Korea Kaskazini imefanya majaribio ya makombora

Korea Kaskazini imefanya majaribio ya makombora

HERY HERNHO

Senior Member
Joined
Mar 4, 2022
Posts
110
Reaction score
458
Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimesema urushaji huo wa makombora ambao uliothibitishwa na jeshi la Korea Kusini, ulikusudiwa kuthibitishwa kutegemewa kwa makombora hayo na uwezo wa kujibu kwa haraka kitengo kinachoongoza silaha hizo.

Shirika la habari la Pyongyang limeripoti kwamba makombora hayo manne yaliruka kwa karibu saa tatu baada ya kurushwa kutoka pwani ya kaskazini mashariki, yalionesha yanaweza kulenga shabaha kilometa 2,000.

Hata hivyo taarifa ya pamoja kati ya Korea Kusini na mshirika wake Marekani zimekosoa juu ya taarifa hiyo bila kufafanua zaidi.chanzo dw swahili
 

Attachments

  • 64806378_803.jpg
    64806378_803.jpg
    34 KB · Views: 5
Mwenzake putin alikuwa anasogea vinu vya nuclear kila mara alipovamia Ukraine sasa majigambo na ndaro zote kwisha anatumia makundi ya kigaidi vitani ata jeshi hana
Khe kumbe nyie ndio mnaodanganywa na propaganda za Marekani na.washirika wake😃️😃️😃️😃️. Kwa hiyo Ukraine kashinda Vita? Nchi imechakaa Kama tambara bado hamuoni?
 
Vita ya North na South itakuwa mbaya sababu North ana artillery systems nyingi sana na hana chakupoteza. Kitu pekee kizuri ni kumfanyia Pre emptive strikes

Ila inabidi wajipange haswa.

Ipo siku itatokea tu, ni swala la muda
 
Wababe wa dunia wanamhofia. Wewe uko hapo Kisiju unamuita "coward".

A coward with nukes is no coward at all!
Hizo nukes mkuu ni mwendo wa kuzimwa within, lini umesikia US wakijaribu silaha za maangamizi
 
Vita ya North na South itakuwa mbaya sababu North ana artillery systems nyingi sana na hana chakupoteza. Kitu pekee kizuri ni kumfanyia Pre emptive strikes

Ila inabidi wajipange haswa.

Ipo siku itatokea tu, ni swala la muda
Hiyo siyo vita ya s na n korea ni vita ya NK na USA kiduku ana jiandaa kivita na marekani ndiyo maana anaunda makombora yenye kufika usa pia marekani kumshinda kivita kiduku ni vigumu sana
 
Hiyo siyo vita ya s na n korea ni vita ya NK na USA kiduku ana jiandaa kivita na marekani ndiyo maana anaunda makombora yenye kufika usa pia marekani kumshinda kivita kiduku ni vigumu sana
Kumbe hujui, ni Vita ya China na USA kupitia proxies, financier wa NKorea ni China na Russia, hawataki awe defeated maana akiwa Defeated zile THAAD zinawekwa hapo hapo NKOrea
 
Hizo nukes mkuu ni mwendo wa kuzimwa within, lini umesikia US wakijaribu silaha za maangamizi
Kwanini wanazilalamikia kama zinaweza kuzimwa?

Hao wanaozihofia wanajua kitu ambacho wewe hujui.
 
Mwenzake putin alikuwa anasogea vinu vya nuclear kila mara alipovamia Ukraine sasa majigambo na ndaro zote kwisha anatumia makundi ya kigaidi vitani ata jeshi hana
Wenzako wanatumia akili nzito wewe unatumia nyepesi utaelewa nini kuhusu haya!

Haya mambo si ya ki political au ideological! Hizi ni kanuni za kivita. Russia ni taifa kongwe kuliko Marekani.

Limepigana vita nyingi mno na vita kubwa! Ukubwa wake wa km za mraba hazikupatikana kwa sababu hayo maeneo ni baridi bali kwa vita.

Hivyo, huwezi kulishinda au kulielekeza kivita jinsi gani ya kuendesha mashambulizi yao au nini cha kufanya! Wewe umepigana vita gani na ngapi?

Na Ukraine ipi inayoifanya Russia isilale wakati ndani ya nchi ya Russia raia wanaendelea na maisha yao kama kawaida?!

Kama unayoakili ya kufikiri kwa nini Russia ilipotangaza kujitoa kwenye makubaliano ya Strategic Arms Reduction Treaty (START) Mkurugenzi Mkuu wa NATO, Biden na Blinken Katibu Mkuu wa Marekani kwa nini wamelalamika kwa pamoja na kutoa masikitiko yao Russia kujitoa huko kwenye START III?

Unazungumza nini humu zaidi ya kutuletea ngano za pauka pakawa?

Kama hujui North Korea na USA ni karibu sana kijiografia. NK wakirusha kombora la nuclear linatua New York City ndani ya dakika 30 na hizi takwimu ni za miaka takribani 4 iliyopita, vipi kwa sasa?

Licha ya majaribio yote anayoyafanya kwa nini hawamvamii? Kwa nini wanaishia kumlaani tu?

Unajua ya kwamba manuari ya kivita ya North Korea ilishawahi kuvuka mpaka baada ya kupata hitilafu na kuingia Gangneung South korea? South Korea ilipeleka wanajeshi 43,000 kupambana na wanajeshi wa North Korea 26 na mapambano yalichukua siku 49.

Kim Jong ill baba wa kiongozi wa sasa wa NK alimwambia Bush ajaribu kuivamia NK tena kama miaka ya nyuma aone. Na wao watahakikisha Bush atasomeka kama Rais mjinga aliyewahi kutokea America na atakayesomwa vizazi na vizazi.
 
Ni tishio kwa nchi nyengine zisizo na technologia
Nani mwenye means of delivery nzuri za hayo makombora? Russia ina makombora wa kufika UK chini ya dakika 2 ya nuclear. Unazungumzia nini wewe?

Unafikiri rais Macron ni mjinga kusema hatoingia kupambana na Russia kwenye vita ya nuclear?

Baada ya USSR kuvunjika makachero wengine waliyodondokea kwenye nchi za NATO walitoa siri kuwa Russia ina mfumo unaoitwa DEAD HAND ni automatic nuclear weapons-control system. Hata uilipue Russia yote kwa nuclear huo mfumo unajiendesha wenyewe na kurudisha mashambulizi kwa wahasimu wao.

Putin alipofanyiwa interview aliwaambia west. Hata kama mkitushambulia DEAD HAND itafanyakazi yake, na watahakikisha West wote wanaenda kuzimu kwani hawatowaachia hata muda wa kufanya toba/kutubu.

Russia imeshajiweka tayari kwa lolote, ngoja west wakosee mahesabu na waone kitakachowajia.
 
Back
Top Bottom