Kongole Rais kwa kumuondoa Abdu -Razak Badru pale PSSSF

Kongole Rais kwa kumuondoa Abdu -Razak Badru pale PSSSF

Mimi nafikiri wakitaka hii mifuko (PSSSF & NSSF) ipate ufanisi wa haraka wapewe Viongozi waliosoma enzi kukiwa na Internet, Namaanisha wapewe watu wanaoweza kuintegrate Internet, Digital Data base, Kitambulisho cha Nida/Passport na hivyo kumaliza kabisa tatizo la wastaafu kusumbuliwa.....kwa sababu kila kitu kitawekwa kwenye digital data base wakati mstaafu bado yupo kwenye ajira. Hii ya kudai mstaafu barua ya ajira aliyopewa miaka 30 iliyopita, sijui mkataba gani nk nk naona haijakaa sawasawa.....

Wakiunganisha hivyo pia kila kitu kinakuwa wazi na mfanyakazi anaweza hata kuandika miradhi yake ya mafao inawekwa huko hata akifa wana angalia tu faili lake mnufaika (mkewe/Mumewe/watoto) anapewa fungu lake bila longo longo....tofauti na sasa hela zinaweza kuwa zinabaki tu zina float...hazina mwenyewe kwa kuwa walalahoi wanafuatilia hadi wanachoka....na wajanja wanajichotea....
Wstaafu wanapima ufanisi wa ofisi kwa kupata huduma kwa urahisi/bila urasimu ambao unaweza kuondolewa kama kutakuwa na watu sahihi.
Pamoja na hayoyote, rushwa chuki na roho mbaya ndio vinawasumbua.
Kama wakiona vipi nao siwastaafu wachukue hela zao?
 
Ama kweli watanzania sio wafuatiliaji, bure kabisa! Badru kapelelwa pazuri zaidi - Ngorongoro. Na hii taarifa ilikuwa ktk press release ile ile ya kumuondoa PSSSF. It's unbelievable, watu hawana muda wa kuzingatia mambo
Haijalishi hata apelekwe kuzimu bora ameondolewa sehemu inayogusa maslahi ya watu wengi. Huyo ametesa wanufaika wa PSSSF
 
Back
Top Bottom