Kongole kwako Profesa Jay kuwa mtangazaji wa redio Clouds

Kongole kwako Profesa Jay kuwa mtangazaji wa redio Clouds

misimajumbasita

Senior Member
Joined
Jun 10, 2018
Posts
157
Reaction score
273
Pongezi kwako kwa maamuzi hayo ya kuwa mtangazaji bado ni fursa nzuri naomba nikutakie heri na wanaJF tumtakie heri mbunge huyu mstaafu wa Mikumi.

--
Clouds kupitia mitandao ya kijamii wameandika haya

Jana kwenye mitandao yetu ya kijamii tulisema leo kwenye #PowerBreakFast kwa mara ya kwanza utasikia sauti ya usajili mpya... Ladies and gentlemen na huyu @ProfessorJayTz ndiyo usajili mpya ndani ya PB.

J.jpg
J1.jpg
 
Ni mbunge wa zamani au aliyewahi kuwa mbunge sio mstaafu,huyo aligombea tena akashindwa kwa mujibu wa matokeo ya tume ya uchaguzi hakuwahi kustaafu naona hili neno kustaafu siku hizi linatumika vibaya.

Binafsi nawajua wabunge kadhaa waliowahi kustaafu mfano Marehemu Mzindakaya, Marehemu Sitta,Mzee Edger Majogo,Mzee Pinda hawa waliamua kuacha kugombea wenyewe baada ya kutumikia ubunge kwa muda fulani na wakafikia uamuzi wa kuachia wengine wabebe jukumu lakini sio hawa wanaogombea na kushindwa waitwe wastaafu.
 
Kwa upande mmoja nimpe pongezi kwa maamuzi binafsi ya kwenda kuwa mtangazaji clouds.

Ila kwa upande mwingine wa kwangu binafsi simpi pongezi kwa uamuzi aliofanya. Kwa level yake na hassle ya mda mrefu aliyofanya, mpaka kufikia kuwa mbunge, ametengeneza brand kubwa sana.

Nilitegemea atengeze ajira kwa vijana na angalau afungue redio yake binafsi! Kwa brand yake nina uhakika ingefanya vizuri sana.

Angekuwa amefanya la maana sana kuliko kwenda kuishi kwa masharti ya mwisho wa mwezi na kufanyia kazi mawazo ya mtu.

Profesa Jay,wee ni brand kubwa hebu jiongeze zaidi, acha hizo, wee ni role model wa vijana wengi, usiwaangushe!!
 
Wale ndugu zangu walio kunywa maji ya bendera ya vyama vyao vya siasa "......clouds CCM........ mimi si sikilizi Clouds sababu ni CCM......",haya sasa Prof J huyo mjengoni,sijui mtampokonya uwanachama.
 
Ni mbunge wa zamani au aliyewahi kuwa mbunge sio mstaafu,huyo aligombea tena akashindwa kwa mujibu wa matokeo ya tume ya uchaguzi hakuwahi kustaafu naona hili neno kustaafu siku hizi linatumika vibaya.
Binafsi nawajua wabunge kadhaa waliowahi kustaafu mfano Marehemu Mzindakaya, Marehemu Sitta,Mzee Edger Majogo,Mzee Pinda hawa waliamua kuacha kugombea wenyewe baada ya kutumikia ubunge kwa muda fulani na wakafikia uamuzi wa kuachia wengine wabebe jukumu lakini sio hawa wanaogombea na kushindwa waitwe wastaafu.
Umesema vyema kuwa alishindwa kwa mujibu wa tume lakini kiuhalisia alishinda
 
Back
Top Bottom