Kongani za viwanda, zawa hatua muhimu kwenye kuhimiza ushirikiano kati ya China na Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
​

Moja kati ya misemo ya China inayofahamika sana duniani ni kuwa, njia nzuri zaidi ya kumsaidia mtu mwenye njaa, ni kumfundisha namna ya kuvua samaki, kwani njia hiyo ni endelevu zaidi kuliko kumpatia mtu samaki. Uzuri wa China ni kuwa kauli zake huwa zinafuatana na vitendo, na hiki ndicho kinachoonekana zaidi kwa sasa kwenye ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika.

Katika miaka ya hivi karibuni, hasa baada ya mkutano wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika Septemba 2024, China na nchi za Afrika zimehimiza ushirikiano katika biashara ya mazao ya kilimo, na kufuta ushuru kwa bidhaa zote za kilimo zinazoingia kwenye soko la China, na pia kuhimiza maendeleo ya ujenzi wa kongani za viwanda.

China imekuwa inasema njia nzuri zaidi ya kutoa msaada, ni ile ya kunufaishana, yaani “win-win cooperation”. Katika muktadha huu, China imekuwa ikisaidia kwa kuwekeza kwenye kongani za viwanda, ambazo mbali na kunufaisha wawekezaji, wenyeji wanapata nafasi za ajira, serikali zinapata mapato ya kodi, na nchi zinazopokea uwekezaji huo zinaongeza uzalishaji wa bidhaa na hata uuzaji nje wa bidhaa.

Hivi karibuni nchini Tanzania serikali ilisema uwekezaji uliofanywa na Sino-Tan kwenye Kongani ya Viwanda ya Kwala, iliyopo wilayani Kibaha mkoani Pwani, ulifanikisha ujenzi wa viwanda 200 vitakavyogharimu zaidi ya shilingi trilioni 8. Uwekezaji huo umeleta ajira zaidi ya 100,000 kwa watanzania, na kuleta mapato zaidi ya shilingi trilioni 1.3 kwa mwaka.

Mbali na kuongeza mapato, nafasi za ajira na kuingiza teknolojia mpya, kongani hiyo pia imekuwa ni kichocheo cha kuvutia uwekezaji zaidi. Kwa sasa mamia ya wawekezaji na wafanyabiashara kutoka China, wamekuwa wakitembelea eneo hilo, ambalo wanaona lina mazingira mazuri ya kuweka vitega uchumi vyao.

Hata hivyo utayari wa wawekezaji wa China kwenye nchi nyingi za Afrika bado unakabiliwa na changamoto kadhaa. Ni ukweli usiofichika kuwa hali ya miundombinu, iwe ni ile ya barabara, mawasiliano ya habari, na hata umeme na maji, bado ina udhaifu. Ingawa baadhi ya wataalam wa uchumi wanasema changamoto hiyo yenyewe pia ni fursa ya uwekezaji, lakini ukweli ni kuwa ni uwekezaji ambao unahitaji muda mrefu sana kwa mwekezaji kupata faida. Hili ni eneo ambalo serikali linatakiwa kuwekeza pesa nyingi ili kuvutia wafanyabiashara wawekezaji.

Serikali za nchi mbalimbali za Afrika zimechukua hatua za ziada ili kuhakikisha kuwa udhaifu wa miundombinu hauwi kikwazo kwenye uwekezaji. Kenya, Ghana, na Ethiopia kwa mfano zimeanzisha vikosi kazi vya wizara mbalimbali vilivyojitolea kusimamia miradi ya miundombinu inayofadhiliwa na China. Vikosi kazi hivyo hufuatilia maendeleo ya mradi ya miundo mbinu, na kuhakikisha kuwa miundombinu bora inakuwa kichocheo cha kuvutia uwekezaji.

Ni wazi kuwa kongani za viwanda ni ongezeko la muhimu kwenye ushirikiano kati ya China na Afrika, na mtindo huu wa uwekezaji umekuwa na matokeo ya kunufaisha pande mbili. Kama kasi ya kuboresha miundombinu barani Afrika itaendelea kuongezeka, kutakuwa na kongani nyingi zaidi na kunufaisha watu wengi zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…