Kongamano la Katiba Mpya - Nkurumah Hall Jan 15, 20011

Kongamano la Katiba Mpya - Nkurumah Hall Jan 15, 20011

Masanilo

Platinum Member
Joined
Oct 2, 2007
Posts
22,286
Reaction score
4,523

Attachments

Angalieni uwezekeno mkaalika watu kama akina Lipumba, Dr.Slaa, Mchungaji Mtikila, Makamba wanasiasa wengi tusikie nao mawazo yao
 
Muda haotoshi nadhani kungewekwa vipindi kila week kwa mwezi mzima wa january
 
Angalieni uwezekeno mkaalika watu kama akina Lipumba, Dr.Slaa, Mchungaji Mtikila, Makamba wanasiasa wengi tusikie nao mawazo yao

Cha muhimu ni watu kujitokeza kwa wingi na kuchangia kwa hoja!
 
Muda haotoshi nadhani kungewekwa vipindi kila week kwa mwezi mzima wa january

Umenena. Nkurumah uwe mwanzo tu. Kimsingi kinachotakiwa ni katiba kusomwa yote hadharani ukurasa baada ya ukurasa kila siku kupitia radio na televisheni. Magazeti nayo yasibaki nyuma katika kuichapisha katiba yote katika magazeti yao.
 
Nina mpango wa kujiwekea japo saa moja kwa siku kuisoma Katiba ya sasa ya nchi yetu. Kwa kweli Watanzania wengi hatujaisoma kabisa Katiba ya sasa na inakuwa vigumu hata kujadili mapungufu yake!

Pia tuwaelimishe na Watanzania wenzetu wenye uelewa mdogo kuhusu umuhimu wa Katiba ya Nchi. Waelewe ya kwamba hiyo ndiyo sheria mama inayowalinda kila uchao bila ya wao kujua. Kwa hiyo kuijua ni vema zaidi na itawasaidia zaidi. Pia elimu itolewa kwa Watanzania kwa njia mbali mbali kuhakikisha watu wanaelewa kwanini tunataka Katiba Mpya!
 
Ni muhimu kuhusisha wanaharakati mbalilmbali walio mstari wa mbele katika kupigania Katiba Mpya, nawakusudia Mch Mtikila, njelu Kasaka na kundi la G55 enzi zile, Kituo cha Sheria na haki za binadamu, wanafunzi wasomi, n.k.
Binafsi napendelea mjadala uwe wa wazi tena kama ikiwezekana uwe live kupitia Tv ya Umma (TBC) au StarTV ili kuwafikia wananchi wengi.
 
Binafsi napitia kipengele kwa kipengele kwa katiba yetu pamoja na marekebisho yote! Ni aibu raisi yuko juu ya kila kitu
 
Binafsi napitia kipengere kwa kipengere kwa katiba yetu pamoja na marekebisho yote! Ni aibu raisi yuko juu ya kila kitu

Kipengere ni jina la milima huko kusini mwa Tanzania.

Vilivyomo kwenye Katiba ni vepengele.

Tukutane, pamoja na wanaJF wote (wenye mapenzi mema na nchi ya Tanzania kwa VITENDO sio maneno mengi) hapo Nkrumah siku na muda tajwa. Ni muda wa kuacha kuandikia mate.
 
Siku hiyo Nkrumah nahisi patakuwa hapatoshi!
 
Binafsi napitia kipengele kwa kipengele kwa katiba yetu pamoja na marekebisho yote! Ni aibu raisi yuko juu ya kila kitu

Kipengere ni jina la milima huko kusini mwa Tanzania.

Vilivyomo kwenye Katiba ni vepengele.

Sasa Mkuu Uwiano yaani unarekebisha halafu unaboronga tena. Sio Vepengele ni Vipengele.

Back to the topic, mchungaji ahsante kwa taarifa na tunaamini utakuwa ni mwanzo mzuri na hatimaye kelele za chura zitamwamsha mwenye nyumba, ama atufukuze au akaushe maji vyura tuhamie kwenye maji
 
UFISADI wa CCM, kikwete, Rostam Aziz na Edward Lowassa is to blame kwa DAMU ILIOMWAGIKA ARUSHA, period!!!!!!!! Na sasa ndio mwendo mnyato tena mpaka kunakucha!!

'Vita' vya katiba mpya ndio tayari vimeshahamishiwa uwanja na DAMU YA THAMANI KUBWA YA WATANZANIA ambayo CCM imemwaga leo Arusha, harufu yake itasambaa nchi nzima tena kwa kasi ajabu ambayo haijawahi kuonekana!!

Ni damu yao hayo ndio yatakayowaondoa MAFISADI Ikulu na kutuletea KATIBA MPYA ilioandikwa na wananchi wenyewe na wala si wakurugenzi wa MEREMETA kama Mzee Mzindakaya!
 
Kipengere ni jina la milima huko kusini mwa Tanzania.

Vilivyomo kwenye Katiba ni vepengele.

Tukutane, pamoja na wanaJF wote (wenye mapenzi mema na nchi ya Tanzania kwa VITENDO sio maneno mengi) hapo Nkrumah siku na muda tajwa. Ni muda wa kuacha kuandikia mate.

Haya Mkuu wa vepengele nitajitahidi niwepo.
 
Msingi wa Katiba mkuu ni mkutano wa kikatiba utakaochaguliwa na wapigakura kulingana na majimbo ya uchaguzi yaliyopo. Hili linamaanisha ya kuwa mchakato mzima lazima uwe umetungiwa sheria na Bunge siyo ufanyike kwa ridhaa na matakwa ya kikundi kidogo cha watu wachache kikiongozwa na JK.........................Huo utakuwa ni uchakachuaji babu "K"..........................utazidi hata ule wa uchaguzi..........................
 
UDSM kujadili jinsi ya kuiunda katiba
Wednesday, 05 January 2011 20:53

Leon Bahati na Rymond Kaminyonge

WATAALAMU wa fani mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wameamua kujitosa katika vuguvugu la kupigania katiba mpya nchini na wamepanga kukutana ili kuweka bayana namna Watanzania wanavyotakiwa kuiunda.

Hatua ya wasomi hao imekuja wakati ambapo Rais Jakaya Kikwete amekubali mkakati wa kuandikwa kwa katiba na kuahidi kuunda tume itakayoongozwa na mwanasheria aliyebobea ili kuongoza mchakato wa kuelekea kuiunda kwa umakini.

Kwa mujibu wa taarifa kwa gazeti hili iliyotolewa na Jumuia ya Wanataaluma wa UDSM (Udasa) ,wasomi hao watatimiza azma hiyo kwa kuendesha mjadala katikati ya mwezi huu.

Miongoni mwa wanataaluma, nguli wa kisiasa, watakaoongoza mjadala huo ni Profesa Issa Shivji, ambaye ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Taaluama cha Mwalimu Nyerere na Jenerali Ulimwengu, Mwandishi wa Habari Mashuhuri nchini.

Udasa imeeleza kwamba mhadhara huo ambao utafanyika katika ukumbi wa Nkrumah, UDSM, mbali na kuwahusisha wanataaluma hao, pia watakaribishwa watu mbalimbali wakiwepo wanasiasa, wanaharakati pamoja na wananchi, wakereketwa wa katiba.

Vuguvugu la kutaka iandikwe katiba mpya lilitia kasi nchini mara baada ya kumalizika uchaguzi mkuu, Oktoba mwaka jana, likiongozwa na vyama vya siasa vya upinzani.

Udasa imesema kwamba mjadala huo wanatarajia kuufanya katikati ya mwezi huu.

Wakati huo huo, Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), limempongeza Rais Jakaya Kikwete, kwa uamuzi wake wa kuruhusu mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya.

Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Shaaban Simba, alisema jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba katiba ijayo ijumuishe makundi yote ya kijamii na kwamba waislam pia watachangia waliyonayo mengi katika katiba hiyo mpya.
" Waislam wanayo mengi ya kupendekeza katika mchakato mpya wa katiba mpya kama zilivyo jamii nyingine za Watanzania," alisema.
Katika hatua nyingine Jumuiya ya Tawala za Mitaa (Alat), imesema Katiba mpya ikipatikana, itatoa fursa katika kujenga mfumo bora wa serikali za mitaa utakaokidhi ndoto za Watanzania katika kupeleka madaraka kwa wananchi.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa Alat, Habrahamu Shamumoyo kwenye mkutano wa jumuiya hiyo wa kupanga mikakati ya kuukaribisha mwaka mpya 2001.

Alisema Jumuiya hiyo inayoziunganisha halmashauri na mamlaka za miji na wilaya,inaangalia namna inavyoweza kushiriki kikamilifu kwenye mchakato wa kutunga katiba mpya.
 
Siku hiyo Nkrumah nahisi patakuwa hapatoshi!

Ingewezekana hilo kongamano lifanyikie uwanja wa Jangwani --yaani iwe ni kama mkutano wa hadhara vile maana ni kweli nkurumah haitatosha.
 
Kipengele cha GPA kwenye degree ya kwanza ni muhimu kiwekwe kama moja ya sifa ya mgombea raisi. Kikwete ana GPA ya 1.9 no wonder anaipeleka anavyojua yeye. Kuepuka watu kama hawa GPA ni muhimu walau ianzie 3.0 kwa wagombea uraisi
 
Back
Top Bottom