MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Wasalaam,
Nimetokea ghafla kumkumbuka sana huyu komredi wangu wa ukweli mzee wa "Piga Tuu"
Huyu ndugu yangu baada tu ya kuisha kwa uchaguzi na awamu hii ya tano kuingia madarakani tumekuwa hatumsikii kabisa.
Mawaziri wakuu wastaafu wengine kama Mzee Malecela, Mzee Warioba, Mzee Msuya na Mzee Sumaye walikuwa wanaunguruma hata baada ya vipindi vyao kuisha. Lakini komredi Mizengo Pinda amekuwa adimu sana kwenye masikio na macho yetu, ni kama yupo lakini hayupo.
Binafsi nimekukumbuka sana komredi wangu mzee wa "hisia kali" na maamuzi mazito lakini yenye busara ya aina yake.
Popote pale ulipo komredi, Malcom Lumumba anakusalimu sana sana. Angepata nauli na wasaa wa kufahamu ulipo kwasasa angefunga hata safari kuja kukusalimia.
NB: Pia hizi salamu zimfikie ndugu yetu Former Minister Plenipotentiary Mheshimiwa sana Bwana Benard Kamilius Membe ambaye naye sijamtia machoni kwa muda mrefu sana.