Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Kongamano hilo lenye kauli mbiu ya “Kulinda Utaratibu wa Kimataifa na Kukuza Maendeleo ya Amani kwa pamoja,” limefanyika wakati dunia inapoadhimisha miaka 80 tangu kupatikana kwa ushindi wa Vita ya Kupambana na Ufashisti, na miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, na lina umuhimu mkubwa. Zaidi ya wajumbe 1,800, wakiwemo wawakilishi wa serikali, wataalamu, wasomi, na waangalizi kutoka zaidi ya nchi 100, na mashirika ya kimataifa na kikanda, wamekukutana ili kujadili amani na usalama na kutafuta suluhisho la kudumu la utatuzi wa migogoro.
Hivi leo dunia iko kwenye njiapanda tena. Migogoro inatokea mara kwa mara, na vitendo vya upande mmoja vinaongezeka. Jamii ya kimataifa ina wasiwasi wa pamoja: ni vipi dunia inaweza kukabiliana na changamoto hizo? Kongamano la Xiangshan limetoa jibu la wazi, ni kwa ushirikiano wa pande nyingi tu, na ujenzi wa utaratibu wa usalama wa pamoja, ndipo binadamu wanaweza kushughulikia kwa ufanisi changamoto hizo.
Katika hotuba yake kwenye ufunguzi wa kongamano hilo, Waziri wa Ulinzi wa China Dong Jun amesisitiza kwamba, ushirikiano ni chaguo bora zaidi, na inapaswa kubadilisha migogoro kuwa ustawi wa pamoja, na kugeuza upinzani dhidi ya utandawazi kuwa mshikamano wa kimataifa.
Kinyume na baadhi ya nchi za Magharibi ambazo zinatanguliza usalama wao, na kutumia vibaya vikwazo vya upande mmoja, China inashikilia ushirikiano wa kimataifa unaoegemea pande nyingi, na kutetea utatuzi wa mizozo kwa njia ya mazungumzo badala ya makabiliano. China si kama tu ni mtetezi wa utaratibu wa kimataifa, bali pia ni mtoaji wa bidhaa za umma za kimataifa. Kutoka Pendekezo la Usalama wa Kimataifa, hadi Pendekezo la Usimamizi wa Mambo ya Kimataifa, China inachukua hatua madhubuti ili kuhimiza ushirikiano wenye usawa, jumuishi na unaofaa zaidi duniani. Kama Rais Xi Jinping wa China alivyosema, hatma ya binadamu ina uhusiano wa karibu,na ni kwa kuchukuliana kama watu sawa, kuishi kwa maelewano na kusaidiana, ndipo binadamu wanaweza kutokomeza vita.
Upana na uwakilishi wa kongamano hilo pia umetoa ishara thabiti: wajumbe kutoka nchi zilizoendelea, nchi zinazoibuka kiuchumi, nchi ndogo na za kati, na hata nchi zinazopambana zimekusanyika pamoja, kwa majadiliano ya wazi juu ya mada muhimu zikiwemo “Njia Sahihi ya Nchi Kubwa Kuishi Pamoja”, “Usimamizi wa Teknolojia ya Akili Bandia”, na “Ushirikiano wa Usalama wa Asia na Pasifiki”.
Hata katika masuala nyeti, pande zote zimekuwa wazi na kutafuta mwafaka. Huu ni moyo wa Kongamano la Xiangshan. Umevuka mipaka ya nchi na mawazo, na kulifanya kongamano hilo liwe jukwaa kweli la mawasiliano.