Korea Kusini: Viwango vya Uzazi vyazidi kushuka. Hofu ya kutoweka kwa Taifa yaibuka

Ni kweli Mkuu, tukiendelea na haya maigizo ya family planning baada ya miaka 50 ijayo huenda yakatukuta ya wenzetu huko
 
Ni kweli Mkuu, tukiendelea na haya maigizo ya family planning baada ya miaka 50 ijayo huenda yakatukuta ya wenzetu huko
Ttz serikali zetu hizi zmejaa rushwa,ubinafsi na roho mbaya.

Zikishafeli kimipango, zigo lote anabebeshwa raia wajitafte wenyewe.
 
South Korea ina ukubwa kama Morogoro na Dodoma pamoja ina watu milioni 51, Tanzania ina watu milioni 61.
 
Ni upumbavu kuzaa watoto ili wakapigane vita.
 
Sa utajuaje km kwenye maisha yako unaweza kutunza idadi flani ya watoto wakati maisha huwa yanabadilika ? Na hata tukichukulia maisha yako ni magumu ukaacha kuzaa nani atakusaidia ukizeeka !?
Ni ujuha kuzaa watoto ili wakusaidie ukizeeka,
Je hao watoto wakiwa masikini kuliko wewena wakahutqji msaadq wako hata ukiwa mzee??
 
Hahaha..............nimetania Mkuu πŸ˜…

Ila suala la kuzaa lipewe kipaumbele, bado Nchi yetu imejaa mapori ambayo hayana watu
Sio kweli kwamba nchi yetu imejaa mapori yasiyo na watu, kusingekuwa na migogoro ya kugombania na kutapeliana ardhi karibu nchi nzima.
 
Wapenzi pia walitaja mzigo mkubwa wa kifedha kama kizuizi cha ndoa, ambayo inachukuliwa kama sharti la kuwa na Watoto
Hawa wamechoka, kuzaa na ndoa vina uhusiano gani? Waje huku wafundishwe na Ma-single maza, unaweza kuzaa na yeyote na maisha yakaenda.
 
Ni ujuha kuzaa watoto ili wakusaidie ukizeeka,
Je hao watoto wakiwa masikini kuliko wewena wakahutqji msaadq wako hata ukiwa mzee??
Ujuha mbaya ni kudhani kuwa masikini hawezi kumsaidia mtu, lkn ujuha mbaya zaidi ni kudhani msaada ni pesa tu, unatakiwa ujue kuwa hata kuuguzwa wakati wa maradhi pia ni msaada.
Ukiwa huna watoto, ni masikini na unamaradhi jua umeyaingia mateso yasiyo vumilika, yani angalau uwe na pesa unaweza ukajimudu.

Hivi unapata picha gani katika familia ambayo inaishi na wazazi wawili tu hakuna mtoto hata wa kumwambia nenda dukani, safisha uwanja nk. Na hapo una 50/60 yrs, unaishije ? Au ndo utaita watoto wa jirani wakusaidie kuanua nguo zako ? Nahapo nimekupeleka tu kwenye miaka hiyo, lkn hata uwe na age ya miaka 30 ukiwa na familia tu lazima utahitaji mtu wa kukusaidia , na hakuna zaidi ya mtoto.
 
Ni ujuha kuzaa watoto ili wakusaidie ukizeeka,
Je hao watoto wakiwa masikini kuliko wewena wakahutqji msaadq wako hata ukiwa mzee??
Na hata tukirudi kwenye msaada wa kipesa, mtoto anahaki ya kumsaidia baba yake alichokikosa ikiwa ye anacho.
 
Ni ujuha kuzaa watoto ili wakusaidie kukuuguza, kununua nyanya dukani, kuanua nguo n.k. Hutakiwi kuzaa watoto kama pension yako ya msaada wowote.
 
Na hata tukirudi kwenye msaada wa kipesa, mtoto anahaki ya kumsaidia baba yake alichokikosa ikiwa ye anacho.
Mtoto hana haki au wajibu wa kumsaidia baba yake alichokikosa, anaweza kufanya hivyo kama hisani tu ila sio lazima. Tuache kukariri maisha ya kijima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…