Kongole kwako Profesa Jay kuwa mtangazaji wa redio Clouds

Kwa upande mmoja nimpe pongezi kwa maamuzi binafsi ya kwenda kuwa mtangazaji clouds.

Ila kwa upande mwingine wa kwangu binafsi simpi pongezi kwa uamuzi aliofanya. Kwa level yake na hassle ya mda mrefu aliyofanya, mpaka kufikia kuwa mbunge, ametengeneza brand kubwa sana.

Nilitegemea atengeze ajira kwa vijana na angalau afungue redio yake binafsi! Kwa brand yake nina uhakika ingefanya vizuri sana.

Angekuwa amefanya la maana sana kuliko kwenda kuishi kwa masharti ya mwisho wa mwezi na kufanyia kazi mawazo ya mtu.

Profesa Jay,wee ni brand kubwa hebu jiongeze zaidi, acha hizo, wee ni role model wa vijana wengi, usiwaangushe!!
Kwa iyo anahamia dar, afu wakati wa uchaguzi anahamia Moro?
Kama vile Steve Nyerere na Massanja wapo Dar sasa ivi, wanasubiri uchaguzi mwezi mmoja kabla waende Iringa na kuanza kuhudhuria misiba.
 
Ni mbunge wa zamani au aliyewahi kuwa mbunge sio mstaafu,huyo aligombea tena akashindwa kwa mujibu wa matokeo ya tume ya uchaguzi hakuwahi kustaafu naona hili neno kustaafu siku hizi linatumika vibaya.
Binafsi nawajua wabunge kadhaa waliowahi kustaafu mfano Marehemu Mzindakaya, Marehemu Sitta,Mzee Edger Majogo,Mzee Pinda hawa waliamua kuacha kugombea wenyewe baada ya kutumikia ubunge kwa muda fulani na wakafikia uamuzi wa kuachia wengine wabebe jukumu lakini sio hawa wanaogombea na kushindwa waitwe wastaafu.
Hivi pinda si ni mgombea mstaafu?
Alishindwa kwenye kura za maoni urais ndani ya ccm ndio ikiwa basi mpaka sasa.
 
hawa nao ni kama walikua hawaweki akiba jmn mke mara mc mara muigizaji ye na utangazaji wapi na wapi c wamuone Jongwe awashauri agh
 
Kwa upande mmoja nimpe pongezi kwa maamuzi binafsi ya kwenda kuwa mtangazaji clouds.

Ila kwa upande mwingine wa kwangu binafsi simpi pongezi kwa uamuzi aliofanya. Kwa level yake na hassle ya mda mrefu aliyofanya, mpaka kufikia kuwa mbunge, ametengeneza brand kubwa sana.

Nilitegemea atengeze ajira kwa vijana na angalau afungue redio yake binafsi! Kwa brand yake nina uhakika ingefanya vizuri sana.

Angekuwa amefanya la maana sana kuliko kwenda kuishi kwa masharti ya mwisho wa mwezi na kufanyia kazi mawazo ya mtu.

Profesa Jay,wee ni brand kubwa hebu jiongeze zaidi, acha hizo, wee ni role model wa vijana wengi, usiwaangushe!!
Hakika
 
Hivi pinda si ni mgombea mstaafu?
Alishindwa kwenye kura za maoni urais ndani ya ccm ndio ikiwa basi mpaka sasa.
Nimemtaja kwenye ubunge, alikuwa mbunge kwa miaka kadhaa mwisho aliona astaafu ubunge kwani kama angekuwa na nia ya kuendelea na ubunge baada ya kupigwa chini kwenye urais nafasi ilikuwepo ya kugombea ubunge kama walivyofanya kina Mwigulu, Kigwangalla,January na wengine wengi.
 
Ni mbunge wa zamani au aliyewahi kuwa mbunge sio mstaafu,huyo aligombea tena akashindwa kwa mujibu wa matokeo ya tume ya uchaguzi hakuwahi kustaafu naona hili neno kustaafu siku hizi linatumika vibaya.
Binafsi nawajua wabunge kadhaa waliowahi kustaafu mfano Marehemu Mzindakaya, Marehemu Sitta,Mzee Edger Majogo,Mzee Pinda hawa waliamua kuacha kugombea wenyewe baada ya kutumikia ubunge kwa muda fulani na wakafikia uamuzi wa kuachia wengine wabebe jukumu lakini sio hawa wanaogombea na kushindwa waitwe wastaafu.
alistaafishwa na NEC, alisikika jamaa mmoja kutokea ufipa..
 
Kitaa sio poa huku pasikieni tu [emoji81] hasa ukiwa umetoka kwenye life la kupokea 300K kwa masaa!!! Acha ajishkize term ijayo agombee tena mikumi huenda akapata
Ila huyu c dhan Kama anafanyia njaa kwakweli
Na Kama hana biashara nyingine yoyote
Inayomuingizia pesa bas n ulembuken
Wake na mke alie nae
 
Back
Top Bottom