N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 8,308
- 12,812
Kuanzia Leonardo, yule jamaa wa "Tutakufuatilia", Eliud na mkewe, Koy Mzungu, Mama Mawigi, Mwenyekiti, Big na wenzie, Mlima Viazi Nziku kule Njombe, Wanyalu Tulizo na wenzie kitefu cha makani, Mwalimu wa Songea, rais wa mawinga na demu wake (huyu namcrush), Nyanda Kabundi (the lake zoner na chalii anemuigiza mako jako), street journalists wote wawili na wengine wengi ambao si rahisi kuwataja wote.
Mmetuonyesha kwamba ubunifu hauhitaji studio kubwa wala bajeti kubwa.
Kwa kutumia simu, mitandao ya kijamii na vipaji vyenu, mmeweza kutengeneza comedy inayogusa maisha ya kila siku na kutufanya tutabasamu hata siku ambazo zinaonekana nzito.
Pia hongereni kwa kizazi kipya cha watoto kama Mafuru, Nayan wa Mbalizi na wenzie, ambao nao wanaonyesha vipaji vyao kwa namna ya kuvutia.
Ni ushahidi kwamba ubunifu unaendelea kukua na si lazima uwe na studios kubwa za recording na dubbing Azm TV!!!.
Sijakusahau mdogo wangu unaesema Malawi sijui nini na nini!!!
Mbali na kuishukuru teknolojia iliyowapa jukwaa, pongezi kubwa ziende kwenu kwa uthubutu, ubunifu na uwezo wa kubadilisha matukio ya kawaida kuwa burudani inayounganisha Watanzania.
Mara nyingi mnatupunguzia mawazo na msongo wa mawazo kwa vichekesho vyenu kuliko tunavyotambua.
Ni tofauti pia na zama za akina mzee Jangala.
Wakongwe kama Mama Mawigi, Bambo na Mtanga, Mwenyekiti, Mama Imma nk nyie pia tunawapongeza kwa kuendana na zama, hamkuzika vipawa vyenu!!.
Endeleeni kuburudisha, lakini msisahau kuendelea kuheshimu maadili, utu na matakwa ya jamii zenu mnazozihudumia, wanachotaka wapeni!!.
Vipaji vyenu ni sehemu ya uchumi wa ubunifu (creative economy) na mchango muhimu katika maendeleo ya taifa na famili zenu!.
Hongereni Gen Z!
Mnafanya Watanzania wenzenu watabasamu kila siku. 👏🇹🇿
Uzi huu ni kutoka kwa millennial anaetambua kazi yenu nzuri...endeleeni!!!