Kondoa: Afisa Manunuzi amlalamikia Mkurugenzi kwa kutukana watumishi, asema ubabe wake umezidi

Kondoa: Afisa Manunuzi amlalamikia Mkurugenzi kwa kutukana watumishi, asema ubabe wake umezidi

Hata Mimi sielewe kwa Idara ya TISS na Takukuru mpaka leo wameacha wajibu wao kwa viongozi kama Mkurugenzi huyo ambaye taarifa ziko wazi hata mitaani ?!
 
Bei ya petrol laziama ipande kwa hii vita inayoendelea ya urusi vs ukraine
 
Mimi boss anitukane kazini mbona kesho yake magazeti yote nchini yataandika habari zangu.
 
Afisa Manunuzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Mussa Kimwaga amemlalamikia Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa kutukana na kuwa mbabe kwa watumishi.

View attachment 2129745
Bw. Kimwaga akitema cheche

Tuna ubunifu mwingi sana na ushauri mwingi lakini hatupewi nafasi ya kutoa ushauri mzuri. Ubabe ni mkubwa sana kwa Mkurugenzi wetu.

Binafsi hata mimi natamani niondoke Kondoa; nashindwa tu sina mtu wa kunihamisha. Ulikuwa unamtamka hapa Muweka Hazina, Muweka Hazina amekimbia – ameondoka Kondoa si kwa mapenzi ni kwasababu ya kusemwa vibaya na Mkurugenzi.

Sawa, mtumishi kuna kukosea lakini pia kuna namna ya kumuonya mtumishi, lakini unatukanwa matusi ya nguoni. Binafsi nimetukanwa kwenye site. Unafanya kazi wakati mwingine tunatumia resources zetu za mshahara tunajua Halmashauri yetu ya Kondoa wakati mwingine mambo ni magumu. Unatoa hela yako binafsi unafanya kazi lakini no appreciation kwa Mkurugenzi. Inafika mahali inavunja moyo!

Binafsi, Mkuu wa Mkoa mimi natamani niondoke hata kesho kwenye hii Halmashauri. Mimi nimechoka!

Sijaanzia hapa kufanya kazi; nimefanya kazi Muheza (miaka minne), Handeni (miaka minne) Shinyanga Manispaa… Nimefanya kazi sina rekodi ya ubadhirifu, sijawahi kupelekwa Takukuru, lakini kwa Kondoa nimekata tamaa. Na Mkurugenzi naye hanitaki! Amesema “Wewe sikutaki!” Hata kwenye hii miradi inayoendelea amesema “Wewe sikutumii!” Ubabe umezidi!


Hawaongei hao. Wanakaa kimya Wakuu wa Idara lakini wanaugua …
DED ni kada wa CCM hakuna namna
 
Back
Top Bottom