hatuwezi kuwatumia wachezaji wote 29 hivyo lazima kuchagua wachezaji wa kuwatumia, na kwa huu mchezo labda kutakuwa na mabadiliko machache.

"Mashabiki wetu wajitokeze kutushangilia, tupo kwenye hali nzuri na tutacheza mchezo mzuri" amesema Vanderbroeck.

Huu ni mtanange wa kukata na soka, nani kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya ASFC? wachezaji kuamua ndani ya dakika 90.

Kumbuka mchezo huu wa Azam Sports Federation kupigwa kuanzia saa 10: 00 jioni..Usikose Ukaambiwa

.......Ghazwat....

Wanaoanza SSC:

Beno Kakolanya, Haruna Shamte, Gadiel Michael, Tairone Santos, Kennedy Juma, Gerson Fraga, Hassan Dilunga, Sharaf Shiboub, Meddie Kagere, Ibrahim Ajibu, Shiza Kichuya.

Akiba:

Salmu, Wawa, Mkude, Chama, Kahata, Kanda, Juma.


View attachment 1368862View attachment 1368863
Simba tunashinda hii mechi tulieni, kama unakunywa soda kunywa kabisa, kama unakunywa bia kunywa tuu wanasimba wenzangu hii mechi tunashinda
 
Hawa lazima watoke, hata kwa mikwaju ya penelti

Simba Nguvu Moja
 
90+6'

Kuelekea kukamilika kwa mchezo huu wa ASFC

Anakwenda kwake Kanda, Chama anapigaaa, lakini golikipa anaruka juu nakudaka

Kuna mchezaji wa Stand, yupo chini

Kona kuelekea Stand, inapigwaaaa Simba wanachelewa mpira unatoka nje

Wanakwenda tena Simba, Deo Kandaa kwake Gadiel, unarudishwa nyuma, unapelekwa tena mbelee kwa Ajibuuu, wanapoteza Simba..

Naaaam mpita umekwishaa kwa kukamilika dakika 90 kwa sare ya moja kwa moja.

ASFC, FT: Stand United 1-1 Simba SC
 
Back
Top Bottom