Kondoa: Afisa Manunuzi amlalamikia Mkurugenzi kwa kutukana watumishi, asema ubabe wake umezidi

Kondoa: Afisa Manunuzi amlalamikia Mkurugenzi kwa kutukana watumishi, asema ubabe wake umezidi

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Afisa Manunuzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Mussa Kimwaga amemlalamikia Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa kutukana na kuwa mbabe kwa watumishi.


Bw. Kimwaga akitema cheche

Tuna ubunifu mwingi sana na ushauri mwingi lakini hatupewi nafasi ya kutoa ushauri mzuri. Ubabe ni mkubwa sana kwa Mkurugenzi wetu.

Binafsi hata mimi natamani niondoke Kondoa; nashindwa tu sina mtu wa kunihamisha. Ulikuwa unamtamka hapa Muweka Hazina, Muweka Hazina amekimbia – ameondoka Kondoa si kwa mapenzi ni kwasababu ya kusemwa vibaya na Mkurugenzi.

Sawa, mtumishi kuna kukosea lakini pia kuna namna ya kumuonya mtumishi, lakini unatukanwa matusi ya nguoni. Binafsi nimetukanwa kwenye site. Unafanya kazi wakati mwingine tunatumia resources zetu za mshahara tunajua Halmashauri yetu ya Kondoa wakati mwingine mambo ni magumu. Unatoa hela yako binafsi unafanya kazi lakini no appreciation kwa Mkurugenzi. Inafika mahali inavunja moyo!

Binafsi, Mkuu wa Mkoa mimi natamani niondoke hata kesho kwenye hii Halmashauri. Mimi nimechoka!

Sijaanzia hapa kufanya kazi; nimefanya kazi Muheza (miaka minne), Handeni (miaka minne) Shinyanga Manispaa… Nimefanya kazi sina rekodi ya ubadhirifu, sijawahi kupelekwa Takukuru, lakini kwa Kondoa nimekata tamaa. Na Mkurugenzi naye hanitaki! Amesema “Wewe sikutaki!” Hata kwenye hii miradi inayoendelea amesema “Wewe sikutumii!” Ubabe umezidi!


Hawaongei hao. Wanakaa kimya Wakuu wa Idara lakini wanaugua …
 
Halafu majungu yalizaliwa Kondoa, yakasomea Kondoa na ndio makazi yake makuu. Huku Mbeya na kwingineko yanakuja Mara moja moja sana
 
Hapo hakuna team work,ni team majungu !! Kati yao mmoja atakuwa ni mzalendo na mwingine ni ant -uzalendo. Ila wamesahau tulikubaliana kila mmoja ale kwa kamba yake, kwa kuzingatia urefu wa kamba yake. Kuna mmoja anataka awe anavimbiwa hapo bila shaka!!
 
Back
Top Bottom