The hitman
JF-Expert Member
- Nov 30, 2017
- 3,673
- 2,288
Mke wa ndugai , Dr fatma ameteuliwa kuwa Ras(Somebody) Ndugai...ni mke wa Ndugai
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mke wa ndugai , Dr fatma ameteuliwa kuwa Ras(Somebody) Ndugai...ni mke wa Ndugai
Ahahah kumbe unamjua vizuri nimesoma nae Chuo uyo Bro.Sorry kwake kama namkosea. Huyu ndugu ni mjeda, hababaiki
Alisoma Songea Boys huyu mwamba,kavurugwa hatari
Nilikuwa naye Muheza ni mtu poa sanaAhahah kumbe unamjua vizuri nimesoma nae Chuo uyo Bro.
Mbombo ngafuHata Mimi sielewe kwa Idara ya TISS na Takukuru mpaka leo wameacha wajibu wao kwa viongozi kama Mkurugenzi huyo ambaye taarifa ziko wazi hata mitaani ?!
DED ni kada wa CCM hakuna namnaAfisa Manunuzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Mussa Kimwaga amemlalamikia Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa kutukana na kuwa mbabe kwa watumishi.
View attachment 2129745
Bw. Kimwaga akitema cheche
Tuna ubunifu mwingi sana na ushauri mwingi lakini hatupewi nafasi ya kutoa ushauri mzuri. Ubabe ni mkubwa sana kwa Mkurugenzi wetu.
Binafsi hata mimi natamani niondoke Kondoa; nashindwa tu sina mtu wa kunihamisha. Ulikuwa unamtamka hapa Muweka Hazina, Muweka Hazina amekimbia – ameondoka Kondoa si kwa mapenzi ni kwasababu ya kusemwa vibaya na Mkurugenzi.
Sawa, mtumishi kuna kukosea lakini pia kuna namna ya kumuonya mtumishi, lakini unatukanwa matusi ya nguoni. Binafsi nimetukanwa kwenye site. Unafanya kazi wakati mwingine tunatumia resources zetu za mshahara tunajua Halmashauri yetu ya Kondoa wakati mwingine mambo ni magumu. Unatoa hela yako binafsi unafanya kazi lakini no appreciation kwa Mkurugenzi. Inafika mahali inavunja moyo!
Binafsi, Mkuu wa Mkoa mimi natamani niondoke hata kesho kwenye hii Halmashauri. Mimi nimechoka!
Sijaanzia hapa kufanya kazi; nimefanya kazi Muheza (miaka minne), Handeni (miaka minne) Shinyanga Manispaa… Nimefanya kazi sina rekodi ya ubadhirifu, sijawahi kupelekwa Takukuru, lakini kwa Kondoa nimekata tamaa. Na Mkurugenzi naye hanitaki! Amesema “Wewe sikutaki!” Hata kwenye hii miradi inayoendelea amesema “Wewe sikutumii!” Ubabe umezidi!
Hawaongei hao. Wanakaa kimya Wakuu wa Idara lakini wanaugua …
Atatafutiwa makosa ya kubumbaHapo kasema dukuduku lake mbele ya boss (mkuu wa mkoa) hawana la kumfanya maana serikali itamlinda
Shida ya kuteua makada kuwa ma-DEDNoma sana !