Kongo na M23 walaumiana baada ya mazungumzo ya amani kukwama

subiri uone

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2024
Posts
753
Reaction score
624

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha D.W:​

Mazungumzo kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa AFC/M23 yameahirishwa kwa muda usiojulikana. Mazungumzo haya yalitarajiwa kurejea leo mjini Doha, Qatar.

Kombobild Felix Tshisekedi und Corneille Nangaa
Picha: Vlad Vanderkelen/Belga/picture alliance/Tony Karumba/AFP
Matangazo

Katika tamko hilo la kanuni zilizotiwa saini tarehe 19 Julai katika mji mkuu wa Qatar, pande hizo mbili ziliazimia kuanza mazungumzo ya amani ifikapo Agosti 8. Hata hivyo, hadi jana, hapakuwa na dalili ya kuanza kwa ufanisi wa mazungumzo hayo Ijumaa (08.08.2025). Alhamisi, AFC/M23 ilikuwa imetangaza tayari kwamba wajumbe wake walikuwa hawajaenda Doha.

Ujumbe wa serikali ya Kongo ulikuwa ungali bado mjini Kinshasa hadi asubui yaleo. Kwa upande wa AFC/M23, msimamo unaonekana kuwa mkali zaidi: wawakilishi wao walifika Alhamisi mjini Bukavu.

Ujumbe wa AFC/M23 umedai kwamba utarejea kwenye mazungumzo huko Doha ikiwa wafungwa wao waliozuiliwa na serikali ya Kongo wataachiliwa. Lakini serikali ya Kongo inaamini kwamba bado haujafika wakati wa kuwaachilia wafungwa hao, na kwamba hatua hii ni suala la mazungumzo yanayotarajiwa kufanyika moja kwa moja.

Wakati huo huo, takriban watu wanne wamepoteza maisha katika mapigano makali yaliyoripotiwa tangu Alhamisi katika maeneo ya Walungu na Kabare katika jimbo la Kivu Kusini kati ya wapiganaji wa AFC/M23 na Wazalendo.

Kule Walungu, mapigano hayo yamefanyika haswa katika vijiji vilivyoko kati ya eneo la Walungu/Centre na Kaniola na huko Kabare mapigano yamefanyika katika vijiji vinavyopatikana kati ya Kavumu na mbuga ya wanyama ya Kahuzi-Biega.

Baraza jipya la mawaziri bila vigogo wa upinzani​

Corneille Nangaa na Betrand Bisimwa viongozi wa kundi la waasi wa AFC/M23

Waasi wa AFC/M23 wameweka masharti kabla ya kurejea kwenye meza ya mazungumzo na seriakli huko DohaPicha: Ernest Muhero/DW

Mick Mutiki ni mwanaharakati wa Shirika la raia katika Jimbo la Kivu kusini, anazitaka pande zote kuweka kando hali yakujipendelea ubinafsi na kuendelea na mazungumzo hayo kwa maslahi ya wakongo.

"Tunachokiona sio cha kutia moyo. kila wakati inaturudisha kwenye mapigano tu ijapokuwa tulipoona saini tofauti huko Washington na Doha, tulianza kutumaini kwamba hatimaye tutapumua sasa lakini!!", amesikitika Mutiki.

Haya yakijiri, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Félix-Antoine Tshisekedi alitangaza muundo mpya wa serikali ya Kongo inayoongozwa na waziri Mkuu Judith Suminwa yenye mawaziri hamsini na tatu, dhidi ya ile yazamani iliyokuwa na mawaziri hamsini na nne. Ingawa mawaziri kadhaa wanahifadhi nyadhifa zao, marekebisho yamefanywa, na sura mpya zimejiunga na serikali hiyo.

Mfano ni waziri mkuu wazamani Adolphe Muzito aliyetajwa kwenye Wizara ya Bajeti, Floribert Anzuluni aliyeteuliwa kusimamia Mtangamano wa Kikanda, Guillaume Ngefa kwenye wizara ya sheria, huku Marie Niangé Ndambo akiwajibika kwa Mazingira.

Je, ni nani anayenufaika kweli na madini adimu ya Rubaya?​

1754665457997.png

07:40

Julie Mbuyi ataongoza Wizara Maalum ya nyazifa, Micheline Ombahe anateuliwa kwa Jinsia, Familia na Watoto, Grace Emi Kutinho anakuwa Waziri wa Vijana, na Eliezer Ntambwe ameteuliwa kuwa Waziri Mjumbe wa Ulinzi na Masuala ya Wanajeshi wa zamani.

"Ni serikali ya watu wamoja"​

Albert Matabaro ni msemaji wa chama cha upinzani cha ECIDé cha Martin Fayulu katika jimbo la Kivu kusini, anasema hatarajiye mabadiliko yoyote kufuatia Serikali hiyo :

"Sisi hatugemee kitu chochote sababu ni serikali inayoundwa na walewale ambao hawajali maslahi ya raia. Martin Fayulu hakukubali kuwa mwanachama wa serikali hiyo, kwa hivyo itashindwa muda sio mrefu", alisema Matabaro.

Wakongo wengine wanaamini kwamba ilikuwa ingekuwa heri kusubiri matokeo ya mazungumzo ya sasa kati ya AFC/M23 na serikali ya Kongo au mazungumzo mengine yanayotarajiwa chini ya uongozi wa maaskofu wa kanisa katoliki na kiprotestanti ECC-CENCO nchini Kongo ili kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.
 
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha D.W:​

Mazungumzo kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa AFC/M23 yameahirishwa kwa muda usiojulikana. Mazungumzo haya yalitarajiwa kurejea leo mjini Doha, Qatar.

Kombobild Felix Tshisekedi und Corneille Nangaa
Picha: Vlad Vanderkelen/Belga/picture alliance/Tony Karumba/AFP
Matangazo

Katika tamko hilo la kanuni zilizotiwa saini tarehe 19 Julai katika mji mkuu wa Qatar, pande hizo mbili ziliazimia kuanza mazungumzo ya amani ifikapo Agosti 8. Hata hivyo, hadi jana, hapakuwa na dalili ya kuanza kwa ufanisi wa mazungumzo hayo Ijumaa (08.08.2025). Alhamisi, AFC/M23 ilikuwa imetangaza tayari kwamba wajumbe wake walikuwa hawajaenda Doha.

Ujumbe wa serikali ya Kongo ulikuwa ungali bado mjini Kinshasa hadi asubui yaleo. Kwa upande wa AFC/M23, msimamo unaonekana kuwa mkali zaidi: wawakilishi wao walifika Alhamisi mjini Bukavu.

Ujumbe wa AFC/M23 umedai kwamba utarejea kwenye mazungumzo huko Doha ikiwa wafungwa wao waliozuiliwa na serikali ya Kongo wataachiliwa. Lakini serikali ya Kongo inaamini kwamba bado haujafika wakati wa kuwaachilia wafungwa hao, na kwamba hatua hii ni suala la mazungumzo yanayotarajiwa kufanyika moja kwa moja.

Wakati huo huo, takriban watu wanne wamepoteza maisha katika mapigano makali yaliyoripotiwa tangu Alhamisi katika maeneo ya Walungu na Kabare katika jimbo la Kivu Kusini kati ya wapiganaji wa AFC/M23 na Wazalendo.

Kule Walungu, mapigano hayo yamefanyika haswa katika vijiji vilivyoko kati ya eneo la Walungu/Centre na Kaniola na huko Kabare mapigano yamefanyika katika vijiji vinavyopatikana kati ya Kavumu na mbuga ya wanyama ya Kahuzi-Biega.

Baraza jipya la mawaziri bila vigogo wa upinzani​

Corneille Nangaa na Betrand Bisimwa viongozi wa kundi la waasi wa AFC/M23
Corneille Nangaa na Betrand Bisimwa viongozi wa kundi la waasi wa AFC/M23

Waasi wa AFC/M23 wameweka masharti kabla ya kurejea kwenye meza ya mazungumzo na seriakli huko DohaPicha: Ernest Muhero/DW

Mick Mutiki ni mwanaharakati wa Shirika la raia katika Jimbo la Kivu kusini, anazitaka pande zote kuweka kando hali yakujipendelea ubinafsi na kuendelea na mazungumzo hayo kwa maslahi ya wakongo.

"Tunachokiona sio cha kutia moyo. kila wakati inaturudisha kwenye mapigano tu ijapokuwa tulipoona saini tofauti huko Washington na Doha, tulianza kutumaini kwamba hatimaye tutapumua sasa lakini!!", amesikitika Mutiki.

Haya yakijiri, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Félix-Antoine Tshisekedi alitangaza muundo mpya wa serikali ya Kongo inayoongozwa na waziri Mkuu Judith Suminwa yenye mawaziri hamsini na tatu, dhidi ya ile yazamani iliyokuwa na mawaziri hamsini na nne. Ingawa mawaziri kadhaa wanahifadhi nyadhifa zao, marekebisho yamefanywa, na sura mpya zimejiunga na serikali hiyo.

Mfano ni waziri mkuu wazamani Adolphe Muzito aliyetajwa kwenye Wizara ya Bajeti, Floribert Anzuluni aliyeteuliwa kusimamia Mtangamano wa Kikanda, Guillaume Ngefa kwenye wizara ya sheria, huku Marie Niangé Ndambo akiwajibika kwa Mazingira.

Je, ni nani anayenufaika kweli na madini adimu ya Rubaya?​

View attachment 3436006

07:40

Julie Mbuyi ataongoza Wizara Maalum ya nyazifa, Micheline Ombahe anateuliwa kwa Jinsia, Familia na Watoto, Grace Emi Kutinho anakuwa Waziri wa Vijana, na Eliezer Ntambwe ameteuliwa kuwa Waziri Mjumbe wa Ulinzi na Masuala ya Wanajeshi wa zamani.

"Ni serikali ya watu wamoja"​

Albert Matabaro ni msemaji wa chama cha upinzani cha ECIDé cha Martin Fayulu katika jimbo la Kivu kusini, anasema hatarajiye mabadiliko yoyote kufuatia Serikali hiyo :

"Sisi hatugemee kitu chochote sababu ni serikali inayoundwa na walewale ambao hawajali maslahi ya raia. Martin Fayulu hakukubali kuwa mwanachama wa serikali hiyo, kwa hivyo itashindwa muda sio mrefu", alisema Matabaro.

Wakongo wengine wanaamini
wamba ilikuwa ingekuwa heri kusubiri matokeo ya mazungumzo ya sasa kati ya AFC/M23 na serikali ya Kongo au mazungumzo mengine yanayotarajiwa chini ya uongozi wa maaskofu wa kanisa katoliki na kiprotestanti ECC-CENCO nchini Kongo ili kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.
Kwani mgogoro aliyo usawazisha Trump kuhusu Rwanda na Congo DRC ulikuwa unahusu mambo gani?? Si mambo haya haya ya Rwanda/M-23 na Serikali ya Congo DRC,mbona kana kwamba tatizo hili linajirudia rudia tena??

Ni hivi: International Community ikifanya makosa ya kuendelea ku-entertain au kuwashirikisha wahuni hawa (M-23) kwenye mapatano/usuruhishi basi tukae tukijua kwamba Congo DRC na M-23 wataendeleza mambo ya vita vita tu wakichochewa na Rwanda,lakini Dunia ikichachamaa ika-deal na Rwanda kikweli kweli hamtasikia tena sijui M-23 sijui nini, Rwanda ndiyo inawapa jeuri/kichwa M-23 - kwamba wapuuzie makubaliano badala yake waendeleze vurugu ili Congo DRC hisitawalike mpaka wao watakapo shirikishwa kwenye mazungumzo kwani Congo DRC ina makabila mangapi?? kwa nini mara zote M-23 ujiona ni bora zaidi ya makabila mengine!! Wakati kila mtu anajua kwamba asili yao wala si Congo DRC wanaleta mambo ya usanii tu hapa.

Tunamshauri Tshekedi ajiongeze kidogo basi, inakuwaje anashindwa hata kuwaiga Wateliban wa Afghanistani walio shinda jeshi la uvamizi la Merikani, nawasii Wacogo mani wapunguze mambo ya starehe badala yake mjikite kupigania/komboa Taifa lenu, M-23 wana wachezea mara kwa mara kwa kuwa wamekwisha gunduwa kwamba nyinyi hamna umoja wala kuwa na hari ya kutaka kukomboa Taifa lenu dhidi ya wavamizi - kama VietNam ingekuwa na attitude kama za kwenu wangekuwa bado wako chini ya jeshi la Merikani mpaka sasa, kwa mara nyingine tena nawakumbusheni kwamba punguzeni mambo ya mayenu na ndombolo ya solo, komboeni Taifa lenu dhidi ya wavamizi kwanza! My opinion.
 
Ndiyo raha ya kuwa na jeshi, hulazimishwi kukubali ujinga.

Hamuelewani kila mtu kivyake.

Hapa kwetu kila kiltu ccm wamesema wameamua.
 
Naunga mkono hoja yako..

Anayeivuruga Drc anafahamika ila jamii ya kimataifa inakwepa kumwajibisha, huenda sababu wana maslahi naye
 
Kinacho wafanya waendeleze masuala ya vita visivyo kwisha linatokana na kugombea madini ya Coltan ambayo yanapatikana kwa wingi Congo DRC hata Rwanda wanayo lakini hayafikii kiwango cha Congo DRC, sasa M-23 wanacho kifanya ni ku-smuggle madini ya Congo DRG na kuyapeleka Rwanda, yakisha fika huko Rwanda yanasafirishwa kwenda kwenye soko la huko Ulaya na Merikani wenye viwanda vya kuunda vifaa vya kieletronic.
 
Back
Top Bottom