Shing Yui
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 15,168
- 38,049
Korea Kaskazini yafyatua makombora ya masafa marefu katika bahari ya Japan
CHANZO CHA PICHA, REUTERS. Maelezo ya picha: Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini amerudia kufanyia majaribio makombora ya masafa marefu
Korea Kaskazini imefyatua makombora mawili ya masafa marefu ndani ya bahari ya Japan, zimesema Marekani na Japan-likiwa ni jaribio la kwanza la aina hiyo tangu Joe Biden awe rais wa Marekani.
Pyongyang ilizuiwa kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu, ambayo yanaangaliwa kama silaha za kutisha, chini ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Japan imesema kifusi kimeanguka ndani ya eneo lake la maji.
Hii inakuja siku chache tu baada ya Korea Kaskazini kufyatua makombora yasiyo ya Bahari ya Manjano.
Waziri mkuu wa Japan Yoshihide Suga amesema Alhamisi kwamba majaribio hayo yanaleta tisho kwa usalama na amani kwa nchi yake pamoja na kanda hiyo nzima.
Taarifa ya pamoja kutoka kwa wakuu wa jeshi nchini Korea Kusini awali ilisema makombora hayo yalirushwa kutoka katika "kitu ambacho hakijatambulika ".
Bw Biden bado hajatoa taarifa rasmi kuhusu jaribio la hivi karibuni la Korea Kaskazini.
Siku ya Jumanne alipuuza ufyatuaji wa makombora yasiyo ya masafa marefu yaliyorushwa mwishoni mwa juma, akisema kuwa Marekani haikuchukulia jaribio hilo kama uchokozi. Makombora hayo ya masafa mafupi yalidhaniwa kuwa ya kutumia roketi au ni ya masafa marefu ambayo kwa kawaida hulenga eneo fulani, ambayo hayajapigwa marufuku na Baraza la Usalama laUmoja wa Mataifa.
Jaribio hili lina maana gani?
Hili ni jambo kubwa sana kwa Marekani na washirika wakeJaribio la mwishoni mwa juma la makombora ya yasiyo ya ballistic linaweza kupuuzwa. Lakini jaribio hili la makombora ya ballistic ni ukiukaji wa wazi wa vikwazo vya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Kwa kusema hivyo, mtangulizi wa Bw Biden Donald Trump hakutaka maswali yoyote kuhusu jaribio la silaha sawa na hizo mwaka 2019.
Mkataba baina ya Bw Trump na Kim Jong-un uliofikiwa nchijni Singapore mwaka 2018 ulikuwa kwamba Pyongyang haitajaribu makombora ya masafa marefu ya ballistic au silaha za nyuklia.
Wakati ule, Ikulu ya White House haikujihusisha na majaribio madogo zaidi ya makombora.
Lakini maafisa wa Bw Biden ndio wametoka tu nchini Japan na Korea Kusini, na kuahidi kuwa "Marekani imerejea" na inawaunga mkono washirika wake.
Labda sasa, utawala Biden, utatakiwa kutoa tamko kuhusu jaribio la silaha ambazo zinatishia marafiki zake Kaskazini mwa Asia.
Washington ia itatambua kuwa Pyongyang ina silaha kubwa katika gala lakeambazo haijazifanyia majaribio tangu mwaka 2017.
North Korea imetengwa kwa mwaka mmoja. Hata iliamua kukata biashara zake nyingi na mshirika wake mkuu China kutokana na janga la Covid-19 , na uchumi wake unasemekana kuwa katika hali mbaya.
Sasa wakati ikionekana kurejesha majaribio yake ya silaha, wengi wanashangaa ni kwa kiwango gani anachotaka kukifikia Bw Kim Jong-un ili kuweza kuutishia utawala wa Marekani.
Majaribio haya yanafanyika huku utawala wa Biden ukiendelea kujaribu kufanya mawasiliano ya kidiplomasia na Korea Kaskazini.