GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Kwa jinsi Iran inavyosigana na mataifa makubwa kama Marekani, inaweza kuleta picha kuwa ni nchi hatari kuishi. Lakini ukifuatilia taarifa za hapa Tanzania, ni wazi kuwa nchi ya Tanzania na Iran hazijawahi kuhasimiana. Hata kipindi fulani, Iran iliipatia Tanzania msaada wa matrekta madogo 100. Imeshatoa na misaada mingine pia.
Rais wa Korea Kaskazini anadaiwa kuwa ndiye dikteta katili duniani. Lakini nchi yake haina ugomvi na Tanzania. Baba wa Taifa hilo alikuwa rafiki wa hayati Nyerere.
Nchi zote hizo mbili zina mabalozi Tanzania, lakini nafikiri Tanzania haina mabalozi kwenye nchi zao.
Kwa muktadha huo, hizo nchi ni salama kwa Mtanzania?
1. Mtanzania anaweza kuishi huko na kufanya shughuli zake halali kwa amani bila kubaguliwa?
2. Kutokana na hizo nchi kutokuwa na uhusiano mzuri na mataifa ya Kimagharibi, hatuwezi kutumia huo mwanya kama fursa ya kiuchumi kwa kufanya nao biashara?