Komredi Kawaida yuko sahihi, Viongozi wa dini wamefeli

Komredi Kawaida yuko sahihi, Viongozi wa dini wamefeli

Mkuu
Labda nikusaidie Kidogo kukufumbua akili Macho na Kutoa Ujinga.

Ukristo Sio Dini.
Ukristo ni Imani thabiti ya Kumfuata na Kumuamini Yesu Kristo, kwa Kutenda Mema sawa sawa na Yesu alivyokuwa mwema au sawa sawa na Mafundisho yake.

Ukristo Sio Jina kama Pascal, Christopher
Lameck, Edward, Julius, Sarah, Christina victoria nk

Matendo ya Kikristo yesu au Mafundisho ya yake yalikuwa ni kutenda wema.
Mfano
43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
Mathayo
lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
Mathayo 5:44.

USICHANGANYE MASHETANI WENYE DHAMBI, WAPAGANI, VUGUVUGU NA IMANI YA WAKRISTO.TENA ALISEMA UKIWA VUGUVUGU ATAKUTAPIKA
 
Yaani kuua napo unataka mpaka padre akuambie usiue wewe akili huna?
 
Hoja ya Komredi Kawaida kuhusu wajibu wa viongozi wa dini katika maadili ya waumini inastahili mjadala wa kina. Si kwa sababu viongozi wa dini wanapaswa kubeba makosa yote ya wanasiasa, bali kwa sababu malezi ya kiroho na kimaadili ni sehemu ya dhamana yao.

Katika maadhimisho ya kuwaombea waliofariki kutokana na matukio ya Oktoba 29, 2025, Kanisa Katoliki Tanzania limetoa nafasi ya tafakari kuhusu toba, ukweli, msamaha na uponyaji wa taifa. Rais wa TEC, Askofu Wolfgang Pisa, amesisitiza umuhimu wa kutafakari hata makosa ya kutotenda, kutosema na kutotoa mwongozo wakati wengine walipokuwa hatarini.

Hapo ndipo hoja ya Komredi Kawaida inapopata uzito: viongozi wa dini wanapowalaumu waumini wao kwa kushindwa kuishi kwa maadili, je, wao wenyewe wanajitathmini kwa kiwango gani kuhusu dhamana yao ya kuwajenga waumini hao?

Ni rahisi kusimama madhabahuni na kukemea rushwa, dhuluma, chuki, matumizi mabaya ya madaraka na ukosefu wa utu. Lakini watu wanaotenda makosa hayo wamekuwa chini ya malezi gani ya kiroho? Wamefundishwa nini kuhusu haki, utu wa binadamu na thamani ya uhai?

Haiwezekani viongozi wa dini wakajipa jukumu la kufundisha maadili, lakini wanapoyaona maadili hayo yakipuuzwa na waumini wao, wajione kama hawana sehemu yoyote ya kujitathmini.
Kanisa Katoliki lenyewe, kupitia tamko la TEC la Novemba 15, 2025, lilisisitiza ukweli, haki, uwajibikaji na uchunguzi huru kuhusu mauaji yaliyotokea. Hayo ni mambo muhimu. Lakini mjadala haupaswi kuishia kwenye kuwakosoa waliotenda makosa. Unapaswa pia kuangalia namna taasisi za dini zinavyotekeleza jukumu lake la kujenga dhamiri za waumini.

Mwanasiasa anayeshindwa kutenda haki anawajibika kwa kushindwa kwake. Lakini kiongozi wa dini anayemlea mwanasiasa huyo hawezi kukwepa wajibu wa kutafakari ubora wa malezi aliyompa.
Hatutaki viongozi wa dini waendeshe serikali, wala hatutaki dini ziwe vyombo vya siasa. Tunataka viongozi wa dini watambue kwamba mahubiri yao yanapaswa kuzaa matunda katika maisha halisi, ikiwemo kwenye ofisi za umma na vyombo vya maamuzi.

Kwa hiyo, hoja ya Komredi Kawaida inapaswa kuchukuliwa kama mwaliko wa kujitathmini, si kama shambulio dhidi ya taasisi za dini.

Kabla ya viongozi wa dini kuuliza kwa nini wanasiasa hawafuati mafundisho yao, wajiulize pia wamefanya nini kuhakikisha mafundisho hayo yanajenga dhamiri za watu wanaowaongoza.

Kwa sababu mwisho wa siku, mafanikio ya malezi ya kiroho hayawezi kupimwa kwa idadi ya waumini wanaohudhuria ibada pekee, bali pia kwa namna wanavyoishi, wanavyotenda na wanavyowatendea wengine wanapopewa dhamana ya uongozi.

Kawaida yuko sahihi, kufeli kwa wanasiasa ni kufeli kwa viongozi wa dini. Asikilizwe.View attachment 3701736
Uvivu wa kusoma na kujua historia ya dini na Siasa kwa huyu bwana Mdogo.Kazi ya dini sio kupeleka watu mbinguni kwa sababu mbinguni unaenda kwa kukata pumzi na hakuna nauli.Dini kazi yake kuu ni kuona watu wanaishi kwa upendo,wanaishi maisha mema,wanatendeana haki na maisha ya Amani.Tokea enzi na enzi viongozi wa Dini kama sio watawala huwa ni sauti ya watu dhidi ya watawala.Kwa Kawaida mimi simlaumu kwa kuwa bado anasafari ndefu ya kujifunza maisha hata kama anaweza kupata vyeo bila kujua mambo ndio mfumo wetu wa siasa unaoacomodate watu ambao hawana legacy nyingine.
 
Back
Top Bottom